Shamra shamra za uchaguzi ndani ya Chama cha Mapinduzi zinaendelea, ambapo hivi leo Julai 29, 2025, majina ya watia nia walioteuliwa na Kamati Kuu ya chama hicho kwa ajili ya kwenda kwenye kura za maoni yametangazwa.
Hata hivyo, wabunge zaidi ya 40 ambao wako Bungeni kwa sasa hawataonekana katika kura za maoni ya chama hicho baada ya Kamati Kuu ya chama hicho kuyaondosha. Baadhi ya majina yaliyokumbwa na panga hilo yameendelea kuzua gumzo kubwa mitandaoni.
Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina, ni jina ambalo wengi walikuwa wakisubiria kuona kama atatokea au la, hii ni kutokana na misimamo yake iliyomfanya kuwa maarufu jimboni kwake na miongoni mwa watu wengi, huku akigeuka kuwa mwiba kwa serikali . Jina la Mpina halijarudi na halitakuwepo kati ya watu saba waliopitishwa kama wagombea wa kura za maoni Kisesa.
Akiongea na The Chanzo kuhusu suala hilo Mpina ameeleza kuwa, hana kitu cha kusema kwa sasa kwani ndio amepokea tu taarifa hizo.
Jina lingine lililozua gumzo kubwa ni la Januari Makamba, Mbunge wa Bumbuli, naye jina lake halitakuwa kati ya majina sita yaliyorudishwa Kwenda kwenye kura za maoni jimboni, wengi wanahusisha kukatwa kwa jina la Makamba na makundi mbalimbali yaliyoibuka ndani ya chama hicho.
Mbunge wa Arusha, Mrisho Gambo, ambaye amekuwa katika mvutano mkali na Paul Makonda, naye ni moja kati ya watu walioachwa nje ya kinyang’anyiro hicho.
Wengine waliokatwa ni pamoja na Mbunge wa Ngorongoro Emmanuel Ole Shangai na Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka, Wabunge wanaotokea kwenye maeneo ambapo kumekuwepo na mvutano mkali kati ya hifadhi, serikali na jamii hasa za wamasai.
Wabunge wengine ambao nao hawataonekana kwenye kura za maoni ni pamoja na:
- Godwin Emmanuel Kunambi, Mbunge wa Mlimba
- Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula, Mbunge Ilemela
- Twaha Ally Mpembenwe, Mbunge wa Kibiti
- Vedastus Mathayo Manyinyi, Mbunge Musoma Mjini
- Zuberi Mohamedi Kuchauka, Mbunge wa Liwale
- Dr. Alfred James Kimea, Mbunge wa Korogwe Mjini
- Rashid Abdalla Rashid, Mbunge wa Kiwani
- Geoffrey Idelphonce Mwambe, Mbunge wa Masasi Mjini
- Stephen Byabato, Mbunge wa Bukoba Mjini
- Abdallah Jafari Chaurembo, Mbunge wa Mbagala
- Khamis Said Gulamali, Mbunge wa Manonga
- George Ranwell Mwenisongole, Mbunge wa Mbozi
- Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Mbogwe
- Hassan Zidadu Kungu, Mbunge wa Tunduru Kaskazini
- Daimu Iddi Mpakate, Mbunge wa Tunduru Kusini
- Mansoor Shanif Jamal, Mbunge wa Kwimba
- Justin Lazaro Nyamoga, Mbunge wa Kilolo
- Shabani Omari Shekilindi, Mbunge wa Lushoto
- Mohamed Lujuo Monni, Mbunge wa Chemba
- Flatei Massay, Mbunge Mbulu Vijijini
- Innocent Edward Kalogeris, Mbunge Morogoro Kusini
- Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge Ngara
- Cecil David Mwambe, Mbunge Ndanda
- Toufiq Salim Turky, Mbunge wa Mpendae
- Ravia Idarus Faina, Mbunge wa Makunduchi
- Yahya Ali Khamis, Mbunge wa Kijini
- Omar Ali Omar, Mbunge wa Wete
- Juma Hamad Omar, Mbunge wa Ole
- Haji Makame Mlenge, Mbunge wa Chwaka
- Simai Sadiki, Mbunge wa Nungwi
- Ahmed Ngwali, Mbunge wa Ziwani
- Abbas Ali Mwinyi, Mbunge wa Fuoni
- Amour Khamis Mbarouk, Mbunge wa Tumbe
- Omar Issa Kombo, Mbunge wa Wingwi
- Khamis Hamza Khamis, Mbunge wa Uzini
- Salum Mohammed Shaafi, Mbunge wa Chonga
- Iddi Kassim Iddi, Mbunge wa Msalala