Taarifa ya utafiti wa ajira rasmi na mapato inaonesha mwaka 2023/24, kulikuwa na jumla ya ajira rasmi 4,073,887, ambapo ajira 2,853,566 zilitoka sekta binafsi na ajira 1,220,322, kutoka sekta ya umma.
Katika mwaka huo jumla ya ajira 364,787 zilizalishwa Tanzania ambapo ajira 155,792, zilikuwa ni mpya kabisa. Mikoa iliyoongoza kwa kuzalisha ajira rasmi Tanzania 2023/24. Jumla ya mishahara yote katika sekta rasmi ni Trilioni 37. Fuatilia zaidi katika kielelezo cha picha:
