Tume ya Taifa ya Uchaguzi imefanikiwa kuwaandikisha Watanzania milioni 37.6 kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ikielezwa kuwa ni ongezeko la asilimia 26.55 kutoka wapiga kura 29.7 waliokuwa kwenye daftari, mwaka 2020.
Idadi hii ni kubwa kuliko idadi ya watu wenye umri wa miaka 14 na kuendelea waliohesabiwa katika sensa iliyofanyika Agosti 23, 2022.
Akiongea mnamo Julai 26, 2025, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji Jacobs Mwambegele ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kupiga kura.
“Tume inatoa wito kwa wadau wote ikiwa ni Pamoja na wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi kwa kuzingatia sheria, kanuni, miongozo na maelekezo yatakayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Kura yako haki yako jitokeze kupiga kura,” alieleza Jaji Mwambegele.
