The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Kwa Nini Mtoto Wako Analia Sana?

Tafiti zinasema huenda si kosa lako ni sehemu ya ukuaji wake.

subscribe to our newsletter!

Wengi wetu wazazi, hasa wazazi wapya, tumewahi kuwa kwenye hali hii: mtoto analia sana bila kunyamaza. Tunajaribu kila kitu kumbeba, kunyonyesha, kubadilisha nepi, lakini kilio hakikomi. Tunachoka, tunakata tamaa, na wakati mwingine tunajiuliza: “Je, kuna kitu kibaya kimemtokea mtoto wangu?” “Au kunakitu nakosea?”

Habari njema ni kwamba, kulingana na tafiti nyingi, hali hii, ambayo kwa kitaalamu hujulikana kwa jina lake la kimombo kama colic, mara nyingi ni sehemu ya ukuaji wa kawaida wa mtoto, na si kosa la mzazi.

Kwa mfano, utafiti mmoja unaonesha kuwa baadhi ya watoto huzaliwa wakiwa na mfumo wa hisia nyeti zaidi. Hii inamaanisha kuwa wanaweza kuhitaji muda mrefu zaidi kujifunza kutuliza hisia zao.

Kwa maneno mengine, mtoto anayelia sana si lazima awe na tatizo la kiafya. Watafiti wanasema hii mara nyingi huhusiana na temperament, au hali ya kiasili ya mtoto. Dk Thomas Boyce, mtaalamu wa ukuaji wa watoto, anaita watoto hawa orchid children, au wale wanaohitaji uangalizi zaidi, lakini hupevuka vyema wanapolelewa katika mazingira yenye upendo.

Watoto hawafanani na jambo hilo ni sawa kabisa.

Kila mtoto ni wa kipekee. Dk Joel Gator Warsh anaeleza kuwa kila mmoja huzaliwa na muundo wake wa hisia na tabia, yaani temperament. Wataalamu wanasema, hata watoto wawili kutoka familia moja wanaweza kutofautiana sana.

SOMA ZAIDI: Tabia Kumi Ambazo Watoto Wetu Hujifunza Kutoka Kwetu 

Dk Jerome Kagan, mtafiti maarufu wa saikolojia, anaeleza kuwa temperament ni sehemu ya vinasaba, genetics, na haibadiliki kwa urahisi. Wengine ni watulivu, wengine wachangamfu, na baadhi hulia mara kwa mara bila sababu ya moja kwa moja.

Utafiti mwingine unaonesha kuwa watoto wenye mfumo wa neva unaochangamka zaidi, yaani highly sensitive, wana uwezekano mkubwa wa kulia mara kwa mara. Hii haimaanishi wana tatizo; mara nyingi, ni njia yao ya kushughulikia msisimko wa mazingira mapya.

Hivyo, kilio cha mara kwa mara si dalili ya malezi mabaya; mara nyingi ni kielelezo cha muundo wa kiasili wa mtoto.

Kama wazazi inatupasa tuelewe hili, kwa sababu katika utamaduni wetu, mara nyingi tunaambiwa mtoto mzuri ni “mtulivu” na asiyelia sana. Tunapokumbana na mtoto anayelia mara kwa mara, tunajisikia kushindwa hasa tukisikia kauli kama: “Mbona mtoto wa fulani hafanyi hivi?” 

Lakini ukweli ni kwamba: tofauti hizi ni kawaida na si kosa letu. Badala ya kujilaumu, tujiulize swali hili: “Mtoto wangu anajaribu kuniambia nini kupitia kilio hiki?”

Vidokezo muhimu

Tutambue mda ambao mtoto analia sana: Tafiti zinaonesha watoto hulia zaidi nyakati maalumu, mara nyingi jioni. Angalia mpangilio wa mtoto wako: analia baada ya kula? Baada ya kelele nyingi? Tambua ili ujue hatua ipi ichukuliwe.

SOMA ZAIDI: Je, Tunawafundisha Watoto Wetu Kuchagua Chakula Bora?

Nguvu ya mguso: Cleveland Clinic inasema kumgusa mtoto kipole pole na kumbeba mtoto huongeza homoni ya oxytocin kwa mzazi na mtoto inayosaidia kupunguza msongo na kumsaidia mtoto kuacha kulia.

Pumzika unapoweza: Utafiti unaonesha mzazi anapochoka kupita kiasi, anaweza kuwa na upungufu wa subira. Tutafute msaada wa kumwangalia mtoto kutoka kwa wenza wetu, ndugu, au rafiki. Ni vizuri kupumzika kabla ya kurejea kwa mtoto.

Tuache kujilinganisha: Kila mtoto na kila safari ya malezi ni tofauti. Kujilinganisha huongeza wasiwasi bila faida yoyote.

Tuombe ushauri kwa wakati: Ikiwa tuna wasiwasi juu ya kilio cha mtoto, tusisite kumwona daktari. Wataalamu wanashauri kuangalia dalili za ugonjwa ikiwa kilio kinaambatana na homa, kukataa kula au kutokuwa na choo cha kawaida.

Makala hizi za malezi huandaliwa na C-Sema, shirika lisilo la kiserikali linalojikita katika kuendeleza na kulinda haki za watoto Tanzania. Kwa maoni na ushauri, wapigie kwenye simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile, unaweza kuwapata kupitia kurasa za Facebook: Sema Tanzania, X: @SemaTanzania, na kupitia tovuti yao www.sematanzania.org.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×
×