The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Mnyukano wa kisheria waibuka Mahakamani Kutekwa Twaha Mwaipaya: Mahakama Yaamuru IGP Kenya Afike Mahakamani

Mahakama imeeleza utetezi wa kuwa Polisi Kenya hawamshikilii Mwaipaya hautoshi

subscribe to our newsletter!

Mahakama Kuu nchini Kenya imeagiza leo Novemba 02, 2026, kuwa Mkuu wa Polisi Kenya, IGP Douglas Kanja Kirocho afike Mahamani kesho saa nne na nusu asubuhi kwa ajili ya kutoa ripoti juu ya alipo Twaha Mwaipaya aliyeripotiwa kutekwa Oktoba 25, 2026, huko nchini Kenya.

Mahakama iliagiza mnamo Oktoba 30, 2026, kuwa IGP Kenya, pamoja na DCI wafike Mahakamani leo au kutuma mwakilishi, ambapo leo wawili hao waliwakilishwa na Wakili wa serikali aliyefahamika kwa jina la Marwa.

Katika taarifa yake Marwa ameeleza kuwa uchunguzi wa jambo hilo unaendelea na kuwa jitihada zimefanyika ikiwa na pamoja na kuandikia barua kampuni za simu ikiwemo Airtel na Safaricom juu ya suala hilo, lakini na pamoja na kampuni ya Bolt. Inaelezwa katika siku ambayo Mwaipaya alitekwa alikuwa pamoja na Apolinary Boniface Margwe, wakitumia Bolt, ambapo Margwe aliweza kukimbia ambaye ndio shahidi katika kesi hii.

Mawakili wa Mwaipaya akiwemo kiongozi wa chama cha People’s Liberation Party (PLP), ambaye pia aliwahikuwa Waziri wa Sheria Kenya, Martha Karua pamoja na wakili Abner Mango walipinga vikali utetezi ulioletwa.

“Tunakuomba utoe amri sasa kwamba IGP na DCI wafike wao wenyewe ili waieleze mahakama hii kwamba Polisi hawawezi kutekeleza jukumu walilopewa au waliokabidhiwa na Katiba,” Karua aliieleza Mahakama. “Kwa sababu ikielezwa jambo kama hilo [utekaji] linaweza kutokea, la aina hiyo, na hawajui yuko wapi, ni wanasema kwamba hawawezi kutekeleza wajibu wao.”

Baada ya kusikiliza pande zote, Jaji Alexander Muteti alichambua hoja za pande zote, huku akitambua jitihada zilizofanywa na DCI na IGP kuleta uwakilishi Mahakamani.

“Kenya kama nchi imekuwa mwenyeji wa wakimbizi wengi kutoka nchi jirani, kama vile Somalia na Sudan Kusini. Litakuwa jambo la kutia wasiwasi mkubwa iwapo itabainika, kama inavyodaiwa na mleta maombi, kwamba mhusika alirejeshwa Tanzania bila kufuata utaratibu halali wa kisheria,” ameeleza Jaji Muteti.

“Kenya iliridhia Mkataba wa mwaka 1951 kuhusu Hadhi ya Wakimbizi, ambao unakataza nchi mwanachama kumfukuza au kumrejesha mkimbizi katika maeneo ambayo maisha yake yatakuwa hatarini kwa sababu ya dini yake au utaifa wake, uanachama wake katika kundi fulani la kijamii na, nasisitiza hilo, au maoni yake ya kisiasa,” aliendelea kufafanua.

“Mhusika [Twaha Mwaipaya] na Bw. Margwe Apolinary Boniface wanadaiwa kuangukia katika kundi la watu wanaoweza kukabiliwa na hatari ya kuteswa nchini Tanzania kutokana na uanachama wao na nafasi yao katika siasa za CHADEMA,” aliendelea kufafanua Jaji Muteti. “Hivyo, wanastahili kupewa ulinzi na serikali ya Kenya kwa muda wote watakaokuwa nchini. Kwa hiyo, haitoshi kwa mjibu maombi [DCI na IGP], kupitia Bw. Marwa, kusema kwamba mhusika [Twaha Mwaipaya]  hayupo mikononi mwetu.”

Kufuatia uchambuzi huo Jaji Muteti akakubaliana na maombi la mleta maombi waliotaka IGP afike Mahakamani, hata hivyo akasisitiza hakuna haja ya DCI kufika, kwa kuwa IGP anasimamia huduma zote za kipolisi Kenya.

“Kwa hiyo Mahakama hii inaona kwamba kuna msingi wa kumtaka Inspekta Jenerali wa Polisi afike mbele ya mahakama hii na aeleze iwapo serikali, kupitia mawakala wake, huenda ilimteka na kumrejesha mhusika kutoka nchi hii hadi nchini kwake bila kufuata utaratibu wa kisheria,” ameeleza Jaji Muteti.

Mleta mwaombi katika shauri hii kwa niaba ya Twaha Mwaipaya ni taasisi ya utetezi wa haki za binadamu ya Vocal Africa.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×