
Waliotimkia CCM Kutoka ‘Kundi la Wabunge 19’ Wametoboa Mchujo wa Kamati Kuu CCM
Akitangaza majina ya wanachama wa CCM waliopita katika chujio la Kamati Kuu, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla amewataja wananchama wa CCM 11 waliotoka kundi la wabunge 19 waliopita kwenye mchujo wa ubunge wa majimbo na wawili wamepita kwenye mchujo wa ubunge wa viti maalum ngazi ya mkoa.








