Akizungumza na vyombo vya habari mnamo Februari 6,2025, Katibu Mkuu UN, António Guterres, ametoa rai juu ya mkutano unaoanza Tanzania leo Februari 07, 2025,ukihusisha viongozi wa SADC na Jumuiya ya Afrika Mashariki uje na suluhu kuhusu hali ya mashaka inayoendelea DR Congo.
“Kesho [Februari 07,2025] viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC watashiriki katika kikao Tanzania. Mazungumzo haya yatalenga kutatua mgogoro unaosababishwa na mashambulio ya M23 wanaosaidiwa na jeshi la Rwanda,” alieleza António Guterres
“Mkutano wa Tanzania ukianza, ujumbe wangu ni huu: zinyamazisheni bunduki, acheni kukuza migogoro, heshimuni mipaka na uhuru wa DR Congo,” aliendelea.
Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa toka Januari 2024, takribani wanajeshi wa Rwanda 4,000 waliingia DR Congo kuwasaidia M23 moja kwa moja. Ripoti hiyo pia inaonesha baada ya waasi wa M23 kuushika mji wa Bukaya wenye madini adimu ya Coltan, madini hayo yamekuwa yakitoroshwa kupitia Rwanda kwa wingi kupitia malori.