The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Mjadala Ripoti ya CAG: Wezi Serikalini Wamejifunza Kuiba Kisheria?Mbunge Atoa Hoja

Mvutano umeibuka Bungeni baada ya Mbunge Anatropia Theonest kutoa taarifa kuwa wezi ndani ya serikali wamejua namna bora ya kuiba huku wakiwasilisha vielelezo vinavyofanya wasikamatwe.

subscribe to our newsletter!

Mvutano umeibuka Bungeni baada ya Mbunge Anatropia Theonest kutoa taarifa kuwa wezi ndani ya serikali wamejua namna bora ya kuiba huku wakiwasilisha vielelezo vinavyofanya wasikamatwe.

“Kwa mujibu wa CAG anasema hizo hati zimebadilika kwa sababu wezi wamejua namna nzuri ya kuiba au kutumia risiti kuwasilisha vielelezo,”alifafanua Anatropia.”Kwa mujibu wa CAG wanawasilisha vielelezo hata baada ya kufanya wizi.”

Baada ya taarifa hiyo Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo alisimama na kusema kuwa Mbunge huyo amesema uongo na kutaka uthibitisho toka kwa Mbunge aliyetoa taarifa.

Spika wa Bunge, Tulia Ackson, alipokea taarifa hiyo na kutolea ufafanuzi.

Spika Tulia alianza kwa kuuliza ni halmashauri ngapi zilipata hati safi, ambapo ilionekana halmashauri 170 kati ya 184 ambayo ni sawa na asilimia 92 zilipata hati safi.

Spika Tulia akaeleza:

“Kwa maelezo na kwa michango tuliyoanza nayo Alhamisi jana na leo na kwa namna ambavyo Wabunge wameeleza halmashauri zao zilivyo na changamoto hizi hati 170 ni hati safi.’

“Na huu unaoitwa wizi ubadhirifu umetokea kwenye hizo halmashauri hizi hati safi zimetolewa kwa muktadha upi? Ni kwa maana ya kwamba zinakaguliwa kwa utaratibu ule wa kawaida na kwa utaratibu ule wa kawaida wamefuata taratibu za upelekaji wa taarifa kwa CAG.

“Na kama hivi ndivyo kwa takwimu hizi zilizopo kwenye taarifa hii ya kamati na taarifa ya CAG ni dhahiri hawa wabadhirifu wamejifunza namna nzuri ya kutoa taarifa.”

Spika Tulia akahitimisha hoja kuwa kwa mazingira hayo inamuwia vigumu kusema kuwa Mbunge kasema uongo, huku Wabunge wengi wakishangilia.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *