The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Polisi: Hatuendi Vitani Lakini Tunaenda Kusimamia Usalama, Amani, Utulivu Kabla, Wakati na Baada ya Uchaguzi

Polisi wameeleza kuwa tayari wameweka mikakati ya kujiandaa na uchaguzi na kuhakikisha serikali inaingia madarakani bila kikwazo chochote

subscribe to our newsletter!

Akizungumza leo Agosti 11, 2025, katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi uliofanyika katika shule ya Polisi Moshi, Inspekta Jenerali wa Polisi, Camillus Wambura ameeleza kuwa hali ya usalama ni shwari na Jeshi hilo linajiandaa na uchaguzi kwa kuweka mikakati mbalimbali.

“Shughuli yoyote kubwa na muhimu ni lazima iwe na mipango mahususi, lazima iwe na mipango iliyopangiliwa kwajili ya kwenda kutimiza shughuli hiyo kwa umakini mkubwa, kwa kawaida hakuna vita inayopiganwa kwenye uwanja wa mapambano,” alieleza IGP Wambura katika shughuli hiyo ambayo Makamu wa Rais, Philip Mpango alikuwa mgeni rasmi.

“Vita yote hupiganwa mezani na pale mezani ndipo mikakati hupangwa na pale mezani, miongoni mwa mikakati inayopangwa ni kubaini nguvu ya adui ,kubaini vifaa anavyotumia adui, iliujue Je? wewe unahitajika kwenda na AK-47 au unahitajika kwenda na mizinga au kwenda na aina gani ya silaha lakini ni vizuri kujua idadi ya askari alionao adui na utakapofika vitani unachokwenda kufanya ni utekelezaji wa mikakati uliokwisha kujiwekea,” anendelea kufafanua IGP Wambura.

“Tumejipanga, tuna mikakati, tunakutana, tunaongea, tunajadiliana; hatuendi vitani lakini tunakwenda kusimamia usalama, amani, utulivu wa taifa letu kabla, wakati na baada ya uchaguzi,” alisisitiza Wambura.

Akieleza kuhusu hali ya usalama katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi, Wambura alieleza ni shwari, hata hivyo alifafanua walichukua hatua dhidi ya watu waliotoa kauli za kichochezi kwa mwamvuli wa siasa na demokrasia za harakati.

“Hivi karibuni ilijitokeza hali ya baadhi ya vikundi vya watu kwa mwamvuli wa siasa, demokrasia za uwanaharakati, kuanza kuleta taharuki ya kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani kwa kutoa maneno ya uchochezi katika majukwaa mbalimbali yakiwa na uelekeo wa kuvuruga amani ya nchi yetu,” Wambura alitoa taarifa.

“Tayari jeshi la Polisi imeshachukua hatua stahiki za kisheria katika kudhibiti vitendo hivyo vya uhalifu na sasa hali ni shwari na inaendelea kuwa shwari.”

Pamoja na kushukuru juu ya uwezeshaji wa kibajeti unaofanywa na serikali, Wambura alieleza kuwa Jeshi hilo linamuhakikishia Rais Samia Suluhu juu ya usalama na utulivu na kuhakikisha serikali inaingia madarani bila kikwazo chochote katika uchaguzi unaotegemewa Oktoba 29, 2025.

“Sisi hatuna wasiwasi, tunakuhakikishia na tufikishie salamu hizi kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwambie Jeshi lake la Polisi, mwambie tuko sawa,” Wambura alimueleza Makamu wa Rais Philip Mpango.

Na kuongeza: “Watanzania wote wawe na uhakika, Watanzania wote wawe na utulivu wakiamini kwamba kipindi hiki chote kitapita katika hali ya usalama, hali ya utulivu wa hali ya juu na tutapata kiongozi wa nchi yetu na serikali itaingia madarakani bila kikwazo chochote.”

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×