The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Vigogo Sita Hawatakuwa na Mpinzani Kura za Maoni CCM Majimboni

Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa(NEC) ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla ametoa orodha ya majina ya wana CCM waliopita kwenye mchujo wa Kamati Kuu kwa ajili ya kwenda kupigiwa kura za maoni majimboni kwenye mchakato wa uteuzi wa wagombea ubunge na uwakilishhi wa chama hiko kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

subscribe to our newsletter!

Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa(NEC) ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla ametoa orodha ya majina ya wana CCM waliopita kwenye mchujo wa Kamati Kuu kwa ajili ya kwenda kupigiwa kura za maoni majimboni kwenye mchakato wa uteuzi wa wagombea ubunge na uwakilishhi wa chama hiko kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Katika orodha iliyosomwa na Makalla kwa ngazi ya ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, majimbo manne kati ya majimbo 272 ya Tanzania Bara na Zanzibar yatakuwa na mwana CCM mmoja ambaye atapigiwa kuwa za maoni katika mchakato wa uteuzi.

Waliopita peke yao katika majimbo hayo ni pamoja na Salma Kikwete ambaye ni mbunge wa sasa wa jimbo la Mchinga hatakuwa na mpinzani ndani ya CCM katika kura ya maoni jimbo hilo. Salma Kikwete ambaye ni mke wa Rais wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete aliingia Bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2017 baada ya kuteuliwa kuwa mbunge wa viti maalum na Rais wa awamu ya tano John Pombe Magufuli na mwaka 2020 alijitosa ubunge wa jimbo hilo la Mchinga.

Mwingine ni Doto Biteko mbunge wa sasa wa Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Biteko ambaye ni mbunge wa Bukombe tangu mwaka 2015 hatakuwa na mpinzani kwenye kura za maoni za CCM jimbo humo.

Mbunge wa Chalinze wa sasa Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) naye hatakuwa na mpinzani katika kura za maoni katika jimbo hilo. Ridhiwani Kikwete ni mtoto wa Rais mstaafu Kikwete na amekuwa mbunge wa Chalinze kuanzia mwaka 2014 aliposhinda katika uchaguzi mdogo.

Naye Hamad Chande ambaye ni Mbunge wa Kojani visiwani Pemba na Naibu Waziri wa Fedha wa Tanzania kwa sasa, hatakuwa na mpinzani kwenye kura za maoni jimboni Kojan. Chande amekuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu mwaka 2015.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari leo, Makalla pia hii leo alitoa orodha ya wanachama waliopita mchujo wa uteuzi wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambapo majimbo mawili yana jina moja la mtia nia atakayepigiwa kura za maoni.

Wa kwanza ni Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla  ambaye hatakuwa na mpinzani katika kura za maoni za uwakilishi jimbo la Kiwani. 

Mwingine ni Khalid Salum Mohamed ambaye ni mwakilishi wa jimbo la Donge tangu mwaka 2016 na amekuwa akishika nyadhifa mbalimbali za uwaziri katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tangu awe mwakilishi.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×
×