The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Mahakama Yatupilia Mbali Maombi ya Kupinga Kanuni za Maadili ya Uchaguzi Yasema Wananchi waliopeleka Maombi Hawahusiki ni Majirani tu Katika Mchakato

Katika maamuzi yake Mahakama ilieleza kuwa waleta maombi hawajaweza kuishawishi Mahakama kuwa wana msalahi ya kutosha katika kanuni hizo, Mahakama ikieleza kuwa waleta maombi ni majirani tu na sio wenye haki ya kushitaki dhidi ya kanuni.

subscribe to our newsletter!

Mahakama Kuu chini ya Jaji Abdi Shaaban Kagomba imetupilia mbali maombi ya kuzuia matumizi ya Kanuni za Maadili ya Uchaguzi za Mwaka 2025. Katika maamuzi yaliyotolewa mnamo Julai 11, 2025, Mahakama imeeleza kuwa wahusika wanaoweza kuzilalamikia kanuni hizo ni vyama vya siasa, wagombea, serikali, na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mahakama imesisitiza wananchi waliopeleka shauri hilo sio wahusika bali ni majirani tu katika mchakato.

Shauri hilo lilifikishwa Mahakamani na wananchi wawili, Kumbusho Kagine na  Bubelwa Kaiza ambao waliiomba Mahakama kusitisha kwa muda matumizi ya kanuni hizo mpaka zitakapopitiwa upya na Mahakama.

Wananchi hao wawili waliwakilishwa na mawakili wawili; Mpale Mpoki na Jebra Kambole. Waleta maombi hao walitoa sababu sita za kuthibitisha namna kanuni hizo zinavyowagusa . Kwanza waleta maombi walieleza kuwa maneno ya utangulizi katika Kanuni yametaja maneno washiriki wa uchaguzi, ambapo walieleza hii inamaanisha ni umma kwa ujumla. Pili walieleza wao ni wananchi wenye umri wa kupiga kura na wamejiandikisha kupiga kura; hivyo wana haki ya kupiga kura na kuchaguliwa. Tatu, walieleza kwamba kwa kuwa wana haki ya kupiga kura na kuchagua, wanaweza kugombea katika nafasi mbalimbali za uchaguzi.

Nne, waleta maombi wameieleza Mahakama kuwa wana maslahi ya kuona uchaguzi ulio huru na wa haki. Tano wakasisitiza kuwa wana maslahi katika kanuni hizo kama wapiga kura wanaotaka kuwapigia kura watu wanaowataka. Mwisho wakaeleza kuwa Kanuni zinaweka haki na wajibu wa wagombea, vyama vya siasa na wafuasi wao, ambao sio lazi wawe wanachama, hivyo suala hilo linakua wajibu wa kiraia Kama Ibara ya 26(1) ya Katiba inavyoeleza.

Katika shauri hilo Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliwakilishwa na Wakili Mkuu wa Serikali  Mark Mulwambo, Erigh Rumisha, na Edwin Webiro. Katika majibu yao wajibu maombi walieleza kuwa waleta maombi sio wahusika kama ambavyo Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024 inavyoeleza, ambapo walisisitiza wadau wa kanuni hizo ni serikali, wagombea, vyama vya siasa, na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

SOMA: Wataalamu wa Sheria Watofautiana na Tume Juu ya Hoja Kuwa Kwa Kutokusaini Kanuni za Maadili Aprili 12, 2025, Kunazuia Ushiriki wa CHADEMA Katika Uchaguzi

Wajibu maombi pia walieleza juu ya tofauti inayooneka katika majina ya waleta maombi ambapo walieleza katika kitambulisho cha kura cha Kumbusho Kagine jina linaonekana ni Kumbusho D. Kagine, pia wakaeleza jina la Bubelwa Kaiza linaonekane kama Bubelwa E. Kaiza katika kitambulisho chake cha wapiga kura. Utofauti huu wa majina walieleza pia ni sababu, ya waleta maombi kutokua na maslahi katika kanuni hizo, hasa kwa kuangalia kipengele cha wao kuwa wapiga kura.

Pia wakaieleza Mahakama kuwa, kusitisha matumizi ya Kanuni za Uchaguzi itafanya wadau kufanya mchakato bila muongozo. Wakasisitiza zaidi kuwa maaumuzi kama hayo yakikubaliwa yataathiri zaidi umma kuliko waleta maombi kwa sababu tayari rasilimali na maandalizi yameshafanyika kwa ajili ya uchaguzi.

Katika maamuzi yake Mahakama ilieleza kuwa waleta maombi hawajaweza kuishawishi Mahakama kuwa wana msalahi ya kutosha katika kanuni hizo, Mahakama ikieleza kuwa waleta maombi ni majirani tu na sio wenye haki ya kushitaki dhidi ya kanuni.

“Chini ya kifungu (1), Sheria inaeleza kuwa kanuni zitaongoza masuala ya maadili ya vyama vya siasa, serikali na mjibu maombi wa kwanza (Tume ya Taifa ya Uchaguzi) wakati wa kampeni na uchaguzi,” uamuzi wa Mahakama unaeleza.

“Ingawa sioni kwamba sababu zilizotolewa na waombaji kuwa hazina mashiko na naamini kuwa ni hoja nzito na zinazoweza kujadiliwa, kupitia kiapo chao, Waombaji hawajaweza, kuihakikishia Mahakama hii kuhusu namna walivyo na maslahi [katika kanuni]. Kwa uchache kabisa, mtu atajiuliza wako wapi wadau walioathirika ambao maslahi yao katika suala hili yangeweza, bila shaka, kutambuliwa,” Mahakama iliendelea kusema.

“Bila ya wao kuwepo mbele ya Mahakama, yaliyoelezwa na waombaji katika hoja za 6.1, 6.2, 6.3, 6.4 na 6.5 za tamko hilo yanakuwa batili kwa kuzingatia ukweli kwamba waombaji ni majirani tu, na si wenye haki ya kufungua kesi, kwa mujibu wa sheria inayohusu jambo hili,” Mahakama ilisisitiza zaidi.

Mahakama pia ilieleza kuwa hoja za watoa maombi kuwa na maslahi ya kuona uchaguzi huru na wa haki ni hoja za mbali zisizoonesha uhusika wa waombaji katika madai yao juu ya kanuni husika.

Akiongea na Haki TV, Wakili wa waleta maombi, Jebra Kambole, ameeleza kuwa hawajakubaliana na maamuzi hayo ya Mahakama na wanategemea kurudi Mahakamani.Kambole anaeleza walienda Mahakamani hapo kwa sababu ya changamoto katika kanuni hizo, ambazo anaeleza zinaondoa nguvu ya wapiga kura na kushusha thamani ya kura.

Baadhi ya mambo aliyoyataja ni pamoja na msimamo wa Tume ya Uchaguzi kuwa vyama ambavyo havikusaini kanuni hizo mnamo Aprili 12, 2025, havitaruhusiwa kushiriki uchaguzi mpaka 2030. Kambole anahoji kama ikitokea vyama vipya vikaundwa hoja hiyo itakuwajea. Kambole pia anaeleza kuwa kanuni hizo zinapaswa kuwa katika utendaji baada ya uteuzi wa wagombea, lakini pia Kambole anakosoa Kanuni hizo kusainiwa kabla ya kuchapishwa kwenye gazeti la serikali, akisisitiza kilichosainiwa hakikua na hadhi ya sheria.

“Hatujaridhika kwa sababu tunaamini uchaguzi ni wa watu, hakuna uchaguzi bila watu. Hamna mmiliki wa uchaguzi, Mahakama wamesema kwenye hizi kanuni za maadili hawa [waleta maombi] wanaonekana ni majirani, tunaona msingi huo haukua sawa, kwenye uchaguzi hakuna mtu ambaye ni majirani, labda watu wa nje, mtu ambaye anapiga kura hawezi kuwa jirani kwenye mchakato wa uchaguzi,” anaeleza Wakili Kambole.

Na kuongeza: “Kwa hiyo pamoja na kwamba Mahakama imetoa maamuzi, tunayaheshimu lakini tunayachukulia hatua. Kwanza tutayakatia rufaa haya maamuzi, lakini kwa sababu Mahakama inafikiri ikipelekewa vyama ndiyo itafanya hivyo. Tupo kwenye mchakato kuhakikisha  kuangalia kama kuna vyama ambavyo viko tayari kuchukua hatua za kisheria vije sisi tuwape msaada.”

Kanuni za Maadili ya Uchaguzi  ni kati ya masuala yaliyoibua utata katika mchakato wa uchaguzi huu wa mwaka 2025. Hii ni baada ya chama kikuu cha upinzani Tanzania, CHADEMA kutokusaini kanuni hizo mnamo Aprili 12, 2025, jambo ambalo Tume ya Uchaguzi imesisitiza hawataruhusiwa kushiriki uchaguzi kwa miaka mitano ijayo.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×
×