The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Tunavyoweza Kuwafundisha Watoto Kuwa Salama Wakati Wanacheza

Usiwe mzazi au mlezi wa kumkaripia mtoto mara kwa mara, au kumkataza kufanya vitu vyote kwa sababu kuna hatari itakayoweza kumpata

subscribe to our newsletter!

Watoto hukua katika hatua tofauti tofauti. Hatua hizi hutofautiana na vitu vinavyowavutia pia hubadilika kadri umri unavyobadilika. Vitu vinavyomvutia mtoto mwenye umri wa miaka miwili hutofautiana na vitu vinavyomvutia mtoto mwenye umri wa miaka saba.

Mtoto wa miaka minne mpaka tisa, kivutio chake kikubwa ni michezo, hasa ile ya kuchangamana na watoto wenzake. Hii ni kwa sababu katika umri huo anakua na mihemko ya kutumia muda mwingi kucheza. Wakati huu pia watoto hutengeneza marafiki na kujifunza jinsi ya kuishi na watu.

Hivyo, mzazi au mlezi unapaswa kutambua kwamba kuna baadhi ya michezo ambayo ni hatarishi kwa mtoto, hata kama mtoto anaifurahia. Michezo hii inaweza ikawa muhimu kwa maendeleo yake ya kiakili na hata kiafya, lakini inahitaji usimamizi na umakini ili mtoto awe katika hali ya usalama.

SOMA ZAIDI: Fanya Hivi Kujenga Uhusiano wa Karibu na Mtoto Wako Pindi tu Anapozaliwa

Kama mtoto anapenda kuogelea, jaribu kutengeneza mazingira ya usalama kwenye maeneo ya bwawa la kuogelea, mfano, mipira au maputo yanayomsaidia kujishikilia endapo atajirusha kwenye maji. 

Mtoto anapotaka kujifunza baiskeli, msimamie ili  asianguke. Kila atakapokua anajifunza.  Usisahau kumtia moyo, na kumwambia kwamba anaweza. Ni vizuri kua na seti ndogo ya huduma ya kwanza endapo kitu chochote hatarishi kikitokea wakati wa kucheza.

Mazingira ya eneo ambalo mtoto wako anacheza yanahitaji kuwa salama. Tengeneza eneo maalum la mtoto kucheza, hii itakusaidia kufahamu mtoto anacheza wapi na usalama wa eneo hilo. 

SOMA ZAIDI: Je, ni Upi Umri Sahihi wa Kumpeleka Mtoto Shule ya Bweni?

Kama anacheza nje ya nyumba, basi hakikisha mahali hapo ni safi, majani siyo marefu na siyo karibu na sehemu ya kutupa taka au mfumo wa maji taka.

Kama mtoto anacheza sehemu za michezo, basi hakikisha unafuata taratibu au sheria za sehemu ambapo mtoto anacheza. Kwa mfano, mabwawa ya kuogelea yana sheria zinazokataza kudumbukia ndani ya maji, sehemu za watoto kuogelea ni tofauti na sehemu ya watu wazima, nakadhalika.

Hata sheria zinazoelekeza jinsi ya kucheza na watoto wengine ni muhimu sana kujilinda yeye na watoto wenzake. Pia, mnunulie mtoto vifaa vya usalama vya michezo kama vile helmeti, viatu vigumu, boya la kuogela na vinginevyo vitakavyomlinda.

SOMA ZAIDI: Mtoto Anapaswa Kuwafahamu Wazazi Wake, Ndugu na Familia Tandaa

Mwisho, usiwe mzazi au mlezi wa kumkaripia mtoto mara kwa mara, au kumkataza kufanya vitu vyote kwa sababu kuna hatari itakayoweza kumpata. Mjengee mtoto wako uwezo wa kujiamini kwa kumfundisha jinsi ya kuvifanya vitu hivyo kwa usalama.


Makala hizi za malezi huandaliwa na C-Sema, shirika lisilo la kiserikali linalojikita katika kuendeleza na kulinda haki za watoto Tanzania. Kwa maoni na ushauri, wapigie kwenye simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile, unaweza kuwapata kupitia kurasa za Facebook: Sema Tanzania, Twitter: @SemaTanzania, na kupitia barua pepe yao www.sematanzania.org.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *