The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Je, Unafahamu Asilimia 80 ya Malezi ni Mahusiano Kati ya Mzazi na Mtoto?

Tuelewe kwamba, malezi yanahitaji malengo na uvumilivu wa kutimiza malengo hayo.

subscribe to our newsletter!

Dk Laura Markham, mwanasaikolojia na mshauri wa malezi anayetambulika ulimwenguni, anasema kwamba asilimia 80 ya malezi ni mahusiano yaliyopo kati ya mzazi na mtoto wake na asilimia 20 ni vile mzazi anavyomwongoza mtoto. 

Markham, ambaye ameshauri maelfu ya wazazi duniani, anamaanisha kwamba watoto watakusikiliza na kufuata unachowaambia vizuri kama mahusiano yenu ni mazuri. Hata sisi watu wazima, aina ya mahusiano yetu na watu yanaashiria namna gani tunawasikiliza.

Kumuongoza mtoto katika maisha yake ni kitu chema lakini tusisahau kuwekeza katika mahusiano yetu na watoto wetu.

SOMA ZAIDI: Tunavyoweza Kuwafundisha Watoto Kuwa Salama Wakati Wanacheza

Tunasisitiza wazazi kuwasikiliza watoto kwa umakini waakiwa wanawaongelesha. Kwanza, kama mzazi jitahidi, kutenga muda maalum wa kuongea na mtoto. Kwa mfano, ukimaliza kazi au shughuli zako, ama wakati wa siku za mapumziko ukiwa umetulia, huu ni wakati mzuri wa kuzungumza na mtoto. 

Mkiwa mnazungumza, mtazame mtoto usoni, epuka kumkatisha, muulize maswali, na yeye akikuuliza maswali mjibu kwa utaratibu.

Mkubali mtoto wako kama alivyo na jaribu kudhibiti matarajio yako kwake. Watoto wanatofautiana na kila mmoja ana upekee wake. Ni vizuri ukamwonyesha mtoto wako kwamba unampenda jinsi alivyo kwa kuthamini vipaji vyake, tabia na upekee wake. 

SOMA ZAIDI: Fanya Hivi Kujenga Uhusiano wa Karibu na Mtoto Wako Pindi tu Anapozaliwa

Pia, hakikisha matarajio yako yanalingana na umri, uwezo na vipaji vya mtoto wako.

Mfundishe kuomba msamaha akikosea na kusamehe akikosewa. Muelezee umuhimu wa msamaha, kwamba hakuna mtu aliyekamilika na mara nyingine tunakosea. 

Hivyo, kuomba msamaha ni njia ya kurekebisha makosa na kujenga uhusiano imara. Pia, mfundishe mtoto jinsi ya kuelezea kosa lake na kuomba msamaha kwa kutumia maneno ya heshima. Unaweza kufanya hivyo kwa kutumia mifano hai kutoka maisha ya kila siku au hadithi.

Kumbuka kwamba mtoto wako anajifunza kutoka kwako. Unapogundua kwamba umemkosea mtoto wako, kuwa tayari kuomba msamaha. Pamoja na kuimarisha uhusiano wako na mtoto, tabia hii inaonyesha unyenyekevu na inamfundisha kwamba hata wazazi wanaweza kufanya makosa.

SOMA ZAIDI: Je, ni Upi Umri Sahihi wa Kumpeleka Mtoto Shule ya Bweni?

Ni muhimu kwa mzazi kutoa ahadi kwa mtoto ambazo unaweza kuzitekeleza, vinginevyo unaweza kuharibu uaminifu ambao mtoto wako anao kwako. Ikiwa kuna sababu ya kutokutekeleza ahadi yako, mueleze mtoto kwa utaratibu, kisha fanya bidii kutimiza ahadi hizo huko mbeleni.

Kutoa pongezi kwa mtoto wako anapofanikiwa ni njia nzuri ya kuonyesha kwamba unajali na kuthamini mafanikio yake, hata kama ni madogo. Hii itamjengea hisia za kujiamini na uthubutu katika maisha yake ya sasa na hata baadaye.

Tuelewe kwamba, malezi yanahitaji malengo na uvumilivu wa kutimiza malengo hayo. Hivyo, kama lengo lako ni kuwa na mahusiano mema na mtoto wako weka juhudi, unaweza!

Makala hizi za malezi huandaliwa na C-Sema, shirika lisilo la kiserikali linalojikita katika kuendeleza na kulinda haki za watoto Tanzania. Kwa maoni na ushauri, wapigie kwenye simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile, unaweza kuwapata kupitia kurasa za Facebook: Sema Tanzania, Twitter: @SemaTanzania, na kupitia barua pepe yao www.sematanzania.org.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *