The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Yatoa Ufafanuzi Takwimu za Wapiga Kura

Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye pia ni Katibu wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC), Ramadhani Kailima amesema kuwa hakuna takwimu za wapiga kura zilizoongezeka kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kama ilivyolinganishwa na baadhi ya watu na takwimu za makadirio ya wapiga kura kwa mujibu wa Sensa.

subscribe to our newsletter!

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye pia ni Katibu wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC), Ramadhani Kailima amesema kuwa hakuna takwimu za wapiga kura zilizoongezeka kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kama ilivyolinganishwa na baadhi ya watu na takwimu za makadirio ya wapiga kura kwa mujibu wa Sensa.

Akizungumza kwenye mkutano wa Tume na wazalishaji wa maudhui ya mtandaoni kuhusu uchaguzi mkuu 2025 uliofanyika jijini Dar es Salaam, Agosti 3, 2025, Kailima amesema kuwa kifungu cha 9 kifungu kidogo cha pili cha Sheria ya Urais, Ubunge na Madiwani kimeipa wajibu Tume wa kuandikisha wapiga kura  waliotimiza umri wa miaka 18 au zaidi au watakaotimiza umri huo wakati wa uchaguzi. 

Amesema kuwa zipo taarifa walizoziona kwenye mitandao kuwa Tume imeandikisha wapiga kura wapya takribani milioni saba, akieleza kuwa taarifa hizo za upotoshaji zinasema idadi hiyo inazidi makisio ya sensa ya kuandikisha watu takribani milioni 5 ambao wangekuwa na umri wa kupiga kura mwaka 2025.

“Takwimu zilizopo kwenye Tume watu takribani milioni 3,113,931 ni wale ambao umri wao umeonesha walikuwa wanapaswa kuandikishwa kwenye daftari mwaka 2015 na mwaka 2020 lakini hawakuandikishwa, wakasema wameandikishwa. Kwa hiyo ukitoa sasa wale watu wapya milioni saba na nukta kadhaa, ukitoa milioni tatu nukta kadhaa maana yake watu wapya kabisa ambao wana miaka 18 au kuzidi umri huo ni watu milioni 4 na kidogo hivi. Kwa hiyo hata takwimu zile za sensa hatujawahi kuzifikia katika eneo hilo,” amesema Kailima.

Tume ilitangaza jumla ya wapiga kura 37,655,559 wamejiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2025 kufatia uboreshaji uliofanyika kwa awamu mbili; kuanzia Julai 20, 2024 hadi Machi 25, 2025 na kuanzia Mei 1, 2025 hadi Julai 4, 2025.

SOMA ZAIDI: Tume ya Taifa ya Uchaguzi Yafanikiwa Kuwaandikisha Watanzania Milioni 37.6

Idadi hiyo ya wapiga kura kwa mujibu wa Tume ni ongezeko la asilimia 26.55 kutoka wapiga kura wapatao milioni 29.7 waliokuwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2020.

Julai 29, 2025 chama cha upinzani CHADEMA ambacho kimeshikilia msimamo wa ‘No Reforms, No Election’ kupitia kwa mkurugenzi wake wa oganaizesheni na uchaguzi, John Pambalu kilitoa taarifa kwa umma na kukosoa takwimu zilizotolewa na Tume kwa kusema kuwa idadi hiyo ya wapiga kura inazidi makadirio ya wapiga kura yanayotokana na Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022. 

Kailima ambaye alisisitiza ufafanuzi huo alioutoa ni kwa lengo la kuondoa sintofahamu  kwa umma, alisema kuwa daftari la kudumu la wapiga kura kwa mujibu wa sheria linawekwa wazi na katika hatua zote za uboreshaji hakuna mtu aliyejitokeza kutaja orodha ya watu ambao wamezidi katika takwimu hizo.

“Juzi tarehe 27 [Julai 2025] Tume imetoa daftari la wapiga kura kwa vyama vya siasa [18] mpaka sahizi hakuna chama cha siasa kilichosimama mbele kikasema katika watu hawa hawa hawapo. Kwa hiyo, mkielewa mtawaelewesha vizuri wanapotoa takwimu zao muwaulize maswali ya namna hiyo hawataweza kufanya upotoshaji tena kuhusu daftari,” amesema Kailima.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×