The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Waziri Mkuu Akanusha Tetesi za Dhahabu ya Benki Kuu Kuuzwa Kinyemela na Mtu Binafsi

Ni kufuatia tetesi kuwa dhahabu ya Tanzania iliuzwa na mtu binafsi katika moja ya nchi Mashariki ya Kati

subscribe to our newsletter!

Akijibu swali aliloulizwa juu ya tetesi za dhahabu ya Benki Kuu kuuzwa, Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba amekanusha jambo hilo. Ambapo ameeleza kuwa dhahabu iliyopo Benki Kuu, ipo kama nyenzo ya sera ya kifedha nchini, ambapo miamala yake lazima ijulikane na taasisi za Kimataifa ikiwemo IMF na Benki ya Dunia.

Waziri Mkuu ametoa majibu hayo leo June 18, 2026, kufuatia kusambaa kwa tetesi mtandaoni kuwa dhahabu ya Benki Kuu iliuzwa katika moja ya nchi iliyopo Mashariki ya Kati, huku mtu binafsi asiye mtendaji wa serikali akitajwa kuongoza huo mchakato.

“Dhahabu haiuzwi na mtu binafsi na wala haiuzwi kwa mtu hivi binafsi. Hawezi mwanaharakati akaona dhahabu iliyouzwa, IMF wasione,World Bank wasione,” Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba alieleza.

“Na kwamba mtu tu anaweza akaondoka na kikapu hivi kimebeba dhahabu. Hayo ni mambo tu ya watu wenye ajenda rasmi ya kutengeneza mitafaruko na kutengeneza chuki ndani ya nchi na kutengeneza mizozo,” alieleza Waziri Mkuu.

Toka Benki Kuu ianze kununua dhahabu manamo Oktoba 2023, imeweza kukukusanya dhahabu takribani Tani 27.5 mpaka kufikia mwezi Juni 2026.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×