The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

TAKUKURU Yatangaza Kuwatafuta Alex Msama wa Matamasha ya Pasaka na Benny Mwita Sammoh

Wawili hao wanatafutwa kwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu

subscribe to our newsletter!

TAKUKURU imetangaza kuwatafuta Alex Msama Mwita, maarufu kwa uandaaji wa matamasha ya pasaka, pamoja na Benny Mwita Sammoh kufuatia mashataka yanayowakabili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

TAKUKURU wanaeleza kuwa shauri juu ya watuhumiwa hao limefunguliwa Januari 21, 2026, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Hassan makube. Sababu kubwa ya shauri hili ni matokeo ya ya uchunguzi wa tuhuma kuhusiana na kiwanja namba 33 kilichopo Vijibweni Kigamboni, kiwanja chenye hati namba 129621 iliyotolewa kwa Africa Energy Limited.

Wawili hao wanadaiwa kughushi hati ya mauziano waliyoiwasilisha Baraza la Ardhi Temeke ikionesha Benny Mwita Sammoh amenunua kiwanja hicho kutoka kwa Mwinyikombo Wahela.

“Kufuatia wasilisho hilo katika Baraza la Ardhi Temeke, Benny Mwita Sammoh kwa kutumia jina lingine la Ben Samson alifanikiwa kuuza eneo hilo kwa kampuni ya World Oil Tanzania Limited na kujipatia jumla ya Tshs. 984,000,000 kati ya Tshs. 1,700,000,000/= zilizoainishwa kwenye mkataba wa mauzo,” taarifa ya TAKUKURU inaeleza.

“Ushahidi uliopatikana uanonesha kuwa Benny Mwita Sammoh alihamisha jumla ya Tsh. 370,000,000/= kati ya 984,000,000/= kwenda kwa Alex Msama, ikiwa ni sehemu ya fedha zilizotokana na mauzo ya kiwanja tajwa,” taarifa ya TAKUKURU inaongeza.

Taarifa ya TAKUKURU inaeleza kuwa baada ya uchunguzi kufanyika ukihusisha ofisi ya TAKUKURU Kinondoni na TAKUKURU Temeke, washitakiwa walitakiwa kuripoti ofisi ya TAKUKURU Disemba 2025, ili wafikishwe mahakamani jambo ambalo hawakulitekeleza.

TAKUKURU imetoa namba zao 0738150236 kwa yeyote mwenye taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa watuhumiwa.

Katika taarifa zingine, TAKUKURU inaeleza kuwa Alex Msama anatafutwa na TAKUKURU Kinondoni kwa ajili ya kujibu tuhuma za kughushi na uvamizi wa eneo la kiwanja namba 234 kilichopo Regent Estate Mikocheni.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×