The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Ratiba Ya Uchaguzi Mkuu Yatangazwa Rasmi, Oktoba 29, 2025 Itakuwa Siku Ya Kupiga Kura

Zoezi la utoaji fomu litakuwa kati ya Agosti 14, 2025 hadi Agosti 27, 2025 na Agosti 28, 2025, kipenga cha kampeni kikipulizwa.

subscribe to our newsletter!

Akitangaza ratiba hiyo Julai 26, 2025 mkoani Dodoma mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Jacobs Mwambegele amesema, Agosti 9, 2025 hadi Agosti 27, 2025 itakuwa ni zoezi la utoaji wa fomu za uteuzi wa wagombea wa kiti ya Rais na Makamu wa Rais.

Mwenyekiti huyo ameendelea kusema, Agosti 14, 2025 hadi Agosti 27, 2025 itakuwa ni utoaji wa fomu za uteuzi wa wagombea ubunge na udiwani.

“Tatu tarehe 27 Agosti, 2025  itakuwa siku ya uteuzi wa wagombea wa kiti ya Rais na Makamu wa Rais, uteuzi wa wagombea ubunge na uteuzi wa wagombea udiwani. Nne, tarehe 28 Agosti, 2025 hadi tarehe 28 Oktoba, 2025 kitakuwa kipindi cha kampeni za uchaguzi kwa Tanzania bara.”

“Tano, tarehe 28 Agost, 2025 hadi tarehe 27 Oktoba, 2025 kitakuwa kipindi cha kampeni za uchaguzi kwa Tanzania Zanzibar ili kupisha kura ya mapema. Oktoba 29, 2025 siku ya Jumatano itakuwa ndiyo siku ya kupiga kura.”

Vyama 18 vimeshiriki katika zoezi hilo kasoro Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho hakikusaini kanuni za maadili ya uchaguzi mnamo Aprili 12, 2025, jambo ambalo Tume ilieleza kuwa chama hicho kitazuiwa kushiriki uchaguzi wowote mpaka 2030.

Wakati ratiba hii ikitangazwa, Tume ilieleza kuwa jumla ya wapiga kura milioni 37,655,559 wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa mwaka 2025.

“Idadi hii ni sawa na ongezeko la asilimia 26.55 kutoka idadi ya wapiga kura 29,754,699 walio kuwa kwenye daftari mwaka 2025,” amesema Jaji Mwambegele. “Kwa upande wa Zanzibar wapiga kura 725,876 wapo katika daftari la wapiga kura. Na wapiga kura 278,751 wameandikishwa na INEC kwa kuwa hawakuwa na sifa za kuandishwa na ZEC.”

Katika idadi ya wapiga kura milioni 37,655,559 waliopo katika daftari wapiga kura milioni 36,650,932 wapo Tanzania bara. Na wapiga kura milioni 1,004,627 wapo Tanzania Zanzibar. Kati ya wapiga kura hao milioni 18,943,455 ni wanawake sawa na asilimia 50.31. Na wapiga kura milioni 18,712,104 wanaume sawa na asilimia 49.69. Na Wapiga kura 49,174 ni watu wenye ulemavu.

Kadhalika Jaji Mwambegele amesema, jumla ya vituo 99,911 vitatumika kupigia kura kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku akieleza mchanganuo wake kuwa vituo 97,349 vitatumika kwa ajili ya kupigia kura kwa Tanzania bara.

“Vituo 2,562 vitatumika kwa ajili ya kupigia kura kwa Tanzania Zanzibar,” amesema wakati akieleza mchanganuo huo. “Idadi hii ya vituo 99,911 ni sawa na ongezeko la asilimia 22.49 ya vituo vya kupigia kura 88,567 vilivyotumika katika uchaguzi mkuu mwaka 2020.”

Hata hivyo, idadi ya vituo 1,766 vilivyopo sasa kwa mujibu wa daftari la wapiga kura la Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC ni sehemu ya vituo vitakavyotumiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi INEC kwa ajili ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na wabunge kutoka Zanzibar.

Tume hiyo imekamilisha uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa awamu mbili. Ambapo awamu ya kwanza ya uboreshaji ulianza Julai 20,2024 na kukamilika Machi 25, 2025. Awamu ya pili ilianza Mosi, Mei 2025 na kukamilika Julai 4, 2025. Jumla ya wapiga kura wapya milioni 7,641,592 wameandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura, sawa na asilimia 136.79 ya makadirio ya awali.

“Jumla ya wapiga kura milioni 4,291,699 wameboresha taarifa zao na wana asilimia 98.23 ya makadirio ya awali. Wapiga kura 99,744 wameondolewa katika daftari kwa kupoteza sifa sawa na asilimia 16.78 ya makadirio ya awali. Na wapiga kura 8,703 wamebainika kujiandikisha zaidi ya mara moja.”

“Mkurugenzi wa uchaguzi atakabidhi orodha hii kwa Jeshi la Polisi ili liendelee na hatua za kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 114 cha Sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Sheria namba 1 ya mwaka 2024.”

Baada ya wito huo, Mkurugenzi wa tume hiyo Ramadhani Kailima alikabidhi orodha hiyo ya wapiga kura waliojiandikisha zaidi ya mara moja wakati wa uboreshaji wa daftari la wapiga kura mwaka 2024/2025.

“Sheria rejewa imeeleza adhabu zake kwa watakao kutwa na hatia katika orodha hii ninayo ikabidhi ina taarifa ifuatazo moja ina namba ya mpiga kura aliyejiandikisha kwenye kila kituo ambacho alijiandikisha zaidi ya mara moja. Ina majina ya wapiga kura aliyo yatumia, ina jina la mkoa, halmashauri, kata.”

“Ina tarehe na muda aliyoandikisha katika vituo hivyo. Ina namba za simu alizo jiandikisha katika vituo hivyo. Sita ina alama za vidole alizoweka kwenye kituo cha kujiandikisha cha wapiga kura. Na inapisha alizo pigwa kwenye vituo hivyo.”  

Ikumbukwe kuwa, kabla ya kuanza kwa zoezi la uboreshaji wa daftari Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilifanya makadirio ya wapiga kura watakao andikishwa kwenye daftari.

Idadi ya wapiga kura wapya, waliokadiriwa kuandikishwa ilikuwa milioni 5,586,433 ambayo ni sawa na asilimia 18.77 ya wapiga kura wote walioandikishwa katika  uboreshaji wa 2019-2020.

Idadi ya wapiga kura waliokadiriwa kuboresha taarifa zao ilikuwa ni milioni 4,369,531 ambayo ni sawa na asilimia 15 ya wapiga kura wote ya walio andikishwa 2019-2020. Pia, idadi ya wapiga kura walio kadiriwa kuondolewa kwa kupoteza sifa ilikuwa ni 594,494 sawa na asilimia 1.9 ya walioandikishwa 2019-2020.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetoa wito kwa wadau wote ikiwa ni pamoja na wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi kwa kuzingatia Sheria, kanuni, miongozo na maelekezo yatakayo tolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Jackline Kuwanda ni mwandishi wa habari wa The Chanzo. Anapatikana mkoani Dodoma, unaweza kumpata kupitia jaquelinevictor88@gmail.com

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×