The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Mahakama Kuu Yaridhia Mashahidi wa Siri Kesi Nyingine ya Tundu Lissu

Katika uamuzi wake Jaji Elizabeth Mkwizu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam amesema kuwa maombi hayo hayakuwa na mashiko akibainisha kuwa uamuzi wa Mahakama ya Kisutu ulizingatia haki ya pande zote ikiwemo mshtakiwa kusikilizwa kwa usawa na usalama wa mashahidi.

subscribe to our newsletter!

Dar es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania imelitupilia mbali ombi la Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu aliyetaka mahakama hiyo kufanya mapitio ya uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kukubali mashahidi wa siri katika kesi inayomkabili ya kuchapisha taarifa za uongo katika mtandao wa Youtube, kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao namba 14 ya mwaka 2015.

Katika uamuzi wake Jaji Elizabeth Mkwizu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam amesema kuwa maombi hayo hayakuwa na mashiko akibainisha kuwa uamuzi wa Mahakama ya Kisutu ulizingatia haki ya pande zote ikiwemo mshtakiwa kusikilizwa kwa usawa na usalama wa mashahidi.

Akizungumza baada ya uamuzi huo, wakili wa Tundu Lissu Dkt  Rugemeleza Nshala amesema kuwa hawakubaliani na uamuzi huo wa Jaji Mkwizu na hivyo watashauriana na mteja wao kwa hatua zaidi kama ya kukata rufaa.

Nshala amepinga utetezi wa Jamhuri wa kutaka mashahidi ambao ni raia watakaotoa ushahidi wao kwa kificho kwa madai kuwa wamekuwa wakipokea vitisho jambo ambalo. Dkt Nshala anasema kitendo anachoshitakiwa nacho mteja wao kilifanyika kwa uwazi mbele ya umma na hivyo wanashangaa kwa nini upande wa mashitaka unataka kuleta mashahidi kwa kificho.

“Kama ni mashahidi kila mtu aliyesikia hotuba Ile ni shahidi na kama ni vitisho basi vitisho hivyo ni nani amemtisha mwenzake? Ni vigumu  sana kuweza kuamini, mimi ningeweza kufahamu kwamba ni wewe au yule atayekuwa shahidi wa kesi. Kwa hiyo, tunafikiri kwamba kuna vitu ambayo  haviko sawa na ni vyema vikawekwa hadharani na vikawekwa mbele ya mahakama iliyoko juu na Mahakama nyinginezo za kikatiba kuweza kuangalia kwanza ukatiba wa mashtaka haya na mashtaka ambayo yanamkabili mteja wetu, sana katika hizo kinga zinazotolewa kuhusiana na kinachoitwa kuwalinda au kuwaficha mashahidi,” amesema Dkt Nshala.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×