The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Nini Kinasababisha Ugonjwa wa RedEye, Fanya Haya Kupata Ahueni.

ugonjwa huo kitaalamu huitwa Keratoconjunctivitis na unasababishwa na virusi vya adeno (adeno viruses)

subscribe to our newsletter!

Serikali imetoa tahadhari juu ya ugonjwa wa redeyes au macho mekundu, ugonjwa ambao umeendelea kusambaa katika miji mbalimbali katika siku za hivi karibuni.

Ugonjwa huu umeonekana kuikumba sio Tanzania pekee, hata nchini Kenya, jiji la Mombasa limeendelea kusumbuliwa na ugonjwa huu unaoambukizwa kwa kugusana.

Dalili na Chanzo cha Ugonjwa Huu

Akizungumzia kuhusu ugonjwa huo, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya Profesa Pascal Ruggajo ameeleza kuwa ugonjwa huo kitaalamu huitwa Keratoconjunctivitis na unasababishwa na virusi vya adeno (adeno viruses).

Rugagajo anaeleza kuwa dalili za maambukizi za ugonjwa huo huweza kuonekana kwenye jicho moja au macho yote mawili. Dalili nyingine ni pamoja na  jicho kuwa jekundu, kuwasha na kuchoma choma.

Macho kuvimba, macho huogopa mwanga, macho kutoa tongotongo nyeupe au za njano, na wakati mwingine asubuhi mgonjwa anaweza akashindwa kufungua macho kwa sababu kope za macho zinakuwa zimeshikana, lakini pia uwezo wa kuona unakua kama una ukungu.

Kwa wagonjwa wachache kunaweza kuwa na dalili za ziada ikiwemo homa, kuumwa kichwa, kuchoka kupitiliza na kuvimba matezi.

Inaweza kuchukua siku tano mpaka kumi na nne kwa dalili hizi kuonekana kwa mtu aliyepata ugonjwa huu, na husambaa kutoka mtu mmoja mpaka mwingine, anaeleza Daktari Bingwa wa Magonjwa ya macho Muhimbili, Dokta Joachim Kilemile.

Namna ya Kuzuia na Kutibu Ugonjwa Huu

Dk. Kilemile anaeleza hatua za kwanza za kuzuia ugonjwa huu ni kukata mnyoro wa ugonjwa huu kwa kupunguza uwezekano wa mikono kwenda kwenye macho, kunawa kwa maji na sabuni na kupunguza kushirikiana vitu vinavyohusisha eneo la uso kama leso, vipodozi au taulo.

“Ugonjwa huu ni wa virusi unaweza kupona wenyewe, ndani ya wiki mbili unaweza ukapona, wengine wanaweza Kwenda hadi wiki sita,” anaeleza Dk.Kilemile.

Kilemile ameshauri wanaoumwa ugonjwa huu kufika hospitali na kuwaona wataalamu watakaowapa tiba sahihi katika kupunguza madhila ya ugonjwa huu.

katika kuzuia maambukizi, Profesa Ruggajo alisema usafi ni muhimu na unasaidia kuzuia ugonjwa huo kusambaa kwa wengine. Ameshauri wananchi kutokutumia dawa zisizo rasmi na ambazo hazijaandikwa na daktari kwa wakati huo.

Lakini pia kutotumia dawa za macho anazotumia mgonjwa mwingine, ili kuepuka madhara kwa kuwa dawa za macho ni tofauti na kwa matumizi tofauti.

Jackline Kuwanda ni mwandishi wa habari wa The Chanzo anapatikana mkoani Dodoma. Unaweza kumpata kupitia jackline@thechanzo.com

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *