The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Kamata Kamata ya Wanachama na Viongozi wa CHADEMA Yaendelea. Lissu, Mnyika na Sugu Wakamatwa

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA, Moza Ally mabasi 20 yalizuiwa Iringa, Makambako na Mtera, wakitokea mikoa mbalimbali.

subscribe to our newsletter!

Jumapili ya Agosti 11,2024, inaingia kwenye kumbukumbu kama ya moja ya siku ambayo wanachama wengi wa CHADEMA kutoka maeneo tofauti wamekamatwa kwa wakati mmoja.

Kamata kamata ya wanachama hao na viongozi hao wa CHADEMA waliokua wakielekea kwenye shughuli ya kuadhimisha siku ya vijana ilianza mnamo Agosti 10,2024, ambapo vijana takribani 20 wa BAVICHA Temeke waliokuwa wakijiandaa kuelekea Mbeya walikamatwa.

Agosti 11,2024, wanachama zaidi walikamatwa kwa kuzuiwa kwenye makutano mbalimbali ya barabara, ambapo kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA, Moza Ally mabasi 20 yalizuiwa Iringa, Makambako na Mtera, wakitokea mikoa mbalimbali.

Maeneo ya  Iringa Kilolo wanachama wengi walionekana wakikamatwa huku taarifa za CHADEMA zikionesha takribani wanachama 109 waliwekwa kizuizini na Polisi.

Katika hali hiyo ya sintofahamu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu pamoja na Katibu wa CHADEMA John Mnyika na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Jospeh Mbilinyi na viongozi wa BAVICHA walikutanika jioni katika ofisi ya Kanda ya Nyasa kujadili sintofahamu hiyo. Baadae walifanya kikao na polisi, hata hivyo waliishia nao kukamatwa.

Polisi wamepiga marufuku maadhimisho ya sherehe ya siku ya vijana yaliyopangwa kufanywa kesho Agosti 12,2024, huku wakieleza kauli za viongozi wa BAVICHA zinaashiria uvunjifu wa amani.

Kwa upande wa CCM, umoja wa vijana wa Chama hicho uliweza kuadhimisha sherehe hizo za vijana mnamo jana Agosti 10,2024, katika Viwanja vya Aman Zanzibar ambapo mamia waliweza kusafiri na kujumuika na wenzao katika kufurahia.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *