Leo Mei 27, 2025, The Chanzo imepokea wito kutoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuhusu maudhui ya video tuliyochapisha katika chaneli yetu ya Youtube, ambayo ni mkutano na waandishi wa habari mazungumzo aliyoyafanya Askofu Josephat Gwajima, Mbunge wa Kawe (Chama cha Mapinduzi – CCM), mnamo Mei 24, 2025.
Kutokana na mazungumzo hayo kuendelea kufuatiliwa, ili kuboresha uwazi, na imani ya wafuatiliaji wetu, The Chanzo inapenda kuwajulisha wasomaji na wadau wake wengine kuwa imetubidi kuyaondoa maudhui hayo kutokana na wito huo.
Sehemu ya taarifa tuliyopokea kutoka TCRA inaeleza:
“Maudhui hayo yaliyopakiwa na Chanzo Online TV yalikuwa ni maelezo ya mtu aliyejitambulisha kwa jina la Josephat Gwajima, hayakufuata Sheria, Kanuni, Maadili wala Misingi ya Uandishi na Utangazaji wa Habari kutokana na kukosa mizania/kuwa na taarifa za upande mmoja tu bila ya kuwapa nafasi upande wa Serikali au Mamlaka husika kutolea ufafanuzi shutuma au taarifa kuhusu idadi ya watu waliodaiwa kutekwa kama ilivyodaiwa katika taarifa husika. Kitendo cha Chanzo Online TV kupakia taarifa zenye kuegemea upande mmoja kinaweza kuhamasisha au kuchochea chuki dhidi ya Serikali kutoka kwa wananchi wake.”
Wakati ni nadra wito wa namna hii kutokea, kutokana na wito huu kutoka TCRA, leseni ya maudhui inatutaka kuyaondoa maudhui hayo; jambo ambalo tumelifanya leo Mei 27, 2025, 10:09 asubuhi.
One Response
Nilijua TU hili ni lazima litokee,maana watu wa Leo ama serikali zetu za Africa nyingi hazipendi kuusikia ukweli Bali sifa na nyimbo za kupingezwa
Ninyi mmefanya kazi yenu ya kiuandishi na hakika video bado tunayo na mazungumzo yote yapo,hivyo hawajafanya lolote😆😆😆
Nawapongeza sana the Chanzo