Chama Cha Mapinduzi(CCM) kimeendelea na mchakato wa ndani wa chama wa kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu ambapo katika siku za Agosti 1, 2 na 3, 2025 jumuiya za chama hiko zimefanya mikutano mikuu jijini Dodoma kwa ajili ya kura za maoni ya uchaguzi viti maalum vya wabunge na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Jumuiya za CCM zilizofanya uchaguzi wa kura za mwishoni mwa wiki hii ni pamoja na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa CCM na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT), ambapo katika mchakato huo wa kura za maoni katika hatua hiyo ya awali wanachama wao 21 wameibuka kidedea kwa upande wa ubunge na 8 kwa upande wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Katika mchakato huu imeshuhudiwa wabunge wawili wa sasa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakibwaga na wajumbe kwenye kura zilizopigwa. Wabunge hao ni Neema Lugangira ambaye alikuwa anatetea nafasi yake ya viti maalum kundi la kutoka Asasi za Kiraia (NGOs) na mwingine ni Khadija Taya maarufu kama Keisha aliyekuwa anatetea nafasi yake kundi la watu wenye ulemavu.
Waliotetea nafasi zao ni pamoja na Ummy Hamisi Nderiananga ambaye ni mbunge wa viti maalum kutoka kundi la watu wenye ulemavu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu). Mwingine ni Najma Murtaza Giga mbunge wa viti maalum kutoka kundi la Jumuiya ya Wazazi wa CCM ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge la 12.
Mchakato UVCCM
Katika Mkutano Mkuu wa UVCCM uliofanyika Ijumaa Agosti 1, 2025 na kutamatika Agosti 2, 2025 kwenye nafasi za ubunge wa viti maalum Tanzania Bara ambazo ni nafasi sita zilikuwa na watia nia 31.
Walioshinda ni Mbunge wa sasa wa vijana kupitia CCM Ng’wasi Damas Kamani kura 409, akifuatiwa na Jessica John Magufuli kura 391, Halima Abdalah Bulembo kura 320, Lulu Guyo Macha kura 316, Juliana Didasi Masaburi kura 282 na Timida Mpoki Fyamdomo kura 280.
SOMA ZAIDI: Vigogo Sita Hawatakuwa na Mpinzani Kura za Maoni CCM Majimboni
Kwa upande wa Zanzibar viti vinne vya ubunge wa viti maalum walioshinda kati ya wagombea 17 ni pamoja na Mwanaenzi Hassan Suluhu kura 399, Latifa Khamis Juakali kura 357, Zainab Abdallah Issa kura 334 na Amina Ali Mzee kura 151.
Na kwa upande wa viti maalum Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambapo ni nafasi mbili kati ya watia nia 14 walioshinda ni Salha Muhammed Mwinjuma kura 255 na Hudhima Mbarak Tahir kuwa 233.
Mchakato Jumuiya ya Umoja wa Wazazi CCM
Kwa upande wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM mkutano mkuu ulifanyika Agosti 1, 2025 na walioshinda katika nafasi mbili za ubunge wa viti maalum kwa upande wa Zanzibar ni Najma Murtaza Giga kura 591 na kwa upande wa Tanzania Bara ni Dk.Catherine Joackim aliyepata kura 597 kati ya wagombea 18.
Giga ambaye alikuwa mbunge wa viti maalum katika Bunge lililoisha na Mwenyekiti wa Bunge ametetea nafasi yake, huku mbunge wa viti maalum katika Bunge linalomaliza muda wake kupitia CCM Khadija Taya maarufu kama Keisha akishindwa kutetea nafasi yake.
Kwa upande wa viti maalum Baraza la Uwakilishi kutoka jumuiya ya wazazi kwa upande wa nafasi ya uwakilishi Zanzibar walioshinda ni Aza January Joseph aliyepata kura 350 akifuatiwa na Salama Abbas Juma aliyepata kura 330 na kuwabwaga wenzao sita.
Mchakato UWT
Jumuiya ya wanawake wa CCM (UWT) yenyewe imefanya mkutano wake mkuu wa taifa kwa ajili ya kura za maoni ya wabunge na wawakilishi wa viti maalum kutoka makundi mbalimbali kuanzia Jumamosi Agosti 2, 2025 na kumalizika Agosti 3, 2025.
Kwa upande wa viti maalum kundi la wanawake wenye ulemavu walioshinda kwa upande wa Tanzania Bara ni Ummy Hamisi Nderiananga kura 758 ambaye anatetea nafasi yake, Stela Ikupa Alex kura 708 na Aisha Asantu Mduya kura 326. Kwa upande wa Zanzibar ni Nassriya Nassir Ali kura 656.
Kwa upande wa kura za maoni kundi la kutoka vyama vya wafanyakazi Tanzania Bara walioshinda ni Halima Iddi Nassor kura 566 na Mariam Anzurungi Mangula kura 290 huku upande wa Zanzibar ni Tunu Juma Kondo aliyepata kura 556.
Kwa upande wa kura za maoni kundi la wanawake vyuo vikuu Tanzania Bara walioshinda ni pamoja na Selina Henry Kingalame kura 562, Asha Juma Ferooz kura 494 na Dkt Regina Christopher Malina kura 268 huku kwa upande wa Zanzibar aliyeshinda ni Zeyana Abdallah Hamid aliyepata kura 426.
Upande wa kundi la wanawake kutoka Asasi za Kiraia (NGOs) kwa upande wa Tanzania Bara walioshinda ni Magreth Baraka Ezekiel kura 668, Rahma Riadh Kisuo kura 350 huku upande wa Zanzibar aliyeshinda ni Mgeni Hassan Juma kura 302.
Kwa upande wa viti maalum Baraza la Wawakilishi Zanzibar walioshinda kutoka kundi la watu wenye ulemavu ni Zainab Abdallah Salum kura 384 na Anna Athanas Paul kura 369. Kundi la vyuo vikuu walioshinda ni Lela Muhamed Mussa kura 760 na Khadija Salum Ali kura 323.
SOMA ZAIDI: Panga la Kamati Kuu CCM Lawashukia Wabunge Zaidi ya 40. Hawataonekana Kwenye Kura za Maoni CCM
Mikutano hiyo ya kitaifa ya jumuiya za CCM kwa ajili ya kuteua wagombea wa viti maalum kutoka makundi mbalimbali imefanyika ikiwa ni siku chache tangu kukamilika kwa mchakato wa wagombea wa viti maalum ngazi ya mikoa ambapo kura za maoni za uchaguzi zilipigwa katika mikutano mikuu ya mikoa ya Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) ambapo washindi kutoka mikoa yote walitangazwa.
Ushindi kura ya maoni haimaanishi tayari uteuzi umefanyika
Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM, Naibu Katibu Mkuu CCM kwa upande wa Tanzania Bara, John Mongella aliwakumbusha wanachama wa CCM kuwa walioshinda kwenye uchaguzi wa kura za maoni waendelee kusubiri maamuzi ya vikao vya juu vya chama ambavyo ndivyo vyenye maamuzi ya mwisho.
Kwa mujibu wa utaratibu uliotolewa na CCM hapo awali ni kuwa mchakato huu wa kura za maoni sio wa mwisho kwani vyombo vya juu vya chama hiko yaani vikao vya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa (NEC) na NEC yenyewe ndio vitatoa maamuzi ya mwisho ya uteuzi.
Kwa upande wa nafasi za Ubunge na Uwakilishi wa majimbo, leo Agosti 4, 2025 itafanyika kura ya maoni ya ndani ya chama hiko nchi nzima kupata wawakilishi 272 wa ubunge na