The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

TPDC na Kampuni ya Nigeria Waingia Makubaliano Kuanzisha Utafiti wa Mafuta na Gesi Mnazi Bay Mtwara

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mussa Makame amesema lengo la mkataba huo ni kuweka rasmi mwongozo wa namna ambavyo watakavyoshirikiana kwa matarajio ya kufikia kwenye uzalishaji kutoka kwenye kitalu hiko hapo baadae.

subscribe to our newsletter!

Dodoma. Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Kampuni ya First Exploration & Petrolium Development ya nchini Nigeria wameingia makubaliano ya awali Julai 18, 2025 kushirikiana kufanya utafiti wa mafuta na gesi asilia katika kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini kilichopo mkoani Mtwara.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mussa Makame amesema lengo la mkataba huo ni kuweka rasmi mwongozo wa namna ambavyo watakavyoshirikiana kwa matarajio ya kufikia kwenye uzalishaji kutoka kwenye kitalu hiko hapo baadae.

“Hiki ni kitalu ambacho Serikali imeipatia TPDC ili iweze kukiendeleza kuna kazi nyingi ambazo tumesh zifanya, lakini kuna kazi bado ambazo tunataka kuzifanya hususani hatua inayofuatia ya kuchimba au kuchoronga visima kwa ajili ya kutafuta mafuta au gesi katika eneo hilo,” amesema Makame.

Amesema kuwa mkataba huo ni wa miezi tisa na wameshakamilisha hatua ya kwanza ya kusaini makubaliano hayo. Makame ameeleza kuwa katika sekta ya mafuta na gesi ni jambo la kawaida kushirikiana na wengine kwa lengo la kupunguza hatari na gharama.

“Kwa sababu ni mradi mkubwa unatokea katika bahari ina kina kirefu kidogo kwa sasa tunaona sehemu za kuchimba zipo takriban zenye kina cha mita 800, “ amesema Makame, “Kwa hiyo ni mradi ambao una gharama kubwa.”

Kisima kimoja cha gesi kinaweza kukadiriwa kufika gharama ya dola za kimarekani milioni 60, ambayo ni sawa na takriban bilioni 150. 

Kwa upande wake Kamishna wa Petroli na Gesi kutoka Wizara ya Nishati, Goodluck Shirima amesema, makubaliano hayo ya awali yanaweka misingi ya awali namna ambavyo TPDC inaweza kushirikiana na kampuni hiyo katika kufanya utafiti wa mafuta na gesi katika kitalu hicho.

“Sisi kama Wizara ya Nishati tunawapongeza TPDC kwa jitihada hizi na kama Serikali tumekuwa tukifanya jitihada mbalimbali za kuiwezesha TPDC kuwa shirika la taifa la mafuta lenye nguvu na lenye uwezo wa kuendeleza vitalu vyetu vyenye uwezekano wa mafuta na gesi eidha wenyewe ama kwa kushirikiana na wabia,” amesema.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya First E & P Company Limited, Ademola Adeyemi-Bero amesema kupitia makubalino hayo, Tanzania ina mchango mkubwa katika kuongeza upatikanaji wa nishati, kusambaza nishati kwa mataifa jirani, na kuimarisha usalama wa nishati si tu Afrika Mashariki, bali hata Afrika Magharibi na maeneo mengine ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

“Mafanikio yetu nchini Nigeria yalijengwa juu ya utaalamu wa kina wa kiteknolojia, timu yenye utendaji wa hali ya juu, na fikra za ujasiriamali. Tunaamini kwamba Tanzania ni mahali sahihi, na TPDC ni mshirika sahihi.”

Jackline Kuwanda ni mwandishi wa habari wa The Chanzo anapatikana mkoani Dodoma. Unaweza kumpata kupitia jaquelinevictor88@gmail.com 

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×
×