The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Hifadhi ya Jamii kwa Wajasiriamali: Kinga, Fursa na Maendeleo ya Baadaye

Maisha ya ujasiriamali yamejaa misukosuko na kutokuwa na uhakika. Hifadhi ya jamii hutazamwa kama ngao ya kinga na chanzo cha matumaini wakati wa majanga.

subscribe to our newsletter!

Hifadhi ya Jamii ni mfumo rasmi wa kijamii na kiuchumi unaolenga kumpa mtu au familia ulinzi dhidi ya majanga ambayo yako nje ya uwezo wake na yanayoweza kusababisha kuporomoka kwa kipato. Majanga haya ni pamoja na: uzee, ulemavu, kifo, uzazi, ajali na magonjwa. 

Lengo kuu la hifadhi ya jamii ni kuhakikisha mtu anapokutana na janga la kijamii au kiuchumi, maisha yake hayaangukii kwenye umaskini wa ghafla na kwamba anayo kinga ya kumwezesha kuendelea kuishi katika maisha ya kawaida. Mfano wa mifuko ya hifadhi ya jamii Tanzania ni pamoja na NSSF kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, PSSSF kwa watumishi wa umma na NHIF kwa huduma ya Afya 

Kwa nini wajasiriamali wanahitaji Hifadhi ya Jamii? 

Katika uchumi wa kisasa, wajasiriamali ndio injini inayozalisha ajira na kukuza Pato la Taifa (GDP). Hata hivyo, kundi hili mara nyingi liko kwenye “mstari wa mbele wa majanga.” 

Tofauti na waajiriwa wenye mshahara wa kudumu, mjasiriamali hutegemea afya yake na nguvu zake za kila siku ili kupata mkate. Ikitokea dharura au janga, mafanikio yote ya miaka mingi yanaweza kupotea kwa muda mfupi.

Wajasiriamali na sekta isiyo rasmi ikijumuisha makundi kama:Madereva bodaboda, mama lishe, machinga, wakulima wadogo, wavuvi wadogo, fundi seremala, fundi cherehani, wafugaji, wasanii na wabunifu. 

Kundi hili linahitaji kutambua kuwa hifadhi ya jamii si anasa wala si kitu cha watu wa ofisini pekee, bali ni hitaji la msingi kwa usalama wa sasa na wa baadaye katika maisha yao na familia zao kwa ujumla.

Maisha ya ujasiriamali yamejaa misukosuko na kutokuwa na uhakika. Hifadhi ya jamii hutazamwa kama ngao ya kinga na chanzo cha matumaini wakati wa majanga. Miongoni mwa faida hizo ni pamoja na:

Mosi, ni uhakika wa kipato utakapofikia uzee. Watu wengi hufikiri watafanya biashara milele, lakini uzee ni safari isiyoepukika ambapo nguvu ya kuendelea kufanya kazi hupungua. Hivyo Kupitia hifadhi ya jamii, mjasiriamali anapotimiza umri wa kustaafu anapata malipo ya pensheni ya kiinua mgongo na kila mwezi mpaka atakapo fariki. Hii inamfanya aishi kwa heshima bila kuwa mzigo kwa watoto au kutegemea misaada ya ndugu.

SOMA ZAIDI: Je, Wafanyakazi Wanakumbuka Kuomba Fidia Pale Wanapopatwa na Majanga wakiwa Kazini?

Mbili, ni ulinzi wa Familia kupitia fao la warithi. Endapo mjasiriamali anayechangia katika Mfuko wa hifadhi ya jamii atafariki, michango yake haitapotea. Familia kwa maana ya mke au mume na watoto) watalipwa mafao ya urithi. Hii inahakikisha kuwa ndoto za watoto kama elimu haziishii pale mtafutaji mkuu anapopoteza maisha.

Tatu, kupata huduma za matibabu. Mjasiriamali anapougua, gharama za matibabu zinaweza kumaliza mtaji wote wa biashara. Kupitia NHIF au kupitia mafao ya NSSF mjasiriamali anapata kadi ya bima ya Afya, inayomwezesha kutibiwa yeye na familia yake bila kuathiri mtaji wake, hivyo biashara huendelea kuishi.

Nne ni kinga dhidi ya ulemavu wa kudumu chukulia mfano vijana wa bodaboda au mafundi ujenzi, hatari ya ajali ni kubwa. Ikitokea mwanachama amepata ulemavu wa kudumu, hifadhi ya jamii hutoa Pensheni ya Ulemavu. Mwanachama hupata kiinua mgongo na malipo ya kila mwezi mpaka kifo chake, jambo linalookoa familia yake kutumbukia kwenye umaskini uliokithiri na kutokuwa mzigo kwa jamii.

Tano, kwa wanawake wajasiriamali kuna Fao la Uzazi. Mjasiriamali anapojifungua, biashara mara nyingi husimama au kudhoofika lakini kama mjasiriamali huyo atakuwa kwenye Hifadhi ya jamii, atapatiwa fursa ya kupata mafao ya uzazi, ili kulinda afya ya mama na mtoto huku biashara ikibaki salama.

Sita, ni fursa ya kupata dhamana ya mikopo na ukuaji wa biashara. Mifuko ya hifadhi ya jamii sasa inashirikiana na mabenki ambapo michango ya mwanachama inaweza kutumika kama dhamana kwa kimombo collateral. Fursa: Inakuwa rahisi kwa mjasiriamali kupata mkopo kutokana na michango yake aliyokuwa akichangia katika Mfuko wa hifadhi ya jamii.

Jinsi ya Kujiunga na Mifumo ya Hifadhi ya Jamii

Tanzania, mifuko ambayo imefungua milango kwa wajasiriamali na sekta isiyo rasmi ni NSSF. Wameanzisha Skimu ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii kwa Waliojiajiri (Hifadhi Scheme) ili kuwawezesha wajasiriamali na wananchi wa sekta isiyo rasmi kupata kinga dhidi ya majanga. 

SOMA ZAIDI: Unataka Kuomba Fao la Urithi Kutoka NSSF? Soma Hapa Kufahamu Zaidi

Mtu yeyote mwenye umri kati ya miaka 15 hadi 70 anaweza kujiunga kwa taratibu ambazo zimewekwa na NSSF. Baada ya kusajiliwa, mwanachama huchangia kuanzia Tsh 30,000 au 52,200 au zaidi kwa mwezi, kulingana na uwezo wake. Kupitia skimu hii, mwanachama anapata faida/mafao kama pensheni ya uzee, ulemavu, urithi, bima ya matibabu, uzazi, msaada wa mazishi na mafao ya kujitoa.

Pia Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) unatoa bima kwa mtu binafsi kama bodaboda, mama lishe, machinga na wakulima, pamoja na familia. Ili kupata bima ya Afya, unatakiwa kufuata taratibu ambazo zimewekwa na NHIF kwa kufika Ofisi zao kutembelea Kurasa zao za mitandao ya kijamii. Bima hii humsaidia mjasiriamali kulinda mtaji na maisha katika kipindi cha ugonjwa au dharura.

Nihitimishe kwa kusema kuwa Hifadhi ya jamii kwa mjasiriamali si jambo la hiari tena katika ulimwengu wa sasa wenye mabadiliko ya haraka. Ni daraja linalounganisha jitihada za leo na usalama wa kesho. Mjasiriamali mwenye kinga zidi ya majanga ana amani ya nafsi, na amani hiyo ndiyo chimbuko la ubunifu na ukuaji wa uchumi wa taifa.

Thomas Ndipo Mwakibuja ni mtaalamu wa hifadhi ya jamii. Kwa mrejesho, anapatikana kupitia thomasmwakibuja@gmail.com au +255 767 879 281.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×