The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

January Makamba Akanusha Kuengulia Sababu ya Mbio za Urais, Atuma Salamu kwa Wananchi Bumbuli

Makamba amekanusha madai hayo alipoulizwa na waandishi wa habari waliopiga kambi ofisini kwake jijini Dar es Salaam kutaka kupata maoni yake baada ya kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM(NEC) Taifa, kilichoketi Julai 28, 2025 kutomteua kwenye kinyang’anyiro cha ubunge ndani ya CCM jimboni kwake Bumbuli, wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.

subscribe to our newsletter!

Mbunge wa Bumbuli anayemaliza muda wake January Makamba amekanusha madai ya kwamba hajapita katika mchakato wa uteuzi wa ubunge ndani ya CCM kwa sababu ya kumdhibiti katika mbio za Urais akieleza kwamba maneno hayo ni uzushi.

Makamba amekanusha madai hayo alipoulizwa na waandishi wa habari waliopiga kambi ofisini kwake jijini Dar es Salaam kutaka kupata maoni yake baada ya kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM(NEC) Taifa, kilichoketi Julai 28, 2025 kutomteua kwenye kinyang’anyiro cha ubunge ndani ya CCM jimboni kwake Bumbuli, wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.

Amesema kwamba haamini kwamba kikao kikubwa na cha heshima kama cha Kamati Kuu kinaweza kufanya maamuzi ya uteuzi wa ubunge kutokana na mambo mengine yanayokuja huko mbeleni.

“Hizo ni ramli tu za mtaani,” amesema Makamba, “ Kwa sababu muda bado sana na kwenye chama chetu kuna kiongozi ambaye wote tunajua akiendelea.”

Makamba ameeleza kupokea uamuzi huo wa chama na kuutii na kuendelea kueleza kuwa suala la Urais ni suala lenye mkono wa Mungu zaidi kuliko matakwa ya binadamu kama vile wengi wanavyodhani. 

“Kwenye hili mkono wa Mungu ni mkubwa zaidi, kwa hiyo sio jambo la kupania sana kulipata au kupania sana kuzuia mtu,” amesema Makamba.

Makamba ambaye pia ni mjumbe wa NEC amesema kuwa katika CCM vikao ndio vina mamlaka na maamuzi ambayo kila mwanachama na kiongozi wanatakiwa kuheshimu maamuzi hayo, hivyo naye ameyapokea maamuzi ya Kamati Kuu ya CCM.

“Kama unachukua fomu na unajua mwisho wake ni maamuzi ya kamati kuu eidha kuteuliwa au kutoteuliwa ikitoka kutoteuliwa maana yake unapokea na kukubali kama mwanachama mwaminifu. Kwa hiyo, huwezi kutoka ukasema mimi nimeonewa sababu wakati unachukua fomu ulijua kuna eidha kuteuliwa au kutoteuliwa,” amesema Makamba.

SOMA ZAIDI: Panga la Kamati Kuu CCM Lawashukia Wabunge Zaidi ya 40. Hawataonekana Kwenye Kura za Maoni CCM

Amewataka wanachama wenzake wa CCM jimboni Bumbuli kuyapokea  maamuzi ya uteuzi wa CCM na kushirikiana na viongozi wa wilaya, kata na matawi kuhakikisha kwamba utaratibu mzima wa wagombea walioteuliwa kupigiwa kura za maoni unafanyika vizuri.

“Kwa sababu ukivurugukika inaweza ikajengeka dhana mbunge aliyekuwepo kanuna, kwa hiyo kama mnanipenda jamani toeni ushirikiano ili mambo yaende vizuri,” alisisitiza Makamba.

Amesema amewasiliana na viongozi wa wilaya ya Lushoto kumpangia majukumu yoyote ya chama kwa kadiri watakavyoona anafaa, lakini pia kwa nafasi yake kama mjumbe wa NEC anawajibika kukitetea chama kwenye uchaguzi mkuu.

Makamba ambaye ameeleza kuwa amejiunga CCM tangu mwaka 1992, amekuwa Mbunge wa Bumbuli tangu mwaka 2010 na mwaka 2015 aliingia katika tano bora za mchujo wa CCM wa kumpata mgombea Urais kati ya watia nia 38 ambapo mwisho wa siku Hayati John Pombe Magufuli aliibuka kidedea.

Kwa nyakati tofauti ameshika nyadhifa za Unaibu Waziri na Waziri katika awamu ya nne, tano na sita. Kabla ya kuingia kwenye Ubunge alihudumu katika utumishi wa umma kwa nafasi mbalimbali ikiwemo msaidizi wa Rais wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×
×