The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Mpango Mkakati Wa Upatikanaji Wa Fedha Kwa Vijana Wazinduliwa Zanzibar

Mpango mkakati huo umelenga kuwawezesha vijana kuanzisha biashara na kuzisimamia huku wakijua hatua sahihi za kuendeleza biashara pamoja na kupata fedha kupitia taasisi za kiserikali na za binafsi.

subscribe to our newsletter!

Zanzibar. Shirika La Marekani La Maendeleo Ya Kimataifa (USAID) kupitia mradi wa Feed the Future limezindua mpango mkakati wa upatikanaji wa fedha kwa vijana ili kuwawezesha kujikwamua kupitia shughuli mbalimbali.

Mpango huo uliozinduliwa rasmi Machi 27,2023, katika ukumbi wa Golden Tulip, Zanzibar umelenga kuwawezesha vijana kuanzisha biashara na kuzisimamia huku wakijua hatua sahihi za kuendeleza biashara pamoja na kupata fedha kupitia taasisi za kiserikali na za binafsi.

Akizundua mpango huo Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi,Uchumi na  Uwekezaji Shariff Ali Shariff amesema mpango huu unaonesha njia ya kufikia malengo ya kila kijana ambaye ana ndoto za kujiajiri na kupata uwezeshaji.

“Kwa niaba ya serikali niwakikishie wadau na wafadhili wa mradi huu kuwa pesa ambazo zimetolewa leo hapa zitatumika ipasavyo kuhakikisha mpango wa upatikanaji wa fedha kwa vijana waliopo Zanzibar kwenye sekta ya kilimo na uvuvi basi zitawafikia,” alieleza Shariff.

Wakati mradi unafanyika Tanzania bara na Zanzibar, kwa upande wa visiwani mradi unawawezesha vijana kwenye sekta ya kilimo na ya uchumi wa bluu.

Mkurugenzi Mkazi wa USAID Graig Hart amesema mpango mkakati wa upatikanaji wa fedha kwa vijana ni jambo kubwa kufanyika  kwani unaonesha njia za kuanzisha wazo utekelezaji na upatikanaji wa pesa, “Kutokana na uwezeshaji wa vijana mpango huu ambao uko hatua kwa hatua utawasaidia svijana kujua ni wazo gani linaweza kukuvusha na kukunufaisha wewe binafsi pamoja na jamii inayokuzunguka,” alieleza Hart

Akizungumzia juu ya mradi huu Mkurugenzi wa Wakala wa Uwezeshaji Kiuchumi Zanzibar, Juma Burhan amesema kuwa wa uwezeshaji vijana kiuchumi ulianza rasmi pale mkataba huo uliposainiwa rasmi Mei 4,2023, baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na USAID ukiwa na lengo la kutoa mafunzo na ruzuku kwa vijana wapatao 1,400 kwa Zanzibar nzima.

“Mradi huu utaenda kuwasomesha vijana 700 Unguja na 700 Pemba.Ni wigo mpya wa kuongeza ujuzi kwa wajasiriamali ili kwenda kupata fedha katika sekta binafsi,” anaeleza Burhan.

Burhan ameongeza kuwa tayari vijana 156 kutoka Zanzibar wameshapatiwa mafunzo na kati yao 82 wamepatiwa mikopo kutoka Benki ya Amana.

Muundo wa mradi huo unaweka kuwepo na taasisi  binafsi zinazopewa ruzuku ili kuwawezesha vijana katika mafunzo ujuzi wa biashara na kuwasaidia kujisajili pamoja na kupata nembo ya ithibati kwa ajili ya bidhaa wanazozalisha. Taasisi tano zimepokea ruzuku Zanzibar ikiwemo Jumuiya ya Kitaifa  ya Wafanyabiashara Zanzibar waliopokea shilingi milioni 297.

Hamad Hamad ni Mkurugenzi wa Jumuiya ya Kitaifa ya Wafanyabiashara Zanzibar amesema fedha hizo watazielekeza kwa vijana ambao wamejikita katika masuala mawili ya kilimo na masuala ya uvuvi kwenye sekta ya uchumi wa buluu pia zinatoa mafunzo maalum ya kuipa thamani bidhaa wanazozalisha. 

Arafa Barak ni Wazilishi wa Taasis ya Mbolea ya  Asilia Zanzibar akiwa mnufaika wa mafunzo hayo amesema serikali iangalie suala la kuweka uwazi kwenye kuwasaidia vijana na kuwalea hadi kufikia njia ya kuona ni kwa kiasi gani  bidhaa na huduma zao zinatambulika na kuuzika.

 “Suala la elimu na uwezeshaji ni jambo moja ila suala la kuwezeshwa kuwafikia wateja ni jambo ambalo kama vijana linatukwamishwa sana kufikia ndoto zetu,” anaeleza Arafa.

Mradi huo unakusudia kuhakikisha jumla ya wajasiriamali 3000 wanaweza kupata mitaji yenye thamani ya walau Bilioni 6 huku ajira 15,000 zikitegemewa kutengenezwa.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *