The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Serikali: Matukio 21 Ya Watu Kutekwa na Kupotea Yamepatiwa Ufumbuzi.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni ameeleza kuwa robo tatu ya matukio yaliyoripotiwa ya watu kutekwa na kupotea kwa mwaka 2023 tayari yamepatiwa ufumbuzi.

subscribe to our newsletter!

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni ameeleza kuwa robo tatu ya matukio yaliyoripotiwa ya watu kutekwa na kupotea kwa mwaka 2023 tayari yamepatiwa ufumbuzi.

“Sio kwamba labda watu wanapotea halafu hakuna kinachofanyika, watu hawawapati wahalifu, hawawapati wahanga sio sahihi, ameeleza Masauni.

Masauni alikuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima aliyeuliza na kutoa mfano kuhusu matukio ya utekaji Bungeni.

“Kuna taarifa za utekaji zimeanza tena katika nchi ya Tanzania, nakumbuka wiki mbili zilizopita, mtoto wa Muhammad Al-Jabriy wa Zanzibar Cable alitekwa kule Dar es Salaam, na maiti yake ikaja kuokotwa baadae imekatwa vipande vipande na macho yametobolewa,” alieleza Gwajima akiomba ufafanuzi wa serikali.

Akijibu swali hilo Masauni alieleza kuwa matukio 21 kati ya matukio 29 ya watu kutekwa na kupotea yalipatiwa ufumbuzi mwaka 2023.

“Kwa takwimu ambazo ninazo kuanzia Januari hadi Disemba 2023 kati ya matukio ambayo yanazungumzwa ya kusema watu wamepotea, haijulikani wameenda wapi haijulikani nini.Kati ya matukio 29, matukio 21 Polisi imebaini waliohusika.”

“Vyanzo vilivyobainika wivu wa mapenzi, ushirikina, kugombania ardhi, kujiteka, visasi, utapeli,” aliongeza.

Masauni pia kuwa amepokea malalamiko manne kuhusu matukio ya watu kupotea ambayo ameyaundia tume maalum.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *