The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Leseni za Maudhui Mtandaoni Zafutwa, Ada Kwa Maudhui ya Habari Yapunguzwa kwa 50%

Maudhui ya ubunifu, ikiwemo video za Youtube kama za mapishi, mafunzo kwa watoto, urembo na sanaa hazitahitajika kulipiwa chochote. Maudhui ya habari gharama zake zimepunguzwa kwa asilimia 50.

subscribe to our newsletter!

Dar es Salaam. Hatimaye Serikali imesikiliza kilio cha muda mrefu cha warusha maudhui mtandaoni ambapo sasa maudhui yote isipokuwa ya habari na matukio hayatahitaji kuomba leseni.

Hata hivyo, hata kwa warusha maudhui wa habari na matukio ya sasa (news and current affairs), ada za leseni zimepunguzwa kwa asilimia 50.

“Kanuni ya maudhui za mtandao za mwaka 2020, kanuni hizi zimefanyiwa marekebisho kuboresha matumizi ya mtandao na hivyo kukuza fursa ya vipaji,” alisema Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye wakati wa kutangaza mabadiliko hayo.

“Marekebisho haya ni pamoja na haya yafuatayo. Kwanza tumeondoa leseni kwa watoa maudhui mbalimbali mfano mapishi, michezo, usanii ikiwemo mziki na filamu. Tumefuta hizo leseni kuruhusu watu wajiachie,” aliongeza Nnauye.

Hii inamaanisha kwamba maudhui mengi ya ubunifu, ikiwemo video za Youtube kama za mapishi, mafunzo kwa watoto, urembo na sanaa hazitahitajika kulipiwa chochote. Hapo mwanzo ilikuwa ili kurusha maudhui yoyote kwa vyombo kama Youtube ulihitajika kulipa Sh600,000 kwa ajili ya leseni.

“Kwa marekebisho haya habari na matukio ya sasa yaani news and current affairs ambazo hutolewa pia na vyombo vya kawaida ndio zitakazokatiwa leseni,” alisema Nnauye.

Hata hivyo, unafuu ulioletwa kwa warusha maudhui ya habari na matukio ya sasa ni kupunguzwa ada kwa asilimia 50.

“Tumepunguza [gharama] kutoka shilingi laki moja mpaka shilingi 50,000 lakini kutoka shilingi 1,000,000 ada ya mwaka mpaka shilingi 500,000,” anaendelea kutolea ufafanuzi Waziri Nnauye.

Hii inamaanisha kwa wanaomba leseni mpya sasa watalipa sh550,000 badala ya Sh1,100,000 na wanaoendelea watalipa Sh500,000 badala ya Sh1,000,000.

Mabadiliko mengine ambayo Serikali imetangaza ni pamoja na kuruhusu vyombo vya habari vya ndani kujiunga na vyombo vya habari vya nje bila kuhitaji kuomba kibali. Hata hivyo, mrusha maudhui atawajibika moja kwa moja na maudhui hayo.

Lakini pia zuio la kutoruhusu studio za vyombo vya habari kutembelewa na wageni wa nje ya nchi bila uwepo wa Afisa Serikali limeondolewa.

Mabadiliko mengine ni kurasimisha kisheria utaratibu wa vyombo vya habari kurusha matangazo ya redio kwa njia ya video, ambapo mwanzo hakukua na sheria inayoruhusu ingawa vyombo vingi vilikua vinafanya.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *