Wuamini 52 wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church, maarufu kama Ufufuo na Uzima wamefungua kesi ya Kikatiba kudai haki yao ya Uhuru wa Kuabudu.
Kesi hiyo ya Kikatiba iliyofunguliwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Jeshi la Polisi inategemewa kusikilizwa kesho Julai 11, 2025, mbele ya Majaji watatu: Jaji Ephery Sedekia Kisanya, Jaji Cyprian Phocas Mkeha na Jaji Zahra Abdallah Maruma. Kesi imesajiliwa kwa namba16408/2025 na imepangwa kusikilizwa majira ya nane na nusu mchana.
Kanisa la Ufufuo na Uzima linalongozwa na Askofu Josephat Gwajima lilufungwa mnamo Juni 02, 2025, kwa kile ambacho barua kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ilieleza kiongozi wa kanisa hilo amekua akitoa mahubiri yenye nia ya kuichonganisha serikali na wananchi.
Kufungiwa kwa kanisa hilo kunafuatia mahubiri na mkutano na waandishi wa habari aliofanya kiongozi wa kanisa hilo kukemea matukio ya watu kutekwa, kupotezwa na kuuwawa, ambapo alizungumza mnamo Mei 24, 2025 na pia mnamo Juni 01, 2025, ambapo alitangaza maombi ya siku saba juu ya masuala hayo.
Kanisa hilo lilingia katika juhudi mbalimbali za kisheria ikiwemo kukataa rufaa, na kupeleka shauri Mahakamani, sehemu zote juhudi hizi hazijafanikiwa kuleta ufumbuzi.
Kesi ilivyopelekwa Mahakamani na kusikilizwa chini ya jaji Juliana Masabo, Mahakama haikuweza kutoa uamuzi wa moja kwa moja katika suala hilo. Hii ni kutokana na kuwa barua ya kulifungia kanisa hilo iliandikwa jina tofauti yaani Glory of Christ Church badala ya Glory of Christ Tanzania Church. Hata mawakili wa serikali waliieleza Mahakama katika shauri hilo kuwa hakuna barua ya kulifungia kanisa la Glory of Christ Tanzania Church na kusisitiza haipo na ni uzushi.
Kanisa hilo pia limefanya juhudi za kukata rufaa kupitia taratibu za kiserikali, yaani kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, hata hivyo, Wakili wa Kanisa hilo, Peter Kibatala, alieleza kuwa walipokea barua kutoka kwa Waziri ya Mambo ya Ndani iliyoeleza kuwa hawaitambui barua hiyo ya kulifunguia kanisa hilo.Hata hivyo, barua rasmi ya kukusudia kufuta usajili wa bodi ya wadhamini wa kanisa hilo, tofauti na iliyosambaa mtandaoni, iliweza kuwasilishwa kwa Bodi ya Wadhamini wa Kanisa hilo ikionesha kuwa ilitolewa Juni 03, 2025.
Inategemewa hapo kesho Julai 11, 2025, Jaji Masabo pia atatoa uamuzi kuhusu huu mkanganyiko baada ya Wakili wa Kanisa hilo kuwasilisha vielelezo vipya.
Toka kanisa hilo lilivyofungwa mnamo Juni 02, 2025, waumini wamekuwa wakijitokeza kwa ajili ya kusali nje ya kanisa kuu lililopo Ubungo Kibo, hata hivyo waumini hao wamejikuta wakiambulia madhila mbalimbali ikiwemo vipigo, na kukamatwa.
Majina ya waleta maombi hao ni pamoja na:
- Dinali Mbaga
- Elisha Musa
- Nsajigwa Lwijisho
- Basil Kashumba
- Filbert Benedicto
- Stephano Samson
- Ela Mtishbi
- Masihi Kalokola
- John Job
- Emmanuel Asilia
- Joseph John
- Augustin Stamili
- Lameck Msude
- Boniface Maingu
- Amani Sahodi
- Adoph Makumba
- Oscar John
- John Fredrick
- Erick Michael
- Daniel Makiungile
- Ozeniel Shelukindo
- Wiliriki Kereti
- Freeman Kalinga
- George Gilbert
- Petro Faida
- John Boenge
- Joseph Fabian
- Leopodius Martin
- Patrick Augustino
- Jacob Silas
- Andrew Kamulei
- Gwandumi Ngalawa
- Beatus Poryton
- Amos Makaa
- Anderson Hassan
- Fanuel Lameck
- Bahati Mwampamba
- Joshua Musa
- Samuel Bernad
- Gergina Mwiza
- Levina Zakaria
- Maria Gidion
- Rose Erasto
- Nosyaga Mwakila
- Janeth Shoo
- Anna Meataa
- Telesia Michael
- Veronica Mbevu
- Rhoda Raphael
- Laika Mboya
- Hilaria Godfrey
- Mage Henry