The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Tume ya Taifa ya Uchaguzi Yamkabidhi  Samia  Fomu ya Ugombea Urais 2025

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais Samia, aliyeingia madarakani hapo Machi 19, 2021, kushiriki kwenye kinyang’anyiro cha Urais kama mgombea kwani mara zote alizoshiriki – alifanya hivyo akiwa mgombea mwenza wa hayati Rais Magufuli.

subscribe to our newsletter!

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) leo Jumamosi, Agosti 9, 2025, imemkabidhi fomu ya kugombea Urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, mgombea wa nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa nchi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, aliyeongozana na mgombea mwenza wake, Emmanuel Nchimbi, kwenda kuchukua fomu hiyo.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais Samia, aliyeingia madarakani hapo Machi 19, 2021, kufuatia kifo cha mtangulizi wake, John Magufuli, kushiriki kwenye kinyang’anyiro cha Urais kama mgombea kwani mara zote alizoshiriki kwenye zoezi hilo – 2015 na 2020 – alifanya hivyo akiwa mgombea mwenza wa hayati Rais Magufuli.

Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za CCM, jijini Dodoma Rais Samia aliwasisitiza wanachama wa chama hicho kuwa tayari kwa kampeni.

“Kama mnavyojua kwamba tumetoka kuchukua fomu na ndio maana tuko hapa. Wahenga walisema ukitaka uhondo wa ngoma. Sasa CCM tumesha ingia rasmi,” alieleza Samia mbele ya maelfu ya wafuasi wa chama hicho.

“Na tuko tayari kudemka jinsi ngoma itakavyopigwa. Tuko tayari kuicheza na kudemka. Nakishukuru kwa dhati, Chama, chama Mapinduzi, chama chetu, kwa imani kubwa walioonesha kwetu, mimi na mgombea mwenza, kuwania nafasi hii, ” aliongeza zaidi.

Katika hafla hiyo Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho John Mongella alitumia fursa hiyo kueleza kuwa chama hicho kilifuata kanuni na katiba katika uteuzi wa wagombea mnamo Januari 2025.

“Kupitia mkutano mkuu uliofanyika tarehe 18 mpaka 19 Januari mwaka huu. Mkutano huo ilitekeleza mambo makuu matatu; la kwanza ulikuchagua wewe mwenyekiti wetu wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa mgombea wa Kiti cha Urais…” alieleza Mongella.

Na kuongeza: “Pili ulipokea na kuthibitisha jina la Balozi Daktari Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, tatu ulimthibitisha DK. Hussein Ally Mwinyi …kuwa mgombea wa chama cha Mapinduzi wa kiti cha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Kimsingi kazi hizo tatu zilitekelezwa kwa kuzingatia Katiba ya chama chetu bila kukiuka ibara wala kanuni yeyote ile ya CCM,”

Hivi karibuni kumekuwa na mjadala juu ya uteuzi wa  wagombea wa CCM, mjadala huu umeibuka kufuatia ukosoaji mkubwa unaofanywa na aliyekuwa Msemaji wa Chama hicho na Mjumbe wa Kamati Kuu, Humphrey Polepole, aliyejiuzulu wadhifa wake wa ubalozi, akieleza suala kubwa ni kutokubaliana na mwelekeo wa uongozi katika chama chake na serikali.Mwanachama mwingine aliyevuliwa uanachama katika chama hicho, Godfrey Malisa naye ameenda mahakamani juu ya suala hilo.

Hatua ya kuchukua fomu Jumamosi inaonesha kwamba ni rasmi sasa CCM, chama tawala nchini Tanzania kwa takriban miongo sita sasa, kitawakilishwa na Samia kwenye kinyang’anyiro hicho, huku vyama vingine vya siasa vikiendelea kuteua watu watakaokwenda kupambana na mgombea huyo wa CCM kwenye uchaguzi huo.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×