The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Tuwaunge Mkono Watu Wenye Ulemavu Waliojitokeza Kugombea Nafasi za Kisiasa

Uongozi bora haupaswi kuangalia hali ya mtu bali uwezo, maono na dhamira ya kweli ya kuwatumikia wananchi.

subscribe to our newsletter!

“2015 Tanzania ilipata wagombea wengi wenye ulemavu, lakini 2025 imeonesha namna watu wenye ulemavu wameamka kwa kiwango cha juu zaidi, wakijitokeza kwa ujasiri na ari kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa.”

Maneno haya yanadhihirisha hali halisi ya mwelekeo wa sasa nchini. Kadri Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 unavyokaribia, kuna ongezeko kubwa la watu wenye ulemavu waliotangaza nia ya kushiriki moja kwa moja kwenye mchakato wa uchaguzi kama wagombea wa nafasi za udiwani, ubunge, na viti maalum. Hili ni jambo la kihistoria linaloashiria kuongezeka kwa uelewa, ujasiri na hamasa ya watu wenye ulemavu kushiriki katika uongozi wa taifa.

Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), asilimia 95 ya watu wenye ulemavu waliotangaza nia hadi sasa wanatoka ndani ya chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM), jambo linaloonesha namna vyama vya siasa vinavyoanza kutambua uwezo na mchango wa kundi hili muhimu katika ujenzi wa taifa.

Katika kipindi cha miezi michache iliyopita, watu wenye ulemavu kutoka mikoa mbalimbali wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kushiriki kwenye midahalo, mafunzo ya uongozi, na shughuli za maandalizi ya kisiasa. Hii ni ishara tosha kwamba uongozi jumuishi siyo tu ndoto tena—ni mchakato unaoendelea kujengwa kwa vitendo.

SHIVYAWATA, kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ya watu wenye ulemavu, imeendelea kutoa elimu ya uraia na kuwawezesha watia nia kuelewa mfumo wa uchaguzi, haki zao za kisiasa, na mbinu za kuendesha kampeni kwa njia jumuishi. Aidha, juhudi zinafanyika kushawishi wadau wa kisiasa kuhakikisha kuwa taratibu na mazingira ya uchaguzi yanakuwa rafiki kwa watu wa makundi yote.

SOMA ZAIDI: Tunawezaje Kujenga Jamii Yenye Mtazamo Chanya Kwa Wanawake wa Makundi Maalumu? 

Mwakilishi wa SHIVYAWATA alisema: “Tunafarijika kuona idadi hii kubwa ya watu wenye ulemavu wakijitokeza kwa ajili ya uongozi. Ni ushahidi kuwa jamii inabadilika na kuwa tayari kwa viongozi wenye mitazamo mipya, inayojumuisha kila Mtanzania bila ubaguzi.”

Changamoto

Pamoja na mafanikio haya, changamoto kama ukosefu wa rasilimali za kampeni, mitazamo hasi kutoka kwa jamii, na miundombinu isiyokuwa rafiki bado zipo. Hata hivyo, muamko huu mkubwa umeleta matumaini mapya ya mabadiliko chanya na kuweka msingi wa Tanzania jumuishi zaidi.

SHIVYAWATA inatoa wito kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, vyama vya siasa, Serikali, na mashirika ya kiraia kuendelea kuunga mkono jitihada za kuwawezesha watu wenye ulemavu kushiriki kikamilifu kwenye mchakato wa uchaguzi. 

Uongozi bora haupaswi kuangalia hali ya mtu bali uwezo, maono na dhamira ya kweli ya kuwatumikia wananchi. Makundi yaliyojitokeza ni pamoja na wasioona, watu wenye ualbino, watu wenye ulemavu wa viungo na viziwi.

Kufahamu idadi kamili ya watu wenye ulemavu waliojitokeza kuwania nafasi za kisiasa kwenye kura za maoni za vyama mbalimbali, ingia hapa.

Janeth Lugome ni afisa mawasiliano kutoka SHIVYAWATA. Kwa mrejesho, anapatikana kupitia janetlugome@gmail.com. Haya ni maoni binafsi ya mwandishi na si lazima yaakisi mtazamo wa The Chanzo. Ungependa kuchapisha kwenye safu hii? Wasiliana na wahariri wetu kupitia editor@thechanzo.com kwa ufafanuzi zaidi.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×
×