The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

IMF Yaidhinisha Mkopo wa Trilioni 1.2 kwa Tanzania, Yaridhishwa na Hali ya Uchumi

Kwa fedha hizi kunaifanya Tanzania kukamilisha jumla ya shilingi bilioni 872.7 sawa na dola milioni 345.4 kupitia programu ya RSF baada ya mapitio ya pili, na jumla ya shilingi trilioni 2.4 sawa na dola milioni 908.3 kupitia programu ya ECF baada ya mapitio ya tano.

subscribe to our newsletter!

Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF) kuipatia Tanzania kiasi cha shilingi trilioni 1.2 ambayo ni sawa na dola za kimarekani milioni 448.4 punde baada ya Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo kuidhinisha kiasi hiko kupitia kikao chake kilichohitimishwa Juni 27, 2025.

Fedha hizi ni pamoja na shilingi bilioni 405.1 sawa na dola milioni 155.7 kwa ajili ya program za Extended Credit Facility(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii pamoja.

Kiasi kilichobaki cha shilingi shilingi bilioni 761.6 sawa dola 292.7 ni kwa ajili ya Programu ya Resilient and Sustainable Fund (RSF) inayotekelezwa kwa lengo la kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kwa fedha hizi kunaifanya Tanzania kukamilisha jumla ya shilingi bilioni 872.7 sawa na dola milioni 345.4 kupitia programu ya RSF baada ya mapitio ya pili, na jumla ya shilingi trilioni 2.4 sawa na dola milioni 908.3 kupitia programu ya ECF baada ya mapitio ya tano.

Kupitia taarifa yake , IMF wameeleza kuridhishwa na hali ya uchumi wa Tanzania hata katika eneo la ukuaji na utulivu ambapo ukuaji wa uchumi umeelezwa kukua kwa asilimia 5.5 katika mwaka 2024 na unakadiriwa kufikia asilimia 6 mwishoni mwa mwaka 2025.

Programu ya ECF ambayo inatarajia kukamilika mwishoni mwa mwaka wa fedha wa 2025/26 baada ya kuongezewa miezi 6 hapo Juni 2024, utekelezaji wake ulianza mwaka 2022 ambapo Tanzania iliidhinishiwa kuweza kupata mkopo mpaka kiasi cha shilingi trilioni 2.7 sawa na dola milioni 1,046.4.

Mkopo huu wa ECF hutolewa kwa nchi zinazoendelea na zenye changamoto ya urari wa biashara na malipo ya nje (Balance Of Payment).

IMF wameeleza kuwa mageuzi ya kiuchumi ambayo Tanzania imeendelea kuyafanya chini ya programu ya ECF yapo ndani ya malengo program licha ya changamoto ndogondogo zilizojitokeza.

Wameridhishwa na hali ya utulivu wa mfumuko wa bei ambao ulikuwa asilimia 3.2, Aprili 2025 kiwango ambacho kilikuwa chini ya matazamio ya Benki Kuu ya Tanzania.

Wamehimiza Tanzania kuendelea kuimarisha mfumo mpya wa kusimamia sera ya fedha wa riba ambao unatumika hivi sasa na Benki Kuu ya Tanzania ili kudhibiti mfumuko wa bei nchini.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×
×