The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Ripoti ya Haki za Binadamu: Ukeketaji Bado Upo, Unafanyika Kwa Siri

Ngariba wanaotekeleza matukio haya wanatajwa kubuni njia mpya hasa hasa huko mkoani Singida na ili kuhakikisha kuwa ‘mila hiyo inafuatwa’

subscribe to our newsletter!

Ripoti ya Haki za Binadamu (2023) inaonesha ukeketeji bado upo katika jamii, huku wanajamii hao wakifanya kuwa suala la siri ya jamii nzima

Ripoti hiyo inataja kuwa kwa nchi nzima kwa mwaka 2023 yaliripotiwa matukio 76 ya ukeketaji kutoka mkoa wa Mara,Dodoma, na Singida huku waathirika wote wakiwa ni wasichana wadogo.

Ripoti hiyo iliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Kupambana na Changamoto za Vijana Zanzibar (ZAFAYCO) na Kituo cha Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC) Tanzania bara, inafafanua kuwa kwa mkoa wa Dodoma, ukeketaji umekithiri katika maeneo ya Chemba, Kondoa na Kongwa.

Takwimu zaa hivi karibuni za serikali zinaonyesha kupungua kwa kasi matukio ya ukeketaji nchini kwani, kiwango cha ukeketaji kimeshuka kutoka 18% mwaka 1996 hadi 8% mwaka 2022, na kuashiria kupungua kwa asilimia 10.

Hata hivyo ripoti ya haki za binadamu ya mwaka 2023 inaonyesha kwamba kiwango cha ukeketaji ni mara tatu zaidi katika maeneo ya vijijini ikilinganishwa na maeneo ya mijini, huku Kanda za Kati na Kaskazini zikiwa na viwango vya juu zaidi.

Mikoa ambayo ukeketaji ulikuwa umekithiri hapo awali, kama Manyara, Arusha, na Mara, yote kwa pamoja imeonyesha maendeleo makubwa, huku matukio yakiripotiwa kupungua.

“Wakati inadhaniwa wasichana wako salama dhidi ya ukeketaji nchini, mwaka 2023 jumla ya wasichana 71 wilayani Tarime mkoani Mara waligundulika kufanyiwa kitendo hicho, mara tu waliporudi nyumbani kipindi cha likizo,” inaeleza ripoti hiyo.

Ngariba wanaotekeleza matukio haya wanatajwa kubuni njia mpya hasa hasa huko mkoani Singida na ili kuhakikisha kuwa ‘mila hiyo inafuatwa’. Ripoti ya haki za binadamu ya mwaka 2023 inafafanua kuwa watu hawa wanalazimika kuwa ‘wabunifu zaidi’ kwa kuwa wanajua kwamba wanafuatiliwa na serikali pamoja na asasi mbalimbali za kiraia.

Mashirika yasiyo ya kiserikali na mabingwa wa kupinga ukeketaji katika mikoa mbalimbali pia wamepongeza hatua iliyofikiwa na kusisitiza haja ya kuwepo kwa sheria mahususi ya kupinga ukeketaji ili kuimarisha zaidi juhudi dhidi ya mila hiyo ma. Wanakiri kwamba licha ya kwamba changamoto bado zimesalia, ikiwa ni pamoja na matukio ya ukeketaji kufanywa kwa usiri mkubwa, mwelekeo ni mzuri na unaonyesha mabadiliko.

“Kuna visa vichache vya ukeketaji vinavyoripotiwa, lakini hiyo haimaanishi kwamba havifanyiki tena, badala yake vinafanyika kwa usiri mkubwa, kama vile biashara ya bangi” inasomeka ripoti hiyo ikimnukuu Afisa wa NGO moja huko Manyoni, Singida.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *