The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Wadau Wataka Mikakati Imara Kuongeza Ushiriki wa Wanawake Kwenye Uongozi

Ushiriki hafifu wa wanawake kwenye uongozi wa kisiasa umehusishwa na ukatili na unyanyasaji wanawake wanakumbana nao.

subscribe to our newsletter!

Dar es Salaam. Serikali imeshauriwa kuja na mikakati madhubuti itakayosaidia kukabiliana na unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake, hususan wale wanaojihusisha na siasa, huku wadau wakiamini kufanya hivyo kutawaongezea wanawake kushiriki kwenye uongozi wa kisiasa, hususan ule wa ngazi za chini.

Wito huo umetolewa leo, Agosti 9, 2023, kwenye kikao kilichofanyika mkoani mjini hapa kilichoandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali kujadili mikakati muhimu ya kukabiliana na suala hilo.

Ushiriki wa wanawake katika siasa nchini Tanzania unatajwa kuwa mdogo hasa katika ngazi za mitaa na kata. Hali hii imehusanishwa, pamoja na sababu nyingine, na uwepo wa uwiano mdogo kati ya ushiriki wa wanaume na wanawake katika ngazi hizo.

Takwimu zinaonesha katika ngazi ya vitongoji kuna viongozi wanawake 4,117 kati ya viongozi 58,441, sawa na asilimia 6.7. Kwa ngazi ya mitaa, wanawake wanatajwa kuwa 528 kati ya 4,117, sawa na asilimia 12.6.

SOMA ZAIDI: TGNP Yataka Wanahabari Kuchochea Ushiriki wa Wanawake Kwenye Uongozi

Akichangia mada kwenye kikao hicho, Neema Lugangira, Mbunge wa Viti Maalumu anayewakilisha mashirika yasiyo ya Kiserikali, aliihusisha hali hiyo na ukosefu wa wa sera ya jinsia katika vyama vingi.

Kwa mujibu wake, Lugangira alisema hali hiyo inadhoofisha ushiriki wa wanawake katika siasa kwani hupelekea matukio ya udhalilishaji dhidi ya wanawake kutokuchukuliwa kwa uzito, hali inayoondoa motisha kwa wanawake wengi kushiriki katika siasa.

“Sera za jinsia ni muhimu sana katika vyama vya siasa kwa sababu pale ambapo mwanamke awe ni kiongozi ndani ya chama ama jumuiya zake, anapopata unyanyasaji wa kijinsia ambao unaendana na kisiasa anaenda kulalamika wapi?,” aliuliza Lugangira.

“Lazima kuwe kuna mfumo, kama hakuna, unakuta [wanawake] hawalalamiki,” aliongeza. “Kwa hiyo, kukosekana hizo sera kunawarudisha nyuma na wanawake wengine wanapoona wengine wanafanyiwa hivyo vitu, hakuna uwajibiswahi, ina maana inafifisha jitihada za wanawake kujitokeza kuingia kwenye siasa.”

SOMA ZAIDI: Sheria za Uchaguzi, Vyama vya Siasa Kufanyiwa Marekebisho?

Naye Mkurugenzi wa Shirika la NDI, Sandy Quimbaya, ameeleza kuwa ili kuwe na mipango madhubuti ya kupambana na vitendo hivyo, shirika hilo lipo tayari kufanya tafiti juu ya vitendo hivyo vya ukatili kwa wanawake katika siasa nchini.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Evelyn Makala, ameeleza kuwa Serikali imepokea changamoto hizo kutoka kwa wadau na kuahidi kuchukua hatua stahiki kurekebisha hali hiyo.

“Changamoto zilizotolewa na wadau na maoni yenu tumeyachukua na tutayafanyia kazi,” alisema Makala. “Tutafanya hivyo kwa kushirikiana na wenzetu [kwenye] wizara nyingine na wadau wengine wa masuala ya usawa wa kijinsia ili tuwe na uwiano mzuri wa wanawake na wanaume katika ngazi za uongozi.”

Hadija Said ni mwandishi wa habari wa The Chanzo anayepatikana mkoani Dar es Salaam. Unaweza kumpata kupitia hadijasaid826@gmail.com

 

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts