Kisukari: Ugonjwa Unaohitaji Nidhamu
Sukari inapokuwa nyingi katika damu, huathiri mfumo wa mzunguko wa damu kwa kuanzia kwenye mishipa midogo na mikubwa ya damu. Hiki ndicho kiini cha athari nyingi za kisukari zinazoonekana katika sehemu mbalimbali za mwili.