The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

TRA Yasisitiza Wafanyabiashara wa Mtandaoni Kujisajili Kulipa Kodi

Kwa mujibu wa TRA, aina za biashara zinazohitajika kujisajili ni pamoja na; Wauzaji wa bidhaa kupitia majukwaa ya mtandaoni, Wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs) wanaofanya biashara mtandaoni kupitia masoko ya kidijitali au tovuti zao na wamiliki wa mali binafsi wanaotoa huduma za upangishaji kwa njia ya mtandao.

subscribe to our newsletter!

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa wito kwa watu binafsi na taasisi zote zinazojihusisha na biashara kupitia mtandao kuhakikisha zinajisajili na kulipa kodi kabla ya tarehe 31 Agosti 2025, kwa mujibu wa sheria za kodi nchini.

Katika taarifa kwa umma iliyotolewa Agosti 11, 2025, TRA imesisitiza kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 4 cha Sheria ya Kodi ya Mapato (Sura 332) na Kifungu cha 22 cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi (Sura 438), mtu yeyote au taasisi inayopata kipato kupitia biashara, uwekezaji au ajira inapaswa kulipa kodi. Hatua hii inahusisha pia biashara zote za mtandaoni, ikiwemo mauzo ya bidhaa na huduma kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa ya kimataifa.

SOMA: Namna Serikali Inavyoweza Kutumia Leseni za Kidigitali Kuwezesha Biashara za Mtandaoni

“Tunawakumbusha wafanyabiashara wote wa mtandaoni, wakiwemo wanaouza bidhaa kupitia Instagram, Facebook, TikTok, X (zamani Twitter), Jiji na mingineyo, pamoja na watoa huduma za upangishaji kama Airbnb, kuwa ni lazima kujisajili na kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN). Hatua hii inalenga kuhakikisha uchumi wa kidijitali unachangia kikamilifu katika mapato ya taifa.” Imeleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa TRA, aina za biashara zinazohitajika kujisajili ni pamoja na; Wauzaji wa bidhaa kupitia majukwaa ya mtandaoni, Wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs) wanaofanya biashara mtandaoni kupitia masoko ya kidijitali au tovuti zao na wamiliki wa mali binafsi wanaotoa huduma za upangishaji kwa njia ya mtandao.

TRA imefafanua kuwa hata kama mfanyabiashara hana ofisi, duka au ghala, lakini anauza bidhaa au kutoa huduma kupitia mtandao, anatakiwa kutimiza masharti haya. Hata hivyo, wale wanaopata mauzo ya mwaka yasiyozidi shilingi milioni nne (TZS 4,000,000) hawatawajibika kulipa kodi ila watatakiwa kujiandikisha.

SOMA ZAIDI: TRA Yatoa Mwezi Mmoja Wafanyabiashara Mtandaoni Kujisajili

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa muda wa kujiandikisha ulianza tarehe 24 Julai 2025, na ulipaji kodi kwa wanaostahili utaanza kutekelezwa kuanzia 1 Agosti 2025 hadi 31 Agosti 2025. Kamishna Mkuu amebainisha kuwa kutakuwa na nafasi ya kuomba muda wa nyongeza kwa wale watakaokuwa na sababu maalum.

“Tumepokea maombi kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wa upangishaji kupitia majukwaa kama Airbnb, Booking.com, Agoda na Expedia, wakitaka muda zaidi wa kutekeleza matakwa haya. Tunazingatia maombi hayo na tutaamua kama nyongeza itatolewa,” ibainisha sehemu ya taarifa hiyo.

Itakumbukwa kuwa mnamo tarehe 24 Julai 2025, Kamishna Mkuu wa TRA alitoa tangazo kuwa wafanyabiashara wote wa mtandaoni wanatakiwa kujiandikisha ndani ya siku 30, kuanzia tarehe 1 Agosti, 2025 hadi 31 Agosti 2025.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×