The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Kesi ya Uhaini Juni 16, 2025: Tundu Lissu Aamua Kujiwakilisha Mwenyewe, Aeleza Vikwazo Mawakili Wake Walivyokutana Navyo

Kutokana na malalamiko ya kukosa faragha na mawakili wake, Tundu Lissu aliamua kuanzia leo kuendelea mbele atakuwa akijiwakilisha mwenyewe, jambo ambalo Mahakama imeliridhia.

subscribe to our newsletter!

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu imeendelea leo Juni 16, 2025, ikiwa katika hatua za awali za kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga.

Katika kesi hii, Tundu Lissu ameilalamikia Mahakama kutokupata haki ya faragha ya kuongea na Mawakili wake awapo gerezani, lakini pia kuwekwa katika eneo la wafungwa waliohukumiwa kunyongwa, huku akihudumiwa kama mfungwa anayesubiri kunyongwa.

Tundu Lissu pia alilalamika kuwa amekuwa akinyimwa haki yake ya kuabudu, lakini pia ameieleza Mahakama wafungwa wote wanaosubiri kunyongwa wamekuwa wakinyimwa haki hiyo inayotolewa kisheria. Kufuatia malalamiko hayo Mahakama ilijibu kuwa imepokea taarifa hiyo na kueleza kuwa, yatafuatiliwa kwa njia za utawala.

Kutokana na malalamiko ya kukosa faragha na mawakili wake, Tundu Lissu aliamua kuanzia leo kuendelea mbele atakuwa akijiwakilisha mwenyewe, jambo ambalo Mahakama imeliridhia.

Yafuatayo ni mazungumzo yote yaliyotokea Mahakamani leo Juni 16, 2025:

[Baada ya utambulisho wa Mawakili, Tundu Lissu ananyanyua mkono wake, kuomba ruhusa ya kuongea]

Wakili Mpale Mpoki [Utetezi]: Naona mshtakiwa amenyoosha mkono.

Hakimu: Umemruhusu aongee.

Mpoki: Yes. Tumemruhusu

Hakimu: Karibu. Asante mheshimiwa. Mheshimiwa

Hakimu: Ngoja ngoja kwanza tuko kwenye Corum tuko kwenye Corum ah unataka kuongelea kuhusiana na corum

Lissu: Nataka kuzungumza kuhusiana na mawakili wangu nawakili wangu na namna tunaenda tunavyoenda mbele

Hakimu: Tumalize kwanza kwenye corum

Mpoki: Nimeshamaliza kwenye corum

Hakimu: Umemaliza, sawa jamhuri?

Nossoro Katuga [Wakili Mkuu wa Serikali] : Mheshimiwa mshtakiwa yupo na shauri kwa ajili ya kutajwa

Lissu: Mheshimiwa kama ambavyo nimedokeza nataka kuzungumza juu ya uwakilishi wangu kwenye mashauri haya na nitakachokisema mheshimiwa naomba nirekodiwe sawasawa na Mahakama yako. Mheshimiwa nina mawakili kwa hesabu ya haraka haraka kwa jinsi walivyolitambulisha nina mawakili zaidi ya 30.

Hakimu: Yes.

Lissu: Na mawakili hawa Mheshimiwa Hakimu niliwachagua mimi mwenyewe ni mawakili wangu na niliwachagua kwa sababu nina imani nina full confidence na uwezo wao wa kuniwakilisha katika mashauri haya,  katika kesi hii. Wengi wao, nimefanya nao kazi; hawa wazee wawili hawa mzee Alute na mzee Mpale Mpoki  wamenilea mimi, kitaaluma na vile vile kwa kesi ya mzee Alute amenilea literaly, ndiye  amechukua nafasi ya mzee Lissu ni mawakili ambao kwa miaka yote ambayo nimewafahamu wana uwezo mkubwa sana, full confidence.

Sasa mheshimiwa hakimu; leo hii, hapa tulipo ni siku ya 68 tangu nilipoletwa mbele ya mahakama yako tukufu na kusomewa mashtaka ya uhaini. Siku 68, na toka siku niliposomewa mashtaka ya uhaini mheshimiwa uliamuru nipelekwe magereza, magereza nikawe mfungwa mahabusu na kwa siku 68 hizi nimekuwa mahabusu kwa wiki moja gereza la Keko na tangu Ijumaa kuu nimekuwa kwenye gereza kuu la ukonga, siku 68 katika hizi siku 68 mheshimiwa mawakili wangu hawa wamekuja kunitembelea gerezani ili tushauriane namna ya kukabiliana na mashaka hayo hajaacha kuja mahakamani, hawajaacha kuja magereza.

Na muda wote ambao wamekuja katika hizi siku 68, hawajaruhusiwa, hawajaruhusiwa kuniona na kuwasiliana na mimi in-confidence, hawajaruhusiwa kuonana na mimi na kuzungumza na mimi kwa faragha. Kitu ambacho kimetokea mheshimiwa ukiingia kwenye gereza kuu la Ukonga unapopita reception kuna kachumba, kulia kwako hivi, hako kachumba kamegawanywa mara mbili kamegawanywa na ukuta wa kioo, ukuta wa  kioo. Kwa hiyo wanapokuja wanasimama nyuma ya kioo upande wa reception na reception iko nyuma yao kidogo na mimi nasimama upande mwingine wa kioo tunawasiliana kwa simu na mawakili, tunawasiliana kwa simu, hakuna fursa ya kubadilishana nyaraka; na mimi nina manyaraka mengi sana. Hakuna fursa ya kuandika chochote kwa sababu hakuna meza ya kuandikia. Hakuna kiti. Mnazungumza kwa simu

Sasa mheshimiwa; nimedai sana kwa Mkuu wa Gereza, kwamba kama mfungwa mwenye Mawakili nina haki, narudia nina haki ya kuonana na mawakili in-confidence, ni haki. Sio mapenzi ya bwana jela, ni haki kama ambavyofafanua hapa na bwana jela amenikatalia; in fact Mheshimiwa Hakimu kuna wakili mmoja alimtembelea hapa nikapiga nikapiga kelele sana, bwana jela, akaniambia kama unaona simu haiwezekani njoo ukae hapa reception. Reception palipojaa maafisa wa magereza muongee. Yeye yuko upande wa pili wa hili lile lango la grill la chuma.

“Sasa mheshimiwa; nimedai sana kwa Mkuu wa Gereza, kwamba kama mfungwa mwenye Mawakili nina haki, narudia nina haki ya kuonana na mawakili in-confidence, ni haki.”

 Yuko upande wa pili mimi niko upande wa gereza tunazungumza, maafisa wote wa magereza kama walivyo hapa wananiangalia kila mtu anasikiliza tunachozungumza. Kila Afisa wa Magereza anasikiliza ninachozungumza. Bwana jela amesema mzungumze pale na wakili na kwenye simu mheshimiwa hiyo simu anaisikiliza nani mwingine nani anayejua kwamba kuna mtu mwingine huko anayesikiliza tunachozungumza, nani anayejua kwamba kwenye control room hakuna vinasa sauti hakuna bugging instruments kufanya nini, kunasa mazungumzo yangu na mawakili sasa mheshimiwa twende kwenye sheria, twende kwenye sheria kwa sababu hii ni mahakama ya sheria.

Mheshimiwa nataka nikusomee kanuni ya 13 kanuni, regulation 13 ya prisons, prison management regulations 1987; prisons in brackets prison management regulations 1987, government notice number 6 of 1987, GN 60 of 1987 inasema hivi, naisoma kwa kiingereza na nitaizungumza kwa Kiswahili hii umma huu wasikilize yanayo endelea gerezani: Every prisoner shall be given all reasonable opportunities of communication with legal advisor or with such other person as the officer in charge may approve as representing the interests of the prisoner and visit to a prisoner by the legal advisor or such other person shall take place within the site but out of hearing of the prison officer. Within site; out of hearing, out of hearing.

Sasa mheshimiwa, hii principle, hii kanuni kuu kwamba wakili na mshtakiwa wanatakiwa wasisikilizwe maneno wanayoyazungumza na mtu mwingine yeyote ni sehemu ya sheria kuu za kimataifa mheshimiwa Hakimu. Na nataka nisome the body of principles for the protection of all persons under any form of detention or imprisonment. Hizi body of principle zinaitwa maarufu kama the Mandela principle, kanuni za Mandela zilipitishwa, zilipitishwa kwa resolution of the General Assembly of the United Nations resolution number 43/173 of 9th December 1988, kanuni kuu kuhusu ulinzi wa watu wote ambao wako mahabusu, detention au wamefungwa. They are in prison. Sasa tuvumilie kidogo mheshimiwa, principle 18; kanuni ya 18 ya Mandela principles 18 (i) A detained or imprisoned person shall be entitled to communicate and consult with his legal counsel. Two, a detained or imprisoned person shall be allowed adequate time and facilities for consultations with his legal counsel. Three, the right of a detained or imprisoned person to be visited by and to consult and communicate without delay or censorship and in full confidentiality with his legal counsel may not be suspended or restricted serve in exceptional circumstances to be specified by law or lawful regulations when it is considered indispensable by a judicial or other authority in order to maintain security and good order.

Hizi kanuni zinasema that that word other authority ni mahakama vile vile sio bwana jela, sio bwana jela anayeamua; ni mahakama ndio inayoamua usionane na mawakili uwekewe vizingiti vya kuonana na mawakili ni mahakama na nitakuja kwenye mahakama yako mheshimiwa. Sasa mheshimiwa Kwa hiyo tunazungumza four (iv) ni muhimu; interviews between a detained or imprisoned person and his legal council mentioned in this principle […………………].

Mheshimiwa haki ya kwanza niliyonayo kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa magereza ni haki ya kuabudu Mungu. Haki ya ibada kanuni ya 14 ya hizi kanuni ya hizi prison management regulations, na vile vile iko kwenye Mandela principle nitakuletea baadaye nina haki ya kuabudu mheshimiwa. Kila Jumapili, wakristo na mimi ni mkristo, wakristo wanafanyiwa ibada; gereza kuu la ukonga, every Sunday na kwenye sikuu za za za Kikristo wafungwa wanafanyiwa ibada gerezani.

Mimi nilikwenda, nilipelekwa Ukonga siku ya Ijumaa kuu asubuhi, ijumaa kuu. Na nilipopokelewa immediately nilimuomba mkuu wa gereza nikasali, sala ya ijumaa kuu akakataa. Jumapili ya Pasaka nikamwambia mkuu wa gereza nataka niende nikasali. Jumapili ya pasaka akakataa. Jumatatu ya pasaka, bwana jela nataka niende kusali. Akakataa na amekataa. Nimeomba na amekataa kila jumapili including ya jana. wafungwa wengine wote, wanakwenda kusali isipokuwa mimi na wengine ambao nitawataja hapa muda si mrefu, isipokuwa mimi.

Kanuni ya 14 inasema: ‘a minister of religion that is 14(i) a minister of religion shall be admitted at proper and reasonable times to a prison to visit prisoners. Mtu kiongozi wa kiroho ataruhusiwa gerezani kwa muda unaofaa kutembelea wafungwa sio kwenda kuwaambia habari gani? Hakuna chai kule wala kunywa nao chai kwa sababu hamna chai. Ni kwenda kuwapa huduma ya kiroho. Waislamu every Friday sisi Wakristo every Sunday and every Christian holiday wote wanakwenda isipokuwa huyu mhaini ambaye hawezi hata kuomba Mungu, hatakiwi sio hawezi hatakiwi kuomba hata kuomba Mungu. 14(ii)A  minister of religion shall be permitted to hold religious services at such hours and in such places as the officer in charge may permit and the officer in charge shall make such arrangements for the holding of religious services and for the religious instruction of prisoners shall not in any way interfere with the routine and administration of the prison. Tunaruhusiwa kufundishwa dini kama hujabatizwa au hujapata kipaimara au komunyo utafundishwa hayo mambo ili ubatizwe au upate kipaimara au uwe unapata mwili wa Bwana. It is the law.

Na tatu inasema the attendance of prisoners at religious services and religious instruction shall be voluntary. Sio lazima. Hatulazimishwi kwenda kanisani. Unaenda ukitaka mimi nimetaka nimekataliwa kwa siku 68. Kwa hiyo, my right of worship has been monstrously violated. Haki yangu ya kuabudu imekiukwa vibaya sana. haki yangu ya kisheria na nimewaambia mawakili wangu throughout wamenipambania sana  imeshindikana.

“Haki yangu ya kuabudu imekiukwa vibaya sana. haki yangu ya kisheria na nimewaambia mawakili wangu throughout wamenipambania sana, imeshindikana.”

La tatu, mheshimiwa hivi ninakaa wapi gerezani? Ninakaa wapi gerezani? Ukonga. Mheshimiwa Hakimu, Mheshimiwa hakimu, gereza la Ukonga lina sehemu kuu mbili. Kuna sehemu ambayo wafungwa wote waliohukumiwa maisha, miaka 30, miaka mitano, mahabusu na nini wanakaa wanatakiwa wakae. Halafu kuna sehemu moja inaitwa special wing,  eneo maalum ambalo wanakaa wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa. Mimi nakaa kwenye hiyo sehemu wanaokaa wanaosubiri kunyongwa. Nakaa death row. Nimewekwa death row.

Sasa mheshimiwa ukiwa death raw maana yake ni nini? Nataka nikusomee sheria maana ya kuwa death raw. Kanuni ya 33 inazungumzia wale walioko Death Row. Walioko Death Row inasema hivi; not withstanding anything contained in these regulations, a prisoner and a sentence of death shall (a) be confined apart from other prisoners and shall be under the constant supervision of two prison officers by day and by night. Ukikaa Death Row mheshimiwa kama navyokaa mimi wakati sijahukumiwa kifo angalau bado pengine tutafika huko lakini bado sheria inasema wanaokaa deathraw wale waliohukumiwa kifo wanatakiwa watenganishwe na wafungwa wengine. wafungwa wengine wote.

Mimi nimekaa Death Row tangu Ijumaa kuu mpaka hapa tulipo. Na nikitoka kwenda kuonana na mawakili wangu au kwenda kuonana na ndugu zangu nafuatana na Askari wawili muda wote kama inavyotakiwa kwa waliohukumiwa kifo. Kama walivyo ambao wako under constant surveillance sheria inasema by day and by night mimi sio sijahukumiwa kifo lakini nakaa death row and I’m under constant surveillance by day and by night.

Ukiwa death row, mheshimiwa kama ambavyo nimekuwa ukiwa death row pamoja na kuwa death row bado una haki bado kuna; una haki kwa mujibu wa sheria hii hizi, kwa mfano, kwa mfano nilizungumza habari ya haki ya kuabudu sio? Haki ya kuabudu: a prisoner a sentence of death shall be permitted to receive visits by a minister of the religious denomination to which the prisoner belongs kwa hiyo hata wa death row wana haki ya kuabudu wote wanakataliwa wote na mimi.

Ukiwa death row pamoja na kuwa umehukumiwa kifo, sheria inasema a prisoner under the sentence of death shall be allowed such amount of exercise as the commissioner may direct wanaruhusiwa kufanya mazoezi, kufanya mazoezi kwenye chumba changu ninakokaa mheshimiwa hapo death row. Death row imezungukiwa na ukuta hivi nyuma tu ya chumba ya selo ninayokaa ni uwanja mkubwa wa mpira wa miguu na wafungwa kila siku wanacheza mpira wanatembea wanaotaka kutembea wanakimbia wanaotaka kukimbia wanafanya mazoezi wanaotaka kufanya mazoezi isipokuwa walioko death row, wa death row hawatoki nje ya death row hawana fursa ya mazoezi ambayo sheria imesema wanaruhusiwa kufanya mazoezi.

Sasa mie siwezi kucheza mpira mheshimiwa miguu yangu iko kama ilivyo lakini huwa nafanya mazoezi ya kutembea na tangu nimekuwa death row kila siku kuanzia jumatatu mpaka ijumaa napumzika jumamosi na jumapili kwa sababu Mungu naye alipumzika siku ya saba kwa huwa napumzika mazoezi lakini from Monday to Friday natembea around hizo block nne za deathroom ziko nne.

Hilo eneo ninalotembelea mheshimiwa, ni mifereji ya maji machafu, ni mifereji ya kupitisha maji machafu na ni maeneo ambayo wafungwa wa death row wanafua nguo na wanapata wakitoka wakitolewa asubuhi wanakopumzikia. Mimi inabidi ninegotiate kwenye mifereji hiyo, huu mguu mmoja haufanyi kazi mheshimiwa, asante watu wasiojulikana. Nafanya mazoezi, natembea kila siku na siku zote na nina hii fear kwamba hivi nikiteleza hapa itakuwaje, kwa sababu mifereji ya maji machafu ni kwa ajili ya kupitishia maji machafu sio kwa ajili ya mazoezi ya wafungwa maeneo ya mazoezi ni uwanja mkubwa ulioko nyuma ya death lakini tangu nime nimeingia Ukonga siku ya Ijumaa kuu mpaka hapa nilipo sijaruhusiwa mimi na hajaruhusiwa mwingine yeyote aliyeko Death row kwenda kufanya mazoezi na sheria inasema waruhusiwe.

Sasa mheshimiwa nimesema nimesema kwamba kanuni zinasema wafungwa walioko kwenye death row wasichanganywe na wafungwa wengine. Sheria ya magereza inasemaje? Prisons Act sura ya 58. naomba uangalie kifungu cha 72 cha sheria hiyo Mheshimiwa.

Section 72 of the Prisons Act. A prisoner under the sentence of death shall be confined apart from other prisoners in a special cell or ward. And the treatment of the death penalty prisoner shall be under of the treatment of a prisoner under sentence of death, as may be prescribed. Na sheria inasema sheria kuu ya magereza inasema sisi ambao sio death row inmate tusikae na watu wa death row. So it is in the act. It is in the regulations. Nimewaambia mawakili wangu for the past 68 days, they have tried. They have tried valiantly. They have failed. They have failed.

Sasa mheshimiwa mawakili wangu wameniambia, nakuja sasa kwenye mahakama. Mawakili wangu wameniambia kwamba wameraise maswala haya mbele yako. Wame-raise huu ukiukwaji wa haki za mfungwa aliyeko mahabusu. They have drawn your attention to this to these unlawful treatment of a remand prisoner. Na wamenieleza jibu walilopewa ni kwamba Mahakama haiingilii mambo ya magereza. Sasa mheshimiwa, huo msimamo, huo msimamo, kama ni wa kweli kama ni kweli umesema hivyo mheshimiwa huo msimamo uko nje ya misingi ya sheria ya nchi hii uko completely out of step with the law mheshimiwa, wewe ni justice, visiting justice.

Wewe ni wale wanaotembelea magereza. Hii sheria inasema kifungu cha 48, nakitafuta mheshimiwa usichoke….Ntakipata…. but the import of the provision ni kwamba a magistrate is a visiting justice for all prisons under his jurisdiction. You are a visiting justice wa magereza yote ya Dar es Salaam, including Ukonga Central Prison. Kwa nini you are visiting justice?

Ni kwa sababu wewe ni Hakimu, you’re a Judicial officer. Na kama judicial officer wajibu wako hauishi unapohukumu mtu. Wajibu wako unaendelea kumsimamia huyo uliyemhukumu au wale ulioamuru waende magereza. Waende mahabusu, you continue to supervise their treatment while in prison. Ngoja nikupeleke kwenye kanuni za Mandela.

Principle four of the Mandela principles:  any form of detention or imprisonment and all measures affecting the human rights of a person under any form of detention or imprisonment shall be ordered by or be subject to the effective control of a judicial or other authority any form of…yes principle four, nimesema zinaitwa Mandela principles but their name is the body of principles for the protection of of all persons under any form of detention or imprisonment. Any form of detention or imprisonment and all measures affecting the human rights of a person under any form of detention or imprisonment shall be ordered by or be subject to the effective control of a judicial or other authority.

 Nimesema mheshimiwa Hakimu hili neno other authority limetafsiriwa humu nitupatia hiyo the proper the proper provision ilyotafsiri lakini maana yake ni Mahakama ndio inatakiwa iwe na effective control over prisoners and detainee kwa hiyo wajibu wako hauishi unaposema mpeleke mahabusu wajibu wako unaendelea ndio maana huwa unatembelea magereza mheshimiwa na nimeambiwa siku za karibuni ulikuwa magereza as a visiting justice nimeambiwa,  nafuatilia mambo haya kwa hiyo mheshimiwa, msimamo sahihi wa kisheria ni kwamba ni mahakama hii ndio inayopaswa isimamie utekelezaji wa haki za wafungwa wakiwa Ukonga central prison au wakiwa mahali pengine popote. Ni mahakama hii sio bwana jela.

Na nimewaambia mawakili wangu yote hayo; they tried valiantly, they fought hard, they have failed. Kwa hiyo mheshimiwa, naomba nisikuchukulie, yako mengi, mengine tutakutana nayo kama tutaenda High Court, tutakutana nayo. Lakini kwa haya ambayo nimeyasema mawakili wangu nawashukuru you fought bravely, you fought professionally, you did you did your duty and you did it well. It is time to step aside and let me do what I must do.

It is time to let me, do what I must do. It is my case again. Kwa hiyo mheshimiwa from now on mimi ndio nitakayejibizana na hawa mawakili wa serikali. Nimemaliza Mheshimiwa.

Mpoki:  Your honor, Justice is based on confidence. It’s between him and the […inaudible…]

“Kwa hiyo mheshimiwa, kuanzia sasa, mimi ndio nitakayejibizana na hawa mawakili wa serikali.”

Hakimu:  So kwa hiyo, kuanzia sasa, hoja zitakuwa zinajibiwa kati ya upande wa mawakili wa serikali, upande wa jamhuri na mshtakiwa mwenyewe mpaka pale atakaposema tena vinginevyo kwamba naomba mawakili wangu warudi au warudi huyu na huyu lakini kwa sasa mshtakiwa atajitetea mwenyewe kama alivyoomba, ombi lake limekubaliwa. Na upande wa utetezi wameridhia hivyo, kwa hiyo, kuanzia sasa ni mawakili wa serikali dhidi ya mshtakiwa.

Lissu: Mheshimiwa labda niombe lingine dogo tu liko nje ya haya naomba nipate kiti kirefu walau niweze kuandika Mheshmiwa. Hiki kifupi, nikikaa hapa hata hunioni.

Hakimu: Mtafutieni kiti, jamhuri kuna hoja nyingi zimesemwa na mshtakiwa naamini mmezirekodi.

[Mawakili wa Lissu wanampa karatasi fulani, Askari Magereza ananyoosha mkono kuipokea baada ya Lissu kuipokea, ambapo Lissu anampa na kueleza:]

Lissu: Unaona mheshimiwa, inabidi mawasiliano na mawakili wangu yapitie [anamnyooshea kidole Askari Magereza, ambaye anamrudishia karatasi hiyo].

Hakimu: Sasa sikiliza nimesha rule out, nimeshatoa uamuzi mdogo kwamba sasa unaendelea mwenyewe.

[Mawakili wa Lissu wanajadili kitu]

Hakimu: Issue ni nini hapo, Mughwai ni nini hapo, unasemaje Mpoki issue ni nini?

Mpoki: Nilikuwa namuuliza kama na karatasi za kuandika nimpe au na zenyewe tunakatazwa?

Hakimu: Sasa nitoe maelekezo, unapokuwa Mahakamani maafisa usalama, unapokuwa mahakamani kama Wakili unahitaji kumpa nyaraka yoyote mshtakiwa, apewe ,asizuiwe; asizuiwe kupewa sawasawa? Kama kutakuwa kuna hoja yoyote nielezwe mimi, Lakini sio vibaya nikajua kabla hamjampatia ili kuondoa hiyo tofauti. Sawa sawa? Ili kuondoa hiyo tofauti.

Mpoki: Sawa mheshimiwa.

Hakimu: Upande wa mashtaka

Nossoro Katuga [Wakili Mkuu wa Serikali] : Mheshimiwa kama tulivyoeleza shauri ni kwa ajili ya kutajwa labda hoja yetu ni kwamba tumesikia mengi kuhusu ambayo mshtakiwa ameiambia mahakama yako. kama tuliyaelewa vizuri yalilenga kuiambia mahakama yako sababu ya kwa nini hataki mawakili waendelee kumwakilisha kama tumemwelewa vizuri alikuwa anatoa sababu zinazopelekea kwa nini anaona sasa ajitetee mwenyewe.

Mheshimiwa hoja nyingine ambazo amezileta zikiwa ni sababu za kuieleza mahakama yako kwamba kwa nini anataka kujitetea mwenyewe? Mheshimiwa japo mahakama yako tukufu imeshaamua kwamba imeshawa-discharge kwa makubaliano mawakili wa utetezi katika shauri hili. Na sisi tunaona ni busara kwa sababu kifungu cha 310 ndio kina cha CPA ndio kinatoa haki ya ya mshtakiwa kuwakilishwa kwenye mashauri ya jinai. Na unapopewa haki ni haki yako pia kuikataa au kuikubali.

Kwa hiyo kama ambavyo Mahakama imesha-rule kwamba hii haki mshtakiwa kaamua kuikataa. […] Tukija kwenye hoja ambazo yeye ametuletea hapa mahakamani, ni hoja ambazo zinaenda moja kwa moja kwenye jeshi la magereza ni kwa jinsi gani ambavyo yeye anakaa huko.  Na hakukuwa na hoja yoyote ambayo humu ndani tunatakiwa tuijibie, hoja ile imesikilizwa imeletwa kwa upande wake, ina maana upande wa magereza bado hauja haujasikilizwa kuhusu hayo anayoyasema.

Nimeielewa mheshimiwa sidhani kama hoja hii hizi zilizoletwa za jinsi gani huko sijui nini zilikuja kwa ajili ya mahakama yako tukufu izitolee izitolee maamuzi kama tulimwelewa vizuri labda atarudia lakini alikuwa anatoa sababu gani zinazomfanya awakatae, awaondoe mawakili; sio awakatae, awaondoe mawakili wake na kuamua kujitetea mwenyewe. Lakini kama kuna hoja ambayo anaamini jeshi la polisi, I mean,  jeshi la magereza samahani  au mkuu yeyote wa wa jeshi la magereza hajaamua au hajafanya kile ambacho sheria inamtaka akifanye tunasema bado ana haki ya kisheria kuomba prerogatives orders. Specifically ni mandamus anaweza akaomba mandamus yeye ni wakili kama alivyojitambulisha na anasema ni mzoefu ni kweli kaka yetu akili mzoefu anajua nini kinachotakiwa kufanyika kuweza kuomba kuomba hizo hizo shufaa staiki katika mahakama husika au mahakama yenye uwezo wa kusikiliza mandamus sindio na mheshimiwa hizi zinaombwa ni kanuni ya nne,  kanuni ya nne ya ya kanuni za law reform fatal accident and miscellaneous provisions, sorry sio regulation, rules ni ni kanuni za sheria ya Law Reform  Fatal Acident in brackets and miscellaneous provisions judicial review procedures and fees rules za mwaka 2014 kanuni ya nne inasema mtu ambaye anayetaka kuomba judicial review afanye nini na pia inatoa [….] ya moja kwa moja.

Na ukitumia application hii au maombi haya ndipo tutapata sasa haki ya pande zote mbili tusikilize. Sio kama hivi ambavyo mahakama yako inapokea taarifa kutoka upande upande mmoja kwamba kama sheria zipo alivyokuwa anazi-cite na hii mamlaka authority haijazifuata au haijazifanya anaamini hilo basi afuate procedure yeye kama mwanasheria kuliko kuiomba mba mahakama yako itoe maagizo maanake ikitoa maagizo inatoa maagizo ya mandamus sasa ambao this is not a proper way kuifanya application hiyo.

Kwa hiyo implied ni kama imeletwa application ya progative order without formal application. Kwa hiyo upande wa jamhuri tunaona kuendelea kuingia kwenye huu mtego wa kuzijibia hoja alizozileta kwamba authority hii hainifanyii hivi, hainipi hiki, hainipi  haki ile tutakuwa tumeingia kwenye mtego ambao pia tutaifanya mahakama hii itoe maamuzi au itoe orders ambazo sio  sehemu yake.

Hizi prerogative orders zinatolewa kwa maombi maalum kama ambavyo nimeiambia mahakama yako tukufu na na utaratibu maalum ambao ambao sasa pande zote mbili zitapata nafasi ya kusikilizwa utaratibu huo ukifuata kweli yuko condemned, kweli sijui nini hivyo vyote sisi tumesikia upande mmoja kwa maneno bila bila kusikiza upande wa pili kwa hiyo sisi tunaona kama kuna hayo malalamiko basi sheria hii itumike kuweza kuweza kutoa hizo kama ikibainika kweli kuna kiongozi au authority fulani ijafanya majukumu yake iliyopewa kisheria basi wawe compelled kufanya hayo majukumu lakini kwa kufuata utaratibu ujumla wa kila kitu kiko kwenye sheria.

Otherwise kwa kusema haya tuondoke huko tuje kwenye ombi la jamhuri, Mheshimiwa nashauri kama tulivyoeleza tulivyoeleza awali kwamba ni kwa ajili ya kutajwa mbele yako leo…

Lissu: Mheshimiwa nahitaji kujibu alichokisema, mheshimiwa, asiendelee tu.

Hakimu: Umemaliza?

Nassoro Katuga: Mheshimiwa kwenye issue gani?

Hakimu: Maombi ya mshtakiwa juu ya submission yake kuhusiana ….[inaudible]

Nassoro Katuga: Mheshimiwa kwenye upande wa malalamiko dhidi ya Jeshi la Magereza sisi tunaona ni hayo kwamba utaratibu ufuatwe ili wenzetu nao wapewe nafasi ya kusikilizwa. Kuliko Mahakama yako ikaingia kuamuru kitu ambacho isivyotarajiwa na bila kufuata ule utaratibu, sisi tumemaliza.

Mheshimiwa nimemsikiliza wakili wa serikali mkuu. Na naomba niseme kwa kifupi sana mheshimiwa ninajua utaratibu wa kuomba amri ya mandamus sio kwamba nimeusahau au siujui. sijaomba mandamus sio kwa sababu sijui, Mheshimiwa nilisema wakati nazungumza kwamba kisheria, mahakama hii ina-retain control effective control over the detainee or the prison. Nilisema mheshimiwa you are a visiting justice. Nilisema nitakuambia kifungu ni kifungu cha 101 cha sheria ya magereza. Kifungu kidogo cha tano, every area commissioner, magistrate and justices of the peace shall be an ex officio visiting justices of all prisons within their respective areas of jurisdiction.

Nachotaka, nimetoa taarifa to a visiting justice, do your duty.

Hakimu: Wakili umeelewa? hii ni taarifa.

Lissu: Ningetaka maombi, ningeleta maombi, nimetoa taarifa kwa visiting justice. Kwa hiyo umeelewa wakili wa serikali?

Nossoro Katuga [Wakili Mkuu wa Serikali] : Mheshimiwa mimi nilivyomuelewa tangu mwanzo ni hivyo sababu kwamba alikuwa anataka kuwaondoa mawakili wake lakini sasa maneno yakawa mengi na jinsi anavyoishi pale. Kwa hiyo  nikasema kama yapo hayo anayoyasema wapewe nafasi wenzetu waweze kuyasemea kuliko mahakama yako kuyaangalia.

Lakini kama ameiweka kwamba ni taarifa kwa mahakama ambayo itatembelea magereza, taarifa haijibiwi. Kama ilikuwa ni taarifa hata mahakama yako ilikuwa haina haja ya kutuambia labda tuijibie sindio? Kwa sababu halikuwa ombi wala haikuwa chochote. Kwa hiyo ni kama ni taarifa mheshimiwa tunategemea tu mahakama iseme imeipokea. Endelea wakili.

Lissu: Ni hayo tu mheshimiwa, ni hayo.

Hakimu: Kwa hiyo niseme, hizo submission zako, kwa sababu ni taarifa nimezichukua na zitafanyiwa kazi kiutawala.

Lissu: Nashukuru

Hakimu: Not judiciously, administratively sawa sawa ni sahihi kabisa. Mahakama hii imekuwa inafanya inspection ukaguzi kwenye magereza yote na personally as an in-charge mimi kama mfawidhi nimekuwa natembelea huko. Kwa hiyo itafanyiwa kazi kiutawala sawasawa?

Lissu: Nashukuru.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×