The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Polisi Yawasaka Wadukuzi Waliochapisha Maudhui Yasiyofaa Katika Kurasa Zao Mtandaoni. Kurasa za Taasisi Zingine Binafsi na Umma Zakumbwa Pia

Katika taarifa yake Polisi imeeleza kuwa inaendelea kuwafuatilia wahalifu waliotengeneza na kusambaza taarifa hizo.

subscribe to our newsletter!

Jeshi la Polisi Tanzania limetoa taarifa kuwa inawatafuta wahusika waliochapisha maudhui yasiyofaa katika ukurasa wake wa X (zamani Twita). Maudhui hayo yalianza kuonekana kuanzia asubuhi ya Mei 20, 2025, kwanza ikiwa ni maudhui ya ngono lakini pia na ujumbe za taarifa za uongo za kufariki kwa kiongozi. Wadukuzi hao pia walihamia kwenye ukurasa wa polisi wa Youtube, maarufu kama Usalama TV na kuchapisha jumbe hizo.

Baadhi ya taasisi zingine ambao kurasa zao zimeathirika ni pamoja na ukurasa wa Tanzania Investment Centre katika mtandao wa X, ukurasa wa timu ya Simba wa Youtube, ukurasa wa Mamlaka ya mapato (TRA Online TV) wa Youtube, na ukurasa wa kampuni ya Airtel kwenye mtandao wa X na Youtube, pamoja na ukurasa wa Chama cha Mapinduzi Youtube na UN Tourism wa Youtube, na ukurasa wa Youtube wa University of Dar es Salaam.

Katika taarifa yake Polisi imeeleza kuwa inaendelea kuwafuatilia wahalifu waliotengeneza na kusambaza taarifa hizo.

“Tunawaomba wananchi wazipuuze taarifa hizo na kuepuka kuendelea kuzisambaza endapo zitakufikia. Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote yule aliyehusika na utengenezaji na utoaji wa taarifa hizo na yeyote yule ambaye ataendelea kuzisambaza,” imeeleza taarifa hiyo.

Msemaji wa Serikali ametoa taarifa ya kuwataadharisha wananchi juu ya uwepo wa taarifa za upotoshaji katika mitandao ya kijamii.

“Wananchi wote mnatahadharishwa kuwa Serikali imebaini uwepo wa taarifa za upotoshaji kupitia mitandao ya kijamii kwa kuchapisha maudhui yenye lengo la kuzua taharuki na kuwajaza hofu wananchi,” imeeleza taarifa hiyo ya Msemaji.

“Aidha, imebainika kuwa kuna wahalifu ambao wanafungua akaunti za mitandao ya kijamii yenye majina yanayofanana na taasisi zinazoaminika na kuchapisha maudhui ya upotoshaji na zenye kuzua taharuki,” ilisisitiza zaidi taarifa hiyo.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa taarifa ya kuutarifu umma kuwa ukurasa wake wa Youtube ulidukuliwa.

Katika taarifa yake TRA imeeleza: “Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kutokana na maudhui ya udukuzi huo kwani taarifa hizo sio za kweli zinalenga kupotosha umma.”

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×