Mwanaharakati nguli na mwanahabari mzoefu Jenerali Ulimwengu ameeleza kuwa Watanzania wamepoteza uwezo wa kufanya mijadala na kwa sasa sehemu kubwa ya mijadala imekuwa ikifanyika kwa kukemeana.
“Tumepoteza uwezo wa kuzungumza wacha ile ya kusema kwamba una uhuru wa kuzungumza,” alieleza Jenerali Ulimwengu.
“Lakini hata uwezo wa kuzungumza na kujenga hoja nchi hii imepoteza. Tumeona juzi juzi tu hapa katika ile suala la bandari lililoibuka ghafla limetukuta kama vile tumeduwaa.”
Ulimwengu alikuwa kizungumza katika mjadala ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia (TCD) kuhusu hali ya demokrasi kuelekea uchaguzi wa mwaka 2024/25.
Jenerali ametolea mfano suala la Bandari kwa namna lilivyozua mjadala usiopata muafaka, “hii bandari ilivyoibua huu mjadala imetuonesha kwamba sisi ni kwama swala waliongia barabarani ghafla na tumekutana na mwanga mkali wa gari tunababaika.”
“Tumepoteza uwezo wa kujenga hoja. Tumefika mahala kwamba sasa Watanzania ni watu ama wa kufokeana ama kukaripiana ama kuonyana ama kutishana. Ama ilimradi hatuzungumzii hatujadiliani ila tunatoa vitisho, tunatoa makemeo na kadhalika.”
Ulimwengu ameelezea kwamba tamaduni hii ilikuja ndani ya miaka sita baada ya uminywaji wa majukwaa ya kujieleza na kuonya hata kwenye majadiliano ya katiba mpya yanaweza yasipate muafaka halii hii ikiendelea.
Unaweza kufuatilia mazungumzo yote ya Jenerali katika video hapa:
[bt_bb_section layout=”boxed_1200″ lazy_load=”yes” show_video_on_mobile=”” show_sticky=”show-top” show_previous_posts=”show” force_posts_show=”default” order_by=”default” border=”default” bb_version=”4.6.1″][bt_bb_row][bt_bb_column order=”0″ lazy_load=”yes” bb_version=”4.6.1″ width=”1/1″ width_xl=”1/1″ width_lg=”1/1″ width_md=”1/1″ width_sm=”1/1″ width_xs=”1/1″][bt_bb_video bb_version=”4.6.1″ video=”https://youtu.be/cptVEkJpJ6A” disable_controls=”no” responsive=”” publish_datetime=”” expiry_datetime=”” animation=”no_animation” el_id=”” el_class=”” el_style=””][/bt_bb_video][/bt_bb_column][/bt_bb_row][/bt_bb_section]