The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Nondo Aibua Utata wa Mikopo ya Vijana, ACT Wazalendo Yalalamikia Idadi Ndogo ya Vijana Walionufaika

Katika maelezo yake, Nondo amesema kati ya vijana 30,384 walioomba mikopo, ni vijana 78 pekee waliopata mikopo hiyo sawa na asilimia 0.30, tofauti na idadi ya wanufaika 1,961 iliyotangazwa na wizara hiyo.

subscribe to our newsletter!

Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Taifa ya ACT Wazalendo, Abdul Nondo amesema utoaji wa mikopo kwa vijana iliyotangazwa na Wizara ya Maendeleo ya Vijana haifanani na uhalisia wa idadi ya maombi yaliyowasilishwa na vijana.

Nondo ameyasema hayo  Mei 8, 2026 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam kufuatia Wizara ya Maendeleo ya Vijana kutoa orodha ya vijana waliopata mikopo ya uwezeshaji waliyoitangaza.

Katika maelezo yake, Nondo amesema kati ya vijana 30,384 walioomba mikopo, ni vijana 78 pekee waliopata mikopo hiyo sawa na asilimia 0.30, tofauti na idadi ya wanufaika 1,961 iliyotangazwa na wizara hiyo.

Mwenyekiti huyo wa vijana wa ACT Wazalendo ameita hatua hiyo kuwa ni “maigizo” kwenye utoaji wa mikopo ya vijana.

Taraifa iliyotolewa na Wizara ya Maendeleo ya Vijana zinaonesha kuwa Serikali  ilifungua rasmi dirisha la maombi ya mikopo kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana chini ya mpango wa kukopesha vijana na wanawake shilingi bilioni 200 uliotangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan. 

Dirisha hilo la maombi ya mkopo lilifunguliwa Machi 21, 2026 kwa mujibu wa tangazo hilo, vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35 walitakiwa kuwasilisha maombi ya mikopo kwa ajili ya miradi ya biashara, uzalishaji na utoaji huduma, huku waombaji wakitakiwa kuwa na NIDA, andiko la mradi, eneo la biashara linalotambulika pamoja na akaunti ya benki au namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina lao. Mwisho wa utumaji wa maombi wa mikopo hii ilikua April 3, 2026.

Hata hivyo, katika taarifa ya matokeo ya awamu ya kwanza ya mikopo hiyo iliyotolewa Aprili 28, 2026, Serikali ilikiri kuwa waombaji wengi walikumbwa na changamoto za uandishi wa miradi na kutowasilisha nyaraka kwa usahihi, jambo lililosababisha Serikali kutangaza mpango wa mafunzo maalum kwa vijana kabla ya awamu nyingine za mikopo.

Taarifa hiyo pia ilieleza kuwa baadhi ya maombi yaliyofaulu yaliwasilishwa benki ya CRDB kwa hatua za uhakiki kabla ya wanufaika kupewa mafunzo ya biashara, matumizi sahihi ya mkopo na elimu ya fedha.

Katika orodha ya wanufaika wa awamu ya kwanza, miradi mbalimbali ilitajwa kunufaika ikiwemo kilimo, viwanda, mifugo, uvuvi pamoja na biashara ndogo ndogo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo jumla ya wanufaika 1,961 kutoka mikoa mbalimbali waliingizwa kwenye hatua ya kwanza ya uchambuzi na uhakiki wa mikopo hiyo.

Ni katika mazingira hayo, Nondo amesema Serikali inapaswa kuhakikisha mikopo hiyo inawafikia vijana wengi kwa uwazi na ufanisi badala ya kubaki kwenye matangazo na ahadi zisizoleta matokeo kwa vijana wanaokabiliwa na ukosefu wa ajira na ugumu wa mitaji.

Kwa mujibu wa ACT Wazalendo, matumizi ya neno “wanufaika” katika orodha iliyotolewa na wizara ni namna ya kuficha idadi halisi ya vijana waliopata mikopo hiyo.

“Mimi katika orodha mbele ya jina langu wameongeza watu 10, wanawake watatu na wanaume saba ambao siwajui na sijui wametoka wapi,” amesema Nondo.

Aidha, ACT Wazalendo imeitaka Serikali kuweka wazi orodha halisi ya vijana waliopata mikopo pamoja na kiasi cha fedha walichopewa kila mmoja ili kuongeza uwazi na uwajibikaji.

Pia, chama hicho kimetaka kufunguliwa kwa dirisha la pili la maombi ya mikopo kwa vijana ambao hawakupata nafasi katika awamu ya kwanza huku kikitaka kuondolewa kwa sharti la leseni ya biashara kwa vijana wanaoanza biashara.

Mbali na suala la mikopo, Nondo pia amezungumzia kupanda kwa bei ya mafuta nchini, akisema hali hiyo inaongeza gharama za maisha kwa wananchi wa kipato cha chini na kuathiri usafiri pamoja na bei za bidhaa mbalimbali.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×