The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Salum Mwalimu, Devotha Minja Kupeperusha Bendera ya CHAUMMA Urais 2025

Kati ya wajumbe 357 waliohudhuria mkutano huo waliopiga kura walikuwa 340 ambapo Mwalimu alipata kura 336 za ndio na kura 4 za hapana. Huku Devotha Minja yeye alipata kura 335 za ndio huku kura za hapana zikiwa 6.

subscribe to our newsletter!

Mkutano Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA) uliofanyika jijini Dar es Salaam Agosti 7, 2025 umemteua Katibu Mkuu wake Salum Mwalimu kuwa mgombea wa Urais wa chama hiko baada ya kupendekezwa na halmashauri kuu na Devotha Minja ambaye ni Makamu Mwenyekiti kuwa mgombea mwenza wake kwenye uchaguzi unaotarajia kufanyika Agosti 8, 2025.

Kati ya wajumbe 357 waliohudhuria mkutano huo waliopiga kura walikuwa 340 ambapo Mwalimu alipata kura 336 za ndio na kura 4 za hapana. Huku Devotha Minja yeye alipata kura 335 za ndio huku kura za hapana zikiwa 6. 

Mwalimu ambaye amezaliwa mwaka 1979 visiwani Zanzibar kujiunga na CHAUMMA mapema Mei mwaka huu kutokea CHADEMA pamoja na kundi la wanachama waandamizi lililojulikana kama G55 ambalo liliundwa na waliokuwa wafuasi wa mwenyekiti wa zamani wa CHADEMA Freeman Mbowe.

Alikuwa msaidizi wa karibu wa Mwenyekiti wa zamani wa CHADEMA Freeman Mbowe na kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi akiwa CHADEMA ikiwemo nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar tangu mwaka 2014 na Mjumbe wa Sekretarieti na Kamati Kuu ya chama hiko.

Mwaka 2015 aligombea ubunge katika uchaguzi mkuu jimbo la Kikwajuni Zanzibar lakini hakushinda, na mwaka 2018 aligombea ubunge wa jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam katika uchaguzi mdogo napo hakushinda katika uchaguzi uliogubikwa na malalamiko kutoka vyama vya upinzani. Mwaka huo 2018 tena aligombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki nako hakushinda.

SOMA ZAIDI: Yericko Nyerere: Tunakwenda CHAUMMA na ‘No Reforms, No Election’ ya Mbowe

Kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 alikuwa mgombea mwenza wa Tundu Lissu aliyegombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakipeperusha bendera ya CHADEMA, uchaguzi ambao Rais wa awamu ya tano wa Tanzania John Pombe Magufuli alitangazwa kuwa mshindi kwa kipindi cha pili.

Naye mgombea mwenza ambaye Mwalimu alimpendekeza Devotha Minja alijiunga na CHAUMMA akitokea CHADEMA na wenzake mwezi Mei, 2025 alipokuwa Mwenyekiti wa Kanda ya  Kati. Amewahi kuwa mbunge wa viti maalum wa CHADEMA kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 na alijiondoa CHADEMA kwa sababu ileile ya kutokukubaliana na uongozi mpya tofauti na upande aliokuwa akiuunga mkono wa mwenyekiti wa zamani wa CHADEMA.

Katika mkutano mkuu wa CHAUMMA uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City ilishuhudiwa pia uzinduzi wa Ilani ya uchaguzi mkuu 2025 na chama hiko kuahidi kuwa kitasimamisha wagombea maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar.

SOMA ZAIDI:  ‘CHADEMA G55’: Makovu ya Uchaguzi, Ushawishi Hafifu na Ndoto za Kujiletea Mabadiliko Binafsi Nyuma ya Kivuli cha Mbowe

Mkutano huo ulishuhudiwa na wageni mbalimbali kutoka Ofisi ya Msajili, Asasi za Kiraia na wanadiplomasia ikiwemo wa kutoka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China jambo ambalo ni la kihistoria katika siasa za vyama vingi kwani hawajawahi kutuma wawakilishi kwenye shughuli za kisiasa za vyama vya upinzani nchini. Wengine waliotuma wawakilishi ni Umoja wa Ulaya, Uingereza na Marekani.

Uteuzi wa Mwalimu kuwa mgombea wa urais kupitia CHAUMMA utapunguza minong’ono ya awali juu ya hisia za watu kuwa huenda chama hiko kikamsimamisha Freeman Mbowe kutokana na ukimya wake wa hivi karibuni huku kundi kubwa la watu waliomuunga mkono kwenye uchaguzi wa ndani wa CHADEMA alioshindwa Januari 21, 2025 pamoja na wasaidizi wake walitimkia CHAUMMA.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×