The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Kesi ya Kufungwa Kanisa la Ufufuo na Uzima Yaahirishwa Hadi Julai 14, 2025. Shauri la Kikatiba Kusikilizwa Mchana

Akiongea kwa njia ya simu wakili Kibatala amesema hiyo imetokana na mwingiliano wa shughuli mbalimbali za kimahakama.

subscribe to our newsletter!

Dodoma. Shauri lilofunguliwa na Bodi ya Wadhamini la kanisa la Glory of Christ Tanzania Church maarufu kwa jina la kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima limeahirishwa kusikilizwa leo Julai 11, 2025 mpaka tena Julai 14, 2025.

Bodi ya Wadhamini inaiomba Mahakama kutupilia mbali zuio la kanisa hilo kuendesha shughuli zake za kidini. Toka shauri hilo lilivyofikishwa Mahakamani mbele ya Jaji Juliana Masabo kikwazo kikubwa kilichojitokeza ni barua husika ya kufuta usajili.

Ambapo barua iliyowasilishwa Mahakamani kutoka kwa msajili ilikuwa na jina la Glory of Christ Church badala ya jina Glory of Christ Tanzania Church, jambo ambalo hata mawakili wa serikali waliita barua hiyo uzushi na haipo.

Hata hivyo Wakili wa Kanisa hilo, Wakili Peter Kibatala aliweza kuwasilisha vielelezo vipya, na shauri hilo kupangiwa kusikilizwa leo. Hata hivyo shauri limeahirishwa mpaka siku ya Jumatatu Julai 14, 2025, saa nane kamili mchana.

Akiongea kwa njia ya simu wakili Kibatala amesema hiyo imetokana na mwingiliano wa shughuli mbalimbali za kimahakama. “Maana imeonekana ni busara iahirishwe mpaka Jumatatu ambapo mambo mengine yataendelea kuhusiana na shauri hilo,” amesema Kibatala.

Ikumbukuwe pia, kesi hiyo ilipaswa kusikilizwa Julai 8, 2025 na haikusikilizwa, huku wakili Kibatala akisema utaratibu huo ni wa kawaida.

“Kwa hiyo kama nilivyosema tulipata taarifa na tukawafahamisha wateja wetu na sisi wenyewe tukachukua hatua za ziada. Kwa hiyo tutaendelea tena hiyo tarehe 14 mwezi wa saba kama nilivyosema,” aliongeza Kibatala.

Katika hatua nyingine waumini 52 wa Kanisa la Ufufuo na Uzima wamefungua kesi ya Kikatiba juu ya kudai uhuru wa kuabudu, kesi hiyo itasikilizwa katika Mahakama Kuu, Dar es Salaam, leo mchana.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×
×