The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Simbachawene Atenguliwa: Hii Hapa Toka Ingia Yake Kwenye Baraza la Mawaziri

Utenguzi huu wa Simbachawene unaonesha panda shuka yake katika safari ya kisiasa hususani katika nafasi ya Uwaziri. Kwani kwa nyakati tofauti amewahi kuondolewa kwenye Barazala Mawaziri na kisha kurejeshwa tena.

subscribe to our newsletter!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Boniface George Simbachawene.

Nafasi ya Simbachawene imezibwa na Patrobas Katambi ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye sasa ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu.

Simbachawene ambaye ni mbunge wa Kibakwe aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Rais Samia alipotangaza Baraza lake la mawaziri  Novemba 17, 2025. Hii ni baada ya Rais Samia kuapishwa Novemba 3, 2025 kuendelea na muhula wa pili wa urais.

Toka Ingia ya Simbachawene kwenye Uwaziri

Utenguzi huu wa Simbachawene unaonesha panda shuka yake katika safari ya kisiasa hususani katika nafasi ya Uwaziri. Kwani kwa  nyakati tofauti amewahi kuondolewa kwenye Barazala Mawaziri na kisha kurejeshwa tena.

Licha ya kuwa mbunge tangu mwaka 2005, safari yake kwenye Baraza la Mawaziri  ilianza kipindi cha pili cha awamu ya nne cha Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, ambapo aliwahi shika nafasi kama Naibu Waziri wa Ardhi, Naibu Waziri wa Nishati na Madini na badae Waziri wa Nishati na Madini.

Katika kipindi cha awamu ya tano cha Hayati John Magufuli aliyeingia madarakani mwaka 2015, Simbachawene aliteuliwa kuwa Waziri wa TAMISEMI hadi Septemba 7, 2017 alipolazimika kujiuzulu baada ya ripoti ya Kamati ya  Bunge ya Uchimbaji wa madini ya Tanzanite na Almasi iliyobaini hasara wakati wa awamu ya nne ambapo Simbachawene alikuwa Waziri wa Nishati na Madini. Kutokana na ripoti hii ya Bunge, Simbachawene alijiuzulu kufuatia maelekezo ya Rais Magufuli kutaka uwajibikaji wa viongozi waliokuwepo kwenye Wizara ya Nishati na Madini kipindi ambacho ripoti ya Bunge imetaja Serikali kupata hasara katika biashara ya Tanzanite na Almasi.

Haikumchukua muda mrefu baada ya kukaa nje ya Baraza, Julai 21, 2019 rais Magufuli alimteua kuwa Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akichukua nafasi ya January Makamba ambaye uteuzi wake ulitenguliwa. Na  Januari 23, 2020 Simbachawene aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya ndani kuchukua nafasi ya Kangi Lugola ambaye naye uteuzi wake ulitenguliwa.

Simbachawene aliondolewa Wizara ya Mambo ya Ndani Januari 2022 katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais Samia na kupelekwa Wizara ya Katiba na Sheria na badaye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Katika kipindi cha awamu ya pili cha Waziri wa Mambo ya ndani, Simbachawene alikuwa akikabiliwa na changamoto kubwa kutokana na nchi kutoka katika kipindi kigumu cha uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 uliokumbwa na maandamano pamoja na mauaji. Jambo lililopelekea katika kazi zake za mwanzo kama Waziri mara kadhaa amenukuliwa akisisitiza masuala kadhaa kama vile wananchi kurudisha imani kwa vyombo vya usalama wa raia pamoja na mageuzi kwenye vyombo hivyo  kuanzia utendaji wake na maslahi ya watumishi wa vyombo.

Mabadiliko na teuzi nyingine

Katika taarifa ya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri, piia, Prof. Palamagamba John Aidan Kabudi ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu ( Kazi Maalum) kutoka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nafasi ambayo imechukuliwa na Paul Makonda aliyekuwa Naibu Waziri.

Naye Denis Lazaro Londo ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara kutoka Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nafasi ambayo imechukuliwa na Ayubu Mohamed Mahmoud.

Pia Rais Samia ameteuwa mabalozi kadhaa ikiwemo Zena Ahmed Said, Wazir Rajab Salum na Meja Jenerali Mbaraka Mkeremy.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×