Mkeka mpya wa wateule wapya wa Rais katika nafasi za wakuu wa wa mkoa, wilaya na wakurugenzi umetoka rasmi Juni 23, 2025, hii ikimaanisha baadhi ya wateule walioonesha nia ya kwenda majimboni kugombea kupitia Chama cha Mapinduzi wanaingia rasmi kwenye mchuano wa kura za maoni.
Wateule hao walitakiwa kuandika rasmi kuonesha nia zao za kuingia kwenye uchaguzi ujao. Uchaguzi huu unatarajiwa kuwa wa kipekee katika historia ya Tanzania baada ya chama kikuu cha upinzani nchini, CHADEMA, kutangazwa kuzuiwa rasmi kushiriki katika uchaguzi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi mnamo Aprili 12, 2025.
Mnamo Machi 11, 2025, katika mkutano wa 39 wa Jumuiya za Serikali za Mtaa (ALAT), Rais Samia alitoa wito kwa wale walioshika nafasi mbalimbali za serikali na wana nia ya kugombea watoe taaarifa rasmi serikalini.
“Nilimuambia Katibu Mkuu kiongozi peleka waraka rasmi Serikali za Mitaa. Yeyote mwenye nia ya kugombea atuambie mapema ili tumpandishe wa chini yake ashike ile nafasi. Hatutaki pale tayari fomu zinatoka watu wote wanakimbia kwenda kuchukua fomu mnatuacha Serikali za Mitaa hazina viongozi, hazina wasimamizi. Mnabakia kujaza watu ambao hawana uzoefu. Lakini tukijua mapema tutatayarisha watu wa kujaza hizo nafasi,” alieleza Rais Samia.
“Sasa usipojisema mapema, ukija ukichukua fomu mbele umekosa yote. Umekosa fomu, umekosa cheo, nafasi yako utaiacha. Ukituambia mapema, ukituambia mapema, umekwenda kujaribu, umeshindwa na wewe ni mzuri tutakufikiria kurudi,” alisisitiza zaidi Rais Samia.
Baadhi ya mabadiliko yaliyofanyika ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenan Leban Kihongosi, kuhamishiwa Arusha kurithi mikoba ya Paul Makonda. Tetesi mbalimbali zinaonesha Makonda anatarajiwa kuingia kwenye kura za maoni Arusha. Mpaka sasa amekuwa na mvutano mkali na Mbunge wa sasa wa Arusha, Mrisho Gambo. Anamringi Macha amehamishwa kutoka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kwa sasa atahamia rasmi Simiyu kama Mkuu wa Mkoa mpya.
Wengine walioteuliwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu, Balozi Simon Sirro ambaye amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma akichukua nafasi ya Thobias Andengenye. Kheri James, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Iringa amepandishwa na kuwa Mkuu wa Mkoa Iringa akichukua nafasi ya Peter Serukamba, aliyetangaza mapema mwezi wa tano nia yake ya kugombea Ubunge.
Mboni Mohamed Mhita aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Kahama ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Beno Malisa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Mbeya pia ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akichukua nafasi aliyokuwa ameishika Juma Zuberi Homera, ambaye katika ukurasa wake wa Instagram, ameonesha kuwa anaenda kugombea Ubunge; “Tayari ule Muda umefika, tukutane site 2025,” anaandika Homera.
Jabiri Omari Makame ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Daniel Godfre Chongolo. Katika ukurasa wake wa Instagram Chongolo ameeleza kuwa anarudi Njombe: “Kijiti nakikabidhi kwa mdogo wangu mkubwa Jabir makame…narudi nyumbani Njombe,” ameeleza Chongolo.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Reli, Masanja Kadogosa naye ameondolewa kwenye nafasi aliyokuwa anaishikilia na Injinia Machibya Masanja kuteuliwa, Machibya alikua ni Mkurugenzi wa miundombinu katika Shirika la Reli. Kadogosa amekuwa akitajwa tajwa Bariadi, na hata katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Emmanuel Nchimbi mnamo Juni 15, 2025, Kadogosa alisimamishwa pamoja na Mbunge wa sasa, Kundo Andrea Mathew na Mbunge wa Viti Maalum Lucy Sabu, ambapo Katibu wa chama hicho alisisitiza kuwa chama hicho kinawahitaji wote, akiongelea kuhusu suala la uchaguzi ndani ya chama hicho.
Mabadiliko haya yanakuja katika siku hiyo hiyo ambayo CCM imetangaza kusitisha ziara, mikutano, semina na makongamano, yanayohusisha wajumbe wa vikao vinavyopigia kura za maoni hadi baada ya kura za maoni, ikionekana ni jitihada za kuzuia ushawishi usio halali kwa wajumbe, Katikati ya joto kali la mchakato wa kura za maoni.
Wengine walioteuliwa jana Juni 23, 2025, ni pamoja na:
- Bi. Agnes Meena ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
- Bw. Rashid Kassim Mchata amehamishwa kutoka Mkoa wa Pwani kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga
- Bi. Pili Hassan Mnyema amehamishwa kutoka Mkoa wa Tanga kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani.
- Bw. Abdul Rajab Mhinte ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam
- Dr. Frank Hawasi ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.\
- Dr. Hussein Mohamed Omar amehamishwa kutoka Wizara ya Kilimo kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
- Prof. Peter Lawrence Makenga Msoffe ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya mazingira
- Mhandisi Athumani Juma Kilundumya ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo anayeshughulikia masuala ya maendeleo ya mazao na usalama wa chakula
- Solomon Jonas Itunda amehamishwa kutoka Wilaya ya Songwe kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya
- Japhari Kubecha Mghamba amehamishwa kutoka Wilaya ya Handeni kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo
- Amir Mohamed Mkalipa amehamishwa kutoka Wilaya ya Arumeru kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya llemela
- Estomin Mwatuyobe Kyando ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo
- Ayubu Yasin Sebabile ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza
- Thecla Mkuchika ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Butiama
- Angelina Marco Lubela ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti
- Maulid Hassan Dotto ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero
- Rukia Ally Zuberi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga
- Mwinyi Ahmed Mwinyi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru
- Jubilete Win Lauwo ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu
- Mikaya Tumaini Dalmia ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni
- Thomas Mendraid Myinga ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Sikonge
- Gloriana Julius Kimath ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli
- Upendo Bert Wella ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora
- Denis Gervas Masanja ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru
- Fadhil Emanuel Nkurlu ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songwe
- Benjamin Samwel Sitta ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa
- Salum Nyamwese ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni
- Frank John Mkinda ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama
- Mwanamwaya Kombo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkinga
- Kassim Salum Kirondomara ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Biharamulo
- Thobias Abwaro ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Babati
- Asycritus Mumena Egaruk ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Meatu
- Nyakaji Etanga Mashauri ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilolo
- Mustapha Ayubu Kimomwe ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji
- Milama Masiko ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Serengeti
- Mpampalika Mfaume Mpampalika ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Mwanga
- Richard Jackson Mwalingo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mtwara
- Zuberi Said Zuberi ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Magu
- Angela Henry Mono ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Tanga
- Mamndolwa Miraj Gembe ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Same
- Sabina Starlin Mwajeka ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Momba
- Sosthenes Chakupanyuka ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kaliua
- Adestino Gwelino Mwilinge ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbogwe
- Justice Laurent Kijazi amehamishwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya
- Zaina Mfaume Mlawa amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
- Raymond Mweli ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali
- Adelina Enock Mfikwa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
- Iddi Ally Ndabona ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi
- Hamisi Hamidu Idd ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega
- Mwarami Seif ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
- Bi. Newaho Mkisi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
- Zainab Salum Mgomi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Nanyamba
- John Marco Pima ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
- Albina Willium Mtumbuka ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
- Paulo Francis Faty ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero
- Shabani Kabelwa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
- Vicent Augustino Mbua ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe.