The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Lusako Akisalimika, Nondo Akilazwa Hospitali: Maofisa TRA Wafananishwa Na ‘Watekaji Wa Landcruiser Nyeupe’

Hali ya watekaji kupendelea kutumia Landcruiser nyeupe ni hali inayojirudia rudia katika matukio mbalimbali.

subscribe to our newsletter!

Hali ya Watanzania kuishi kwa wasiwasi kama vifaranga vinavyosubiri dakika na sekunde za kutwaliwa na Mwewe(Watekaji) imeendelea kushika kasi ambapo kwa siku ya jana Disemba 05,2024, maofisa wa Mamlaka ya Mapato waliodhaniwa kuwa ni watekaji na hivyo baadhi ya Watanzania kuwashambulia kwa mawe na namna zingine.

Ni katika siku hiyo hiyo, Mwanasheria wa Haki za Binadamu, Alphonce Lusako alionekana akikimbizwa katika viunga vya ofisi yake na watu waliokuja kutambulishwa kuwa ni Polisi.

Majira ya saa nne Lusako alituma jumbe za sauti zenye wasiwasi kana kwamba ni mtu aliyekuwa akiangalia maisha yake yakipotezwa mbele yake.

“Jamani natekwa, kuna watu wamekuja ofisini, wanasema wao ni maafande, natekwa, natekwa, natekwa jamani nisaidieni,” alisikika akiongea Lusako katika hali ya wasiwasi mkubwa.

Polisi baadae walikuja kutoa taarifa ya kufafanua na kueleza kuwa walikua wakimtafuta mtu mwingine katika ofisi za Lusako aliyejulikana kwa jina la Emmanuel Mweta. Wengi wamebaki na mshangao wa sababu ya Lusako kukimbizwa ndani ya ofisi yake , lakini pia kuchukuliwa kwa gari yake kumezidisha maswali mengi miongoni mwa watu wengi.

Usiku wa jana uliendelea kuwa wenye matukio hasa baada ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato kufananishwa na watekaji na ushambuliwa maeneo ya Tegeta kwa Ndevu.

Watumishi hao watatu walikuwa katika gari aina ya Landcruiser yenye usajili STL 9923, ambapo kwa mujibu wa TRA, watumishi hao walikua wakilifuatilia gari yenye namba za usajili T229 DHZ aina ya BMW X6, inayodaiwa kuingizwa nchi bila kulipiwa kodi.

“Wakati watumishi wa TRA wanatimiza wajibu wao, walihusishwa na kitendo cha utekaji, kilichopelekea wao na gari kushambuliwa,” TRA wanaeleza katika taarifa yao.

Serikali kupitia Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba imelaani vikali kitendo cha watumishi wa TRA kushambuliwa baada ya wao kuhusishwa na watekaji.

“Wizara ya Fedha inalaani vikali tukio hili na kuahidi kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika wa uhalifu huu. Aidha, TRA itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na kwa mujibu wa sheria,” ameeleza Waziri Nchemba katika taarifa yake aliyoitoa katika mtandao wa X.

Landcruiser Nyeupe

Tukio hili linakuja ikiwa ni siku tano toka Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo, Abdul Nondo, kutekwa mnamo Disemba 01, 2024, na watu takribani sita waliokuwa na pingu.

 Watu hao walimchukua Nondo katika eneo lenye mzunguko mkubwa wa watu la Stendi ya Magufuli, na kumuweka katika gari lao, Landcruiser nyeupe na kutokomea naye. Baada ya kukaa naye kwa saa 18, walimtelekeza maeneo ya Coco Beach, huku wakiwa wamemuumiza vikali. Mpaka sasa Polisi wanaendelea kuchunguza, taarifa kutoka ACT Wazalendo zinaeleza kuwa Nondo amekutwa na kiwango kikubwa cha sumu mwilini.

Hali ya watekaji kupendelea kutumia Landcruiser nyeupe ni hali inayojirudia rudia katika matukio mbalimbali. Mfano, tukio la utekaji likihusisha Landcruiser nyeupe lilimfika pia Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake CHADEMA, Aisha Machano ambaye aliyetekwa mnamo Oktoba 20,2024, huku watekaji wake wakimvua nguo na kumpiga vikali.

Machano anaeleza kuwa watekaji walimteka maeneo ya Kibiti wakiwa na gari aina ya Landcruiser nyeupe.

“Wakati nasubiri pikipiki likaja Landcruiser jeupe, namba sikuzikariri vizuri lakini ni PT,likasimama wakaja wakaka, kwa harakahara niliwaona sita,”anaeleza Machano. 

“Mmoja wao akaja akanigusa bega akaniambia uko chini ya ulinzi, sisi ni Polisi, nikapanda ndani ya gari. Nilipoingia tu ndani ya gari, yule mwanamke ndiye aliyenifunga pingu,askari mwingine mwanaume alikuja na kitambara akanifunga,” anaeleza Machano.

Mashuhuda walioshuhudia namna wauaji wa Marehemu Ali Kibao walivyomteka kutoka katika basi alilokuwemo, waliwaeleza viongozi wa CHADEMA kuwa watekaji walilisimamisha basi alilokuwa akisafiria Kibao wakitumia Landcruiser jeupe.

Kijana wa miaka 24, Shadrack Chaula, aliyeshitakiwa baada ya kuchoma picha ya Rais, naye alitekwa na watu waliokuwa katika Landcruiser nyeupe mnamo Agosti 02,2024, mpaka hivi leo hajapatikana.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts