The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

‘Maisha Hayawezi Kuendelea Kama Kawaida’: Mohammed Kibao Afunguka Mwaka Mmoja Baada ya Mauaji ya Baba Yake

Mtoto wa Ali Kibao, Mohammed, anazungumza na The Chanzo kuhusu simanzi, jitihada zake za kutafuta haki na athari za mauaji ya baba yake kwenye maisha yake binafsi.

subscribe to our newsletter!

Dar es Salaam – Septemba 6, 2025, ilitimia mwaka mmoja kamili tangu Ali Mohammed Kibao aliporipotiwa kutekwa alipokuwa kwenye basi, akiwa safarini kuelekea nyumbani kwake mkoani Tanga. Siku iliyofuatia, ambayo ni Septemba 7, 2024, mwili wa Mzee Kibao ulipatikana maeneo ya Ununio jijini hapa, akiwa bila tayari amepoteza maisha, na mwili wake ukiripotiwa kuwa umeharibika sana.

Mambo mengi yametokea baada ya tukio lile. Tuliona Serikali ikijitokeza, ikilaani na kuahidi hatua zingechukuliwa. Tuliona Waziri wa Mambo ya Ndani wakati ule alienda mpaka Tanga kushiriki kwenye msiba. Lakini sasa tunaenda kumaliza mwaka wa 2025, bado hatujajua nini haswa kimetokea, na nani walikuwa wahusika.

Kujadili haya na mengineyo yanayohusiana na jambo hili, mwadishi wa The Chanzo, Khalifa Said, amezungumza na mtoto wa Kibao, Mohammed, ambapo, pamoja na mambo mengine, mazungumzo yalijikita kwenye jitihada mbalimbali ambazo yeye anazichukua kwenye kulipazia sauti suala hili na kuhimiza uwajibikaji.

Ifuatayo ni sehemu ya mazungumzo hayo:

Khalifa Said: Mohammed, Karibu sana The Chanzo.

Mohammed Ali Kibao: Asante, asante Khalifa. Tulijaribu kufanya mazungumzo haya muda mrefu, na nakushukuru kwa kuchukua nafasi, kwa kunipa fursa na kuchukua muda wa kuongea leo. Asante.

Khalifa Said: Ni muhimu umetaja hiyo kwa sababu mtu anaweza akadhani kwamba mazungumzo haya pengine yamesababishwa na matukio yaliyokuwa yanatokea hivi karibuni. Lakini, kusema kweli, haya ni mazungumzo ambayo tumekuwa tunayapanga siku nyingi kuyafanya. Imetokea tu kwa bahati nzuri kwamba tunayafanya leo.

Mohammed Ali Kibao: Ni kweli. Asante. Labda nianze tu kabla ya yote kutoa ufafanuzi kidogo wa majina, kwa sababu naona yanajirudia rudia: Mohammed Kibao, Mohammed Ali Kibao, Ali Mohammed Kibao. Sasa sisi tulikuwa na utamaduni katika familia zetu. Babu yangu, mzee wa baba, alikuwa Sheikh Mohammed Ali. Mimi baba yangu ni Ali Mohammed Ali Kibao, na mimi nikawa Mohammed Ali Kibao. So majina yamejirudia sana. Sasa tulipoanza mambo ya mtandaoni huku, mimi nika-adopt jina la baba kabla yeye hakulichukua mitandaoni kwa sababu ‘Ali‘ ni rahisi. Umeona? Sasa nafafanua hivyo kwa sababu dada zangu na mama wakiangalia wakisema “unaongea na Ali Kibao,” watasema “Ali Kibao yupi?” Sisi kwetu Ali Kibao ni yule aliyefariki.

Khalifa Said: Aha, sasa, It’s funny, kwa sababu wenzangu hapa wakati tunajaribu kuseti mitambo walikuandika “Mahojiano na Mohammed Ali Kibao”. Na mimi nikawaambia hapana, ni Ali Kibao. Nikamwambia Mohammed Ali Kibao ni baba yake.

Mohammed Ali Kibao: Hayo ni majina kwa ufupi tu. Majina ya mitandaoni ni rahisi kuandika handle, kwa mfano, ya Ali Kibao. Nikaichukua kabla baba hakuichukua Twitter.

Khalifa Said: Kwa hiyo, samahani. Kwa hiyo, wewe jina lako ambalo lipo kwenye cheti cha kuzaliwa ni jina gani?

Mohammed Ali Kibao: Mohammed Ali Kibao.

Khalifa Said: Na baba yako?

Mohammed Ali Kibao: Ali Mohammed Kibao.

Khalifa Said: Aha!

Mohammed Ali Kibao: Na babu ni Sheikh Mohammed Ali Kibao.

Khalifa Said: So basi itakuwa unacheka sio, ukiona waandishi wa habari tunavyoripoti haya majina?

Mohammed Ali Kibao: Sana. Nimesoma mara nyingi sana naona, haya basi heri. Lakini cha msingi ni kwamba jina la ukoo wa Kibao ni jina ambalo lina historia ndefu nchini, katika familia ambazo tumeshiriki katika mengi, katika mambo ya dini, siasa vile vile. Na hilo ndio la msingi, kwamba ni jina la Kibao na ni jina ambalo nina fahari kubwa kulibeba na hopefully kadri siku zinavyozidi kwenda tutalitendea haki.

Khalifa Said: Hebu tujuze kidogo kuhusiana na hiyo historia, kwa sababu nina maswali nimeandaa lakini umejaribu kugusia hapo. Kwa ambao pengine sisi ni wageni wa historia ya nchi labda na mambo yanayotokea, familia yenu ina historia gani ambayo umejaribu kuidokezea hapo?

Mohammed Ali Kibao: Mimi sio mwanahistoria mzuri wa kuiongelea kwa niaba ya familia kwa sababu nilipomaliza tu shule ya msingi, Mzee Kibao alinipeleka boarding school kuanzia Form One mpaka nimemaliza Form Six, na chuo nikaenda kusoma nje vile vile. So sikuwa karibu sana na mengi ya familia. Isipokuwa jambo ambalo liko wazi ni kwamba, pamoja na kwamba ni jina ambalo hutalisikia sana kwa maana kwamba ni watu maarufu wameshika vyeo mbalimbali, sisi kitu kimoja ambacho tuko nayo tangu vizazi vya nyuma vilivyotutangulia ni siku zote masuala ya haki.

Niongelee babu yetu, Sheikh Mohammed Ali, ambaye alishika nyadhifa mbalimbali, mojawapo ikiwa ni kuwa Sheikh Mkuu wa BAKWATA Tanzania. Wakati huo ni mtu ambaye aliheshimika katika uhai wake. Ah, na vile vile sidhani… najaribu kufikiria mengine ambayo naweza kuyaongelea hapa bila ya kuwakwaza watu.

Mohammed Ali Kibao: Sisi ni watu ambao tunajitahidi sana kukaa kwenye spotlight. Umeona eh? Kwa sababu kuna namna nyingi za kufanya mabadiliko, namna nyingi za kusogeza na kusaidia watu. Tunajifaharisha sana kuwa ni watu private. Kwa hiyo tuko… um… lakini ni familia kubwa ambayo tumeshikana. Na waliotutangulia, babu zetu na bibi zetu, walifanya jitihada kubwa sana za kushikanisha ukoo kuwa pamoja. Umeona? Kwa hiyo ni ukoo ambao umetawanyika, tuko sehemu nyingi sana duniani. Ah, sisi binafsi kwenye familia ya Mzee Kibao watu wako sehemu mbalimbali nchini, sehemu mbalimbali duniani, na wengine wengi kwenye extended family pia tumetawanyika sana.

Khalifa Said: Okay. Umezungumzia kuhusiana na familia yako na kwenye muktadha mzima wa haki. Labda tu hiyo ndio ilipelekea labda Mzee wako akajikuta yupo kwenye siasa za vyama na particularly Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Kuna uhusiano kati ya huo uamuzi wake kujihusisha na CHADEMA na hiyo historia ya familia yenu kusimama au kuji-associate na maswala ya haki kama ulivyodokeza hapo?

Mohammed Ali Kibao: Jambo ambalo alitusisitiza sana baba ni kuwa na fikra zako mwenyewe kama mtu. Umeona? Kwa hiyo hakushinikiza, na alijitahidi sana kutofautisha shughuli zake hasa za kisiasa na mambo yake ya biashara. Siku zote alikuwa anaongea kwa wazi na kujaribu kutufunza katika hayo. Lakini ilipofikia maswala ya siasa, um, hakujichukulia kwamba yeye ni mkombozi yuko pale anapigania watu. At least kwa jinsi ambavyo alituonyesha sisi.

Alichokuwa anasisitiza sana, hasa mimi kwangu, kwa sababu mwaka 2005 wakati nadhani ilikuwa ndio mishemishe za Uchaguzi Mkuu wakati ule ilikuwa ni Kikwete nadhani, mimi nilikuwa Handeni pale baada ya kumaliza shule. Aliniambia, “Wewe bado akili hazijakaa sawa, hebu njoo tufanye kazi kidogo kabla hujaenda chuo. Una akili za kitoto bwana”. Nilikuwa naye Handeni pale, alikuwa ni Katibu Mwenezi wa CCM. Nilifanya naye kazi sana. Mimi ndio nilikuwa dereva wake. Nilifanya naye kazi sana vijijini. Unaona? Eh.

Siku zote yeye alichosisitiza katika haya ni kwamba mabadiliko ya kweli yanatoka chini. Na Mzee Kibao nchi alikuwa anaijua vizuri sana. Ingia kwenye majukwaa hutamuona. Lakini ukiingia, kwa mfano mimi naweza kuongelea binafsi mfano wa Handeni pale, lakini kuna vijiji vingi sana nchini ambavyo alikwenda akagusa watu wengi. Na alinisisitiza sana kwamba mabadiliko ya kweli yanatoka huku chini, ingawa wengi ambao wanachukua madaraka wanapenda spotlight. Umeona? Lakini huwezi kufanya mabadiliko bila ya kutoka chini.

Kwa hiyo siasa yeye alijihusisha nazo muda mrefu sana, umeona, ah, kwa namna mbalimbali. Na ni mtu ambaye, pamoja na kwamba alikuwa ni mtu wa msimamo, lakini hakusita kubadilisha mtazamo alipopata taarifa mpya. Hilo ni jambo moja kubwa sana ambacho nilijifunza kutoka kwake: kwamba ndio, unaweza ukaamini kitu kimoja leo, lakini ukipata taarifa mpya na ukiona kwamba kuna mabadiliko yanahitaji kufanyika, basi nenda pale ambapo unaweza ukafanya mabadiliko hayo bila ya kuwa na ule ushabiki, ile loyalty tu kwamba “basi mimi ni mshabiki wa Simba basi hata Simba ikiniudhi nitaendelea kushabikia”. Sio hilo. Hilo ni katika jambo moja kubwa sana la msingi ambalo nimejifunza kutoka kwake.

Khalifa Said: Ah, kwa hiyo kumbe Mzee Kibao alikuwa ni mwanachama wa CCM alafu baadaye ndio akaenda akajiunga na CHADEMA?

Mohammed Ali Kibao: Yeah, sio mwanachama tu, alikuwa Katibu Mwenezi.

Khalifa Said: Ah!

Mohammed Ali Kibao: Nakumbuka kuna siku alikuwa amepishana kimawazo na Mwenyekiti Handeni pale. Akaniambia, “Unajua tatizo la mtu kama Mwenyekiti ni kwamba yeye anakaa ofisini alafu anatoka pale anaenda kuripoti makao makuu na anataka kutetea kazi na nafasi yake. Umeona? Hawajui hali halisi iliyoko huku chini”. Na ndiko yeye alikoshikika sana. Lakini alikuwa ni mwanachama wa CCM.

Lakini pia nisitize kwamba yeye na Mbowe wametoka mbali sana. Mimi Freeman tangu sijajua siasa ni kitu gani nakumbuka jina la Freeman lilikuwa likitajwa. Mzee alikuwa ni mfanyabiashara, alifanya shughuli nyingi tofauti tofauti sana. Ah, mimi binafsi niseme hapa kwa mara ya kwanza labda, wakati mimi nazaliwa Babati, Mzee alikuwa yuko Kenya. Wakati ule ndio mambo ya Ujamaa, ah, yeye alikuwa anaenda kutafuta sabuni na Colgate, kutoa nchi moja kuleta nchi nyingine. Umeona? Amekuja alipata mushkeli kule na vyombo vya usalama Kenya, bila ya kusema mengi. Lakini nilizaliwa katika mazingira hayo. Kwa hiyo siku zote alikuwa ni fighter.

Akaingia kwenye maswala ya shughuli za madini, alifanya sana Handeni pale, ilikuwa ndio sehemu kubwa. Mimi nakumbuka wakati tuko watoto nyumbani kulikuwa na watu kutoka nchi mbalimbali, kuna Wakorea. Tuna mmoja tulikuwa tunamuita “Mr. Mingi Mingi” sababu ndio neno pekee la Kiswahili ambalo alilijua. Kwa hiyo alifanya shughuli nyingi na kipindi hicho ndio majina kama ya kina Freeman tulikuwa tunayasikia. Kwa hiyo yeye na Mbowe wametoka mbali. Na siasa pia yeye ametoka mbali, amenihusisha sana. Nilikuwa nimekaa sana na kina Kigoda wakati ule marehemu Handeni pale, wakati ni Mbunge, wakati Waziri. Ah, nimeona kujifunza mengi.

Khalifa Said: Aha. Na ilikuwa ni lini unakumbuka alijiunga na CHADEMA?

Mohammed Ali Kibao: Um, siku halisi, mwaka halisi sifahamu. Lakini nadhani ni baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2005, kwa sababu mimi 2006 niliondoka kwenda chuo. Kwa hiyo sikuendelea kufuatilia sana siasa na yeye mwenyewe alivyokuwa akijihusisha na siasa. Tulifanya mambo mengine ya shughuli za kibiashara. Tulikuwa tunashirikiana lakini maswala yake ya kisiasa hakutuhusisha sana. Aliweka pembeni kwamba hizi ni shughuli tu kama shughuli nyingine. Na sina hakika hasa.

Khalifa Said: Na bila shaka atakuwa hakuwahi kukuambia kuhusiana na sababu iliyopelekea kuchukua uamuzi huo?

Mohammed Ali Kibao: Sio kwa maneno mengi. Um, sio kwa maneno mengi, lakini kama nilivyosema awali, yeye alikuwa sio mtu wa ushabiki. Alikuwa ni mtu ambaye anaenda kwenye upande ambao angehisi… ni risky hapa kumuongelea yeye katika mengi… lakini siku zote alikuwa ni mtu ambaye anaenda kwenye upande ambao angehisi kuweza kufanya mabadiliko zaidi, au kuleta mabadiliko ambayo yeye angeyaona yanahitajika kwa wakati ambao unahitajika. Um, kama ilikuwa ni CCM kipindi kile, alifanya kwa sababu aliamini kwamba kwa wakati ule ilikuwa ndio move sahihi. Ah, kama alipokwenda CHADEMA au popote pale alipokuwepo, ni alikuwa guided na hivyo: kwamba kwa sasa hivi hapa ndio sehemu ambayo nahisi kwamba naweza nikafanya mabadiliko makubwa zaidi, naweza nikawa na impact, ndio akaenda.

Khalifa Said: Na unavyokumbuka, alishawahi kugombea labda nafasi yoyote ya kisiasa, ukiachana na ndani ya chama? Pengine alishawahi kutaka kuwa diwani, mbunge?

Mohammed Ali Kibao: Alijaribu mara moja um na hakutaka tena. Kipindi kile ilikuwa ni muda mrefu lakini, yeah. Ni Handeni. Najaribu kukumbuka, nachukua muda kidogo kukumbuka kwa sababu kuna mengi yalitokea katikati, lakini alijaribu ubunge nadhani halafu akaachana nao. Akasema hapana, mimi mambo ya kushika madaraka huko juu siwezi, niendelee huku chini. Alipenda sana. Na alipenda sana kwa kweli. Kwa sababu nikisema hivyo najua first hand kwa sababu mimi kipindi kile, nachokuambia 2005, tulikuwa na biashara ya kusambaza vitabu kwenye shule za msingi Handeni pale. Umeona? Kwa hiyo mimi ilikuwa ndio kazi yangu kuja Dar kununua vitabu kutoka kwa publishers kupeleka kule kwenye mashule mbalimbali. Na nilikuwa nikiingia vijijini kule nikisema “Bwana nimeleta hapa, mimi mtoto wa Mzee Kibao,” kila mmoja anamjua. Na nilikwenda katika vijiji ambavyo viko ndani sana, umeona, ndani sana Handeni kule, na niliona impact yake. Umeona? Kuna watu mpaka watoto wameita “Ali Kibao”. So yeye alipenda sana, sana kufanya kazi chini zaidi ya juu.

Khalifa Said: Mmh, na hiyo ilikuwa ni mwaka gani au hiyo ya…?

Mohammed Ali Kibao: Ilikuwa ni kuelekea 2005, 2004-2005. Maana yake nilimaliza sekondari Ilboru pale Form Six um yeah, 2004 kwenda 2005 ilikuwa pamoja pale.

Khalifa Said: Aha. Nataka tu kuelewa so for clarity’s sake, Mzee Kibao hakuwahi kuwa mtumishi wa umma?

Mohammed Ali Kibao: Sio katika maisha yetu sisi. Hapana. Yeye alikuwa ni mfanyabiashara na alishiriki katika siasa na vyama mbalimbali katika uhai wake, lakini hakuwahi kuwa mwajiriwa wa serikali. In a sense, tunafahamu kwamba alikuwa ni mwanajeshi kama ambavyo ilikuwa ni lazima kupitia jeshi kipindi kile. Alikuwa ni mwanajeshi wakati wa vita ya Uganda. Alishiriki katika mambo tofauti tofauti ah mengine ambayo alitusimulia, mengine ambayo hatuyajui rekodi zipo kama zipo, kama kuna ambaye anazo anaweza akatusaidia nazo vile vile, lakini mengi tunayoyafahamu ni kutoka kwake mwenyewe kutuhadithia mambo mbalimbali. Lakini kuwa mtumishi wa umma as in ameajiriwa na serikali, ah mimi sina taarifa hizo.

Khalifa Said: Mmh. Kwa hiyo unachomfahamia yeye ni kwamba ni kwenye biashara na siasa.

Mohammed Ali Kibao: Biashara na siasa. Yeah.

Khalifa Said: Umeshajaribu kumchora, kwa sababu hilo ni swali pia ambalo nilikuwa nalo. Ah, lakini nilikuwa nataka ueleze, if you can, kwa undani kidogo kuhusiana na kumchora zaidi. Alikuwa ni mtu wa aina gani? Umegusia kwa kiwango fulani lakini nilikuwa nataka ueleze kwa undani if you can. Mzee Kibao alikuwa ni mtu wa aina gani? Yaani unaweza kumuelezea vipi? Kwa mfano kama unamwelezea Mzee Kibao kwa mtu ambaye hajawahi kumsikia au kumuona, how would you have described him?

Mohammed Ali Kibao: Katika mambo ambayo mtu yeyote aliyefanya naye kazi kwa muda wowote zaidi ya mwaka, miaka miwili, au mtu yeyote ambaye alikuwa karibu naye kwa muda mrefu kipindi chochote zaidi ya mwaka… Kwa mfano kitu kimoja ambacho mpaka leo mimi nakihisi impact yake ni uwezo wake wa kuona mbali. Mwenyezi Mungu alimjalia hiyo, kwamba alikuwa ni mtu ambaye akikaa, ah kwanza huwezi jua kinachoendelea akilini kwake. Hilo ni moja.

Ah pili, alikuwa na uwezo wa kuunganisha dots mbalimbali na kuona mengi sana. Nitakupa mfano mdogo: um, anaweza akakwambia “Bwana usiende kushoto hapo, ukienda kitakachotokea ni moja mbili tatu”. Na hiyo sio mimi tu. Yeyote yule aliyefanya naye kazi, yeyote katika familia yetu, atakuambia. Atakuacha utaenda, baada ya siku mbili tatu utarudi utasema “Bwana kweli”. Na mimi mpaka leo nina mke, nina watoto, na nimekuwa ni mtu mzima na ya kwangu bado kuna ambayo aliniambia huko nyuma ndio unayaona sasa hivi. Nadhani hilo sio tofauti kwake tu, ni wazazi wengi wako hivi. Hilo ni moja.

Lakini pili, um katika swala lake, uwezo wake wa kuona mbali alisisitiza sana sisi tuwe ni watu wa kujifunza, kusoma elimu na vile vile kujifunza siku zote. Ah, maneno yake, jambo lake kubwa ilikuwa ni kwamba “Mimi siwezi kuachia urithi wa mali nyingi, lakini nitapigania kila atakavyo, kila atakayetaka nitamsomesha mpaka pale mwenyewe atakapoona kwamba ah, amefikia ukomo wake”. Nakumbuka mimi kama mtoto wa kwanza wa Mzee Kibao, wakati ule shule pale shule za msingi alitupeleka katika shule ya Popatlal pale Tanga ambayo ilikuwa ni gharama yake ni kubwa sana. Mpaka wenyewe, watu wengine wa familia wakamwambia “Wewe una wazimu? Hata hela ya kula inakushinda unapeleka watoto huko kwenye English Medium?” Akawaambia, “Nyie hamjui, ulimwengu unabadilika huu. Umeona? Nawaandaa hawa watoto waje kuwa ni watu wanaoweza kujitegemea na watu wenye elimu”.

Kwa hiyo um, nikim-summarize yeye kama mtu ni ngumu sana kwa sababu alikuwa ni mtu wa mambo mengi sana. Alisafiri sana, alikutana na wengi, alifanya mengi ah biashara, siasa…. Lakini kitu ambacho mimi binafsi siwezi kukisahau au kuchukulia kwa wepesi ni uwezo wake wa kuona mbali na kuwa na subira, kwamba mabadiliko siku zote hayatokei kwa usiku mmoja. Umeona? Na mengi ambayo ame-sacrifice kutusaidia sisi kama watoto, tulikuwa hatuyaoni wakati anayafanya lakini manufaa yake unayaona baadaye. Na nadhani hiyo ilikuwa ni theme katika maisha yake. Umeona? Ali-sacrifice mara nyingi sana um mambo ya muda mfupi ili ya muda mrefu yatengemae. Umeona? Alikuwa ni mtu ambaye ange-sacrifice kwamba “Ah hili jambo ni la muda mfupi, it’s painful now, inauma sasa hivi, lakini it will get better tukivuka hapa”. Na hiyo ilikuwa ni principle yake moja kubwa sana.

Khalifa Said: Mmh. Of course pengine kitu kingine ambacho kinamuelezea ni kwamba alikuwa ni mtu wa kufanya kazi kwa background, sio like sio mtu wa kuonekana kwenye hadhara, kwenye nini. Ni mtu wa background.

Mohammed Ali Kibao: Yeah. Hilo hilo hakutaka umaarufu siku zote yeye, hakutaka umaarufu. Alipenda sana, ndoto yake kubwa kabisa, na linanihuzunisha sana kwamba hakufanikisha hilo… Lakini ndoto yake kubwa yeye ilikuwa siku zote anasema, “Kwanza mimi nataka tu niwe na shamba, niwe na kibanda changu na mifugo. Niamke asubuhi nione kuna kuku, viji-mbuzi pale”. Yaani ilikuwa ndio ndoto yake katika maisha. Hakutaka ufahari ule kwamba aje kuishi sijui kwa anasa. Yaani hiyo ndio ilikuwa ndoto yake kubwa, siku zote alikuwa akiiongelea.

Kwa hiyo ni mtu ambaye alikuwa simple. Mtu simple kiasi kwamba nyumbani pale yeye siku zote akija huwa ana masharti yake tu mawili, ndio anavaa hayo hayo kila siku. Nakumbuka mama anasema, “Sasa hili shati limechanika…” anasema “Sasa la nini? Ndio shati langu ndio”. Umeona? Alikuwa ni mtu wa mambo simple ambaye hakupenda makubwa. Na ndio maana mpaka anafariki amechukuliwa kwenye basi. Sio kwamba hakuwa na uwezo; kama angetaka kuendesha magari ya kifahari au kufanya angefanya. Umeona? Alikuwa ni mtu simple. Alikuwa ni mtu simple, simple sana. Na mtu asiyeelewa anaweza kuuliza, “Sasa huyu mzee mpaka saa hizi anaenda panda kwenye basi?” No, efficiency kwake, simplicity kwake ilikuwa ni jambo la muhimu na msingi sana.

Khalifa Said: Asante sana. Nilikuwa najaribu tu kuwaza hapa how often ulikuwa unazungumza naye? Ah, na pengine mara yako ya mwisho kabla ya kutokea kile ambacho kilimtokea ilikuwa ni lini kuzungumza naye? Najaribu I want to pick your mind on your last memories au kumbukumbu zako za mwisho za Mzee Kibao. How often ulikuwa unazungumza naye? Ah mlizungumza lini mara ya mwisho? Kumbukumbu zako za mwisho unamkumbuka vipi mwishoni mwishoni?

Mohammed Ali Kibao: Nitaongea swala moja binafsi sana na linauma. Lakini nitalisema hili ili yeyote ambaye ana mzazi sasa hivi yupo, unamuona mama, unamuona baba, mtu… Lazima tunaambiwa siku zote kwamba “bwana wapende wazazi wako, wapigie simu, ongea nao, kuna siku hawatakuwepo”. Umeona? Sababu ya kutokujihusisha na siasa kwa binafsi hujawahi kuniona nikiongelea maswala ya siasa huko na kule, umeona, tulikuwa tuna utofauti sana wa mawazo. Na jambo ambalo alilikaribisha sana Mzee Kibao, hata kama tulikuwa tunaweza kugombana, alikaribisha sana utofauti wa mawazo: “Wewe sema kinacho… kilicho moyoni sema”. Umeona?

Na wakati mwingine tulikuwa tunakwaruzana mengi tu pamoja na maswala ya kisiasa. Umeona? Tulikuwa tunakwaruzana kwa sababu mtazamo wangu na wa kwake ilikuwa ni tofauti kidogo katika katika maswala ya kisiasa na mengine. Kama nilivyosema awali, sikuyaelewa mpaka sasa. Umeona? Sasa unaongea kwamba kuongea… tulipokuwa tunaongea, tuliongea tukiongea ilikuwa tunaongea kwa masaa, sio tu kupiga simu dakika mbili tatu. Unaongea kwa masaa, masaa mawili matatu. Umeona? Unaongelea kila kitu kuanzia siasa, familia, watoto, wajukuu. Fahari yake kubwa kabisa, fahari yake nimeongelea kwamba alikuwa mtu simple, lakini fahari yake kubwa kubwa ilikuwa ni ah wanawe, watoto wake, wajukuu zake, familia. Hiyo ndio ilikuwa fahari yake. Anasema, “Unajua watu wengine wanaona tuko 10 sisi, matumbo tofauti tofauti tuko 10. Mimi ni wa kwanza, nina wenzangu wengi”. Ah, ilikuwa ni fahari yake kubwa.

Kumbukumbu yangu ya mwisho ya Mzee Kibao siko tayari kuiongelea kwa wazi kwa sababu… sababu ni kumbukumbu ambayo ningetamani kupata nafasi ya kuirekebisha. Lakini pamoja na yote, najaribu sana kumkumbuka kwa mema aliyotusisitiza na mafunzo yake mengi ambayo mpaka sasa yalinisaidia katika maisha. Umeona? Alinitengeneza kuwa tayari sana katika maisha. Sana, sana. Na ali-sacrifice mengi sana ili mimi kufikia hapa nilipo. Hata mimi kukaa hapa kuongea na wewe leo ni kutokana na sacrifices zake. Kwa hiyo inshallah Mwenyezi Mungu akijalia huko mbele naweza kufunguka zaidi. Lakini…

Khalifa Said: Hapo umejaribu kugusia kwamba ah mlikuwa na utofauti wa kimawazo na vitu kama hivo. Na najaribu tu kuwaza, unadhani kile ambacho kimetokea kwake kimesaidia kwa namna moja au nyingine kuamua nani kati yenu alikuwa yuko sahihi?

Mohammed Ali Kibao: Um, kila mmoja wakati mwingine unaweza kuwa sahihi hapa na pale. Lakini kwa sehemu kubwa, 99%, Mzee Kibao alikuwa sahihi. Mara chache sana… ah na akikosea hakuambii, sindio? Lakini kilichomtokea, kama unamaanisha kwamba utekwaji wake na mauaji yake…

Khalifa Said: Mmh.

Mohammed Ali Kibao: Sisi na mimi binafsi niongelee, lakini sisi kwa ujumla kama familia, tumejitahidi sana kutenganisha matukio haya na siasa. Na ndio maana hatuongelei sijui CCM. Hapa tu nimeongelea kutoa background kidogo kwamba alikuwa ni mtu wa siasa na hivi na vile vile. Lakini haijalishi mtazamo wake wa kisiasa, haijalishi alikuwa anafanya kazi na nani wapi, hakuna mtu ambaye anastahili kupitia aliyoyapitia yeye. Hakuna mtu ambaye anastahili kuuawa kinyama kiasi kile. Hakuna. Kwa hiyo ah ni tumefanya kwa makusudi, jitihada za makusudi kutenganisha. Na ndio maana hutanisikia nikitaja jina la kina Mnyika. Ukitaja, pamoja na kwamba walikuwa marafiki, utanisikia nikimtaja Freeman. Umeona? Kwa sababu ukishaongelea tu siasa, basi zinakuwa ni kama vile mambo ya ushabiki sasa, kwamba “ah huku sijui CCM, huku CHADEMA, huyu ni mtu wa CHADEMA”. No. At the end of, baada ya mwisho wa yote hayo, ni binadamu. Umeona? Sisi wote ni binadamu. Sisi wote ni Watanzania. Um, siasa tuziweke pembeni.

Kwa hiyo kilichomtokea sifikirii kwamba ni nani yuko kwenye right au nani yuko kwenye wrong. Hapana. Nafikiria kwamba ni chachu. Chachu nadhani ndio neno sahihi. Um ya sisi kama watoto kuendelea kupigania ah yale mema na mabadiliko ambayo angependa kuyaona. Na vile vile kuendelea kupigania ili isije familia nyingine yoyote ikapitia kama haya. Hatuwezi tu kukaa kimya na kukaa pembezoni na kuangalia tu. Um, sio… ni ngumu sana kwa sababu unaona. Ah, kwa hiyo mpaka kila mtu afikwe sasa ndio aanze kuongea? Umeona? Lakini kama kuna yeyote ambaye anasikiliza na anayetaka uamsho, sio lazima mtu uende ukapiga kelele kwenye majukwaa au mitandaoni ili ulete mabadiliko. Kila mmoja katika nafasi yake, katika nafasi yetu, tuna uwezo wa kupigania au kujaribu angalau kuleta mabadiliko ambayo tunataka kuyaona. Kwa hiyo siangalii kwamba alikuwa sahihi au hakuwa sahihi. Hapana.

Khalifa Said: Lakini kwenye haya maisha… kwa mfano najaribu kutafuta namna ya kuliweka swali langu vizuri. Ah labda niulize: hiki kilichomtokea ilikuwa ni mojawapo ya hofu ambazo nyinyi kama familia kwa mfano, au wewe kama kijana wake, ziliwahi kuwepo akilini mwako? Ah kwa sababu kwenye haya maisha yetu ya kila siku, mtu kulingana na vitu anavyovifanya watu wanakuwa wana hofu. Iini kwa mfano mtu kama unamuona… zipo sasa hivi hizo sio na inayotokea kwangu mimi binafsi. Ah watu wanasema “ah hujatekwa? Ah bwana usifanye hivi, bwana utatekwa, ah utafanya nini”. Kwa hiyo kuna hofu fulani watu wanakuwa wanazo ah akilini mwao kuhusu wewe. Na kwa hiyo hata ukifikwa na lile jambo, of course watasikitika, lakini ni jambo ambalo walikuwa wanahofia kwamba lingeweza kukutokea. Hiki ambacho kilimtokea Mzee Kibao, ni moja kati ya hofu ambayo iliwahi kuwepo kwenye akili yako? Kwamba ah, kwamba hiki kingeweza kutokea?

Mohammed Ali Kibao: Una… kulingana na ukiangalia jinsi ambavyo siasa za Tanzania zimeendeshwa kwa miaka labda 15 iliyopita, 10-15 iliyopita, lazima unakuwa unafikiria hivyo kwamba dah, unajua inaweza ikafikia ah hatua hili likatokea. Lakini sikutegemea. Umeona? Unahisi kwamba wanaweza wakamdhuru. Hofu yangu kubwa ilikuwa ni kwamba wangemchukua wakamweka ndani. Ah kwa sababu na rafiki yangu ah ambaye mzazi wake alipitia hayo, ah tunafahamu wote stori ya kina Mzee Shamte kwa mfano. Umeona? Kutusikitisha sana.

Khalifa Said: Hasa.

Mohammed Ali Kibao: Hata tulipopewa taarifa kwamba ameshushwa kwenye basi, ilikuwa ndio hofu yangu kubwa. Mzee alikuwa na presha, alikuwa akasema watamweka ndani atakuja adhurike. Umeona? Lakini haikuniingia akilini kwa sababu si unahisi kwamba labda mtu haonekani huko, umeona, hivi na vile vile. Umeona? Hao wanaoteka hujui criteria wanayoitumia ni ipi. Kwa hiyo unaweza ukajiona uko salama, ukawa huko salama, na unaweza ukajiona labda huko salama lakini hatujui criteria. Angalau kama ingekuwa kuna sheria zinafuatwa. Sasa hofu ilikuwepo, lakini haukutegemea. Mpaka leo mimi binafsi nahisi kama vile kuna siku atanipigia tu simu niambie “bwana ah haikutokea hivyo”. Umeona? Waswahili wanasema “uchungu ndio uchukwao”. Lakini hiyo nakuambia ili kukuonyesha ni jinsi gani ambavyo hatukutegemea. Na nadhani kuna wengi ambao tunadhani kwamba ah pamoja na yote ndio haya yanayotokea tu wengine. Umeona? Yanatokea wengine. Ah lakini kwa jinsi mambo yanavyokwenda au yalivyokuwa yakienda nchini hopefully kwa sasa tutakuwa tumebadilisha mwenendo kidogo kutokana na yaliyojiri tangu Oktoba 29. Lakini kwa yaliyojiri kabla ya hapo, hofu ilikuwepo lakini hatukutegemea kabisa kwa kweli.

Khalifa Said: Asante. So kama nilivyotangulia kusema pale kwenye utangulizi wangu kwamba sasa hivi ni mwaka na ushee, eh, mwaka na miezi miwili tangu tukio lile litokee na mpaka tunazungumza hivi sasa bado hatujajua exactly kilichotokea. Ah, mamlaka ambazo zinahusika kutupatia haya majibu, kila zinapoulizwa zinasema kwamba uchunguzi unaendelea na kwamba majibu yatatolewa pale utakapokamilika. Na nilikuwa nataka nikuulize, unadhani itafika wakati nyinyi kama familia mkubaliane tu na ukweli wa kile kilichotokea na kuendelea na maisha kama kawaida?

Mohammed Ali Kibao: Maisha hayawezi kuendelea kama kawaida kwa sababu ah utakuja mwaka mpya, itakuja Eid, kwa mfano Ramadhani. Unaona kwamba mtu dah, mimi kwa mfano naweza kukaa mtu unakula tu parachichi, unakumbuka jinsi mzazi wako mara ya kwanza alipokuwa anakula parachichi unamcheka unasema “ah unakulaje”. Umeona? Au unakula matango kwa mfano. Kwa hiyo zile kumbukumbu lazima zitakuwepo na zitakuwepo kwa muda mrefu. Na kukosa majibu kunapelekea ile kutoku-conclude. Yaani closure inakuwa haipatikani. Umeona? Kwa hiyo sidhani kama maisha yanaweza yakaendelea kama yalivyokuwa awali hata siku moja. Hili ni jambo ambalo… lakini sisi kama familia, mimi binafsi hasa, sidhani niko katika sehemu ambayo niko tayari kutokupata majibu yoyote kutoka popote. Umeona? Najua kwamba kuna uwezekano mkubwa sana kutokupata hayo majibu. Kwa hiyo hilo nimejiandaa kuishi nalo. Lakini kuendelea maisha kama kawaida hapa haiwezekani.

Khalifa Said: Aha. Na kwa sababu nilitegemea kwamba, nilitegemea kwamba kutokana na jitihada ambazo wewe binafsi unazichukua kwa mfano Disemba tu 5 ulijitokeza kuzungumzia swala hili pamoja na yale matukio ya Oktoba 29, nilidhani kwamba unafanya hivi kwa sababu unaamini kwamba bado kama familia na kama jamii, kama taifa, tunaweza kupata ah ukweli wa kile ambacho kimetokea, tukawajua waliohusika na pengine wahusika kuchukuliwa hatua?

Mohammed Ali Kibao: Katika mambo ambayo alinifunza baba ni kwamba ah huwezi kuacha kufanya jitihada za kupata yale unayoyataka kwa kujua tu kwamba ah yoyote huko nyuma hatukufanikiwa au… umeona? Hata kama kuna uwezekano mdogo wa kufanikiwa, ni jukumu letu kusukuma. Umeona? Kwa hiyo kuna uwezekano. Kwa sababu watu tunafikiria kwamba labda miaka mitano, 10, 20 ni mingi, lakini sio. Wewe angalia miaka 20 iliyopita ilivyokwenda haraka. Umeona? Kwa hiyo leo labda waliohusika leo hatuwezi, hawawezi kutupa majibu, ila tuna jukumu sisi ah na mimi binafsi kama familia ndio maana hata naongea na wewe hapa ili kuendelea kuendeleza huu mjadala. Kama hatutapata majibu, basi angalau kumulika mwanga katika haya matukio na jinsi yanavyoathiri watu ambao wanaachwa nyuma. Kwa hiyo ya, nafanya jitihada. Kuna matumaini madogo sana, lakini yanafifia kila siku. Lakini bado tuna jukumu la kuendelea kusukuma kutafuta haki na kutafuta majibu.

Khalifa Said: Lakini je kuna gharama? Ah kuna gharama unalazimika kuzipitia kwa kufanya hizi jitihada? Eh kama ulivyozungumza kwamba kukubali kuzungumza na sisi ni moja kati ya jitihada hizi, na sisi tunakushukuru sana kwa sababu katika mazingira kama haya, ah na hususan kwa ambacho kimetokea kwenye familia yenu, ingekuwa rahisi kusema hapana. Lakini ukakubali kuzungumza. Kuna changamoto zozote unazipata as an individual person ambazo zinasababishwa kwa namna moja au nyingine na hivi kuwa vocal au kujitokeza na kuzungumzia hili jambo? Kutokuliacha liende, eh, kutokuliacha… kutokukubali “kufunika kombe alafu mwanaharamu akapita,” kwamba unamshika mwanaharamu hakuna kupita hapa. Kuna gharama zozote unapitia, unalipa?

Mohammed Ali Kibao: Ya kwanza ni hofu. Mimi kabla ya kuongea mara ya kwanza ilibidi niende nikahakikishe kwamba bima yangu ya maisha iko vizuri. Umeona? Ah kwa sababu kama alivyosema awali, kwamba hatujui vigezo wanavyotumia kuua watu ni vipi. Umeona? Ah kwa upande mmoja tumeona ah wakina Ben Saanane, wakina Soka… Umeona? Ni rahisi kusema hao ni watu ambao wameamua kujifanya hii shughuli zao. Lakini kuna wengi, kuna majina karibu 81 ambayo yamekusanywa ya watu ambao hatujawahi kuwasikia, hatuwajui lakini hatujui waliko mpaka leo. Umeona?

So la kwanza ni hilo: hofu. Ah kwangu mimi, na vile vile kumtia presha mama, mama yangu mzazi, wadogo zangu. Umeona? Na ndio maana najaribu kuliongelea hili swala sio kishabiki ila kibinadamu zaidi: kwamba sio swala la siasa, ni swala la usalama, ni swala la utu, binadamu na Utanzania. Umeona? Unaona? Na yeah, la kubwa kubwa kabisa la kwanza ni hilo: ni hofu. Ah lakini ukiishi kwa uoga sasa, umeona, unaweza ukajihadhari na kila kitu, ukavuka tu barabara ukagongwa pia na gari. Siku zako zikifika… Kama Muislamu naamini kwamba Mwenyezi Mungu ndiye anayepanga yote. Umeona? Siku ikifika inatafuta tu sababu. Lakini kubwa kabisa ni hilo.

Khalifa Said: It’s interesting you say that kwa sababu kwenye ile video yako ya Disemba 5, ah ulijaribu kuonyesha kutokuwa na uhakika. Yaani kwa mfano kama watu wanakuja wanakuambia “bwana kuwa makini, eh kuwa makini na vitu unavyosema, bwana kuwa makini na vitu unavyofanya,” na wewe ukaonekana kama vile unapata shida kuelewa. Yaani inakuwaje makini? Kwa nini unaonekana kupata shida wakati unaelewa hatari zilizopo na ambazo umejaribu kuzigusia hapo?

Mohammed Ali Kibao: Sote tunajua jukumu kama Watanzania la kuhakikisha kwamba kwa nafasi zetu zote tunatengeneza nchi ambayo sisi kama wazazi, especially wazazi, tunatengeneza nchi ambayo itakuwa ni fahari kwetu. Waliotutangulia kama wangekuwa na hofu na uoga, um tusingekuwa tunafurahia matunda ambayo tumeyafurahia kwa miaka mingi. Wanakuwa “Kisiwa cha Amani” kabla ya vurugu hizi, kabla ya… Ukiangalia kabla, miaka 15 maybe 20 iliyopita, umeona, tuliishi maisha mema, maisha mazuri. Umeona? Na yote hiyo ni kwa sababu ya jitihada za watu ambao walijitolea. Sio kwamba mimi nataka nijitolee mhanga. Hapana, hakuna ambaye anataka hilo. Ila tuna jukumu katika nafasi zetu wote kushughulikia.

Kwa hiyo hofu ya kutokea chochote kwangu haizidi hofu ya mimi kupanda ndege, kwa mfano. Unaona? Haizidi. Hofu kama unaogopa kupanda ndege lakini inabidi uende nchi nyingine au uende uvuke bahari, umeona, utapanda na panapo majaliwa utafika. Umeona? Unaelewa umuhimu wa ile safari. Kwa hiyo unaweka pembeni hofu yako ya kupanda ndege, unapanda kwa sababu unajua kwamba destination unayokwenda ni muhimu zaidi ya ile hofu uliyokuwa nayo.

Kwa hiyo ni hilo. Na vile vile pia ah inafikia wakati ah mtu lazima uchukue msimamo. Umeona? Lazima usimame useme, ah bila ya kukwaza. Kwa sababu mimi hofu yangu kubwa ni kwamba sio mimi; tunaweza nikatoa tamko hapa akaenda akachukuliwa mdogo wangu ambaye yuko hapo, umeona, kwa mambo ambayo hayamuhusu. Wala ndio maana mimi hata naomba niseme hapa siwashirikishi. Hata hii interview hakuna anayejua anaifanya. Kwa hiyo wote mnayasikia haya kwa mara ya kwanza. Nikafanya mjadala na familia, sishinikizi familia yangu yoyote afanye chochote. Kila mmoja kwa nafasi yake atafanya anachoweza. Kwa hiyo kikubwa ni hicho: kwamba destination au kule tunakokwenda ni muhimu zaidi ya hofu ya safari. Unaona? Na inshallah Mwenyezi Mungu atajalia, yote ni mapito tu.

Khalifa Said: Yeah, pengine, pengine sababu nyingine ya kuamua kuendelea na hizi jitihada ni kwa sababu maybe you don’t want to be cynical, you don’t want to be maybe mbinafsi. Kwa sababu nadhani kuna japo kwamba of course mtu anayekuja anakuambia “kuwa makini” anamaanisha vizuri, ana nia nzuri, it comes from the point of love. Lakini hudhani kwamba pia kuna una mstari mwembamba kati ya kuwa careful na kuwa cynical?

Mohammed Ali Kibao: Nadhani wewe ni mtu ambaye uko katika position ambayo unaelewa hili vizuri zaidi kwa sababu sidhani kama mimi maonyo ninayoyapata yanakuzidi wewe kutoka familia yako, lakini kazi unayoifanya, umeona, sio kwamba unaifanya kwa sababu um unatafuta kwenye… kuwa hatuwezi kukaa ukahope… Niseme hivi: jambo la kwanza kubwa linalonifanya mimi niongee ni namna yangu mwenyewe binafsi ya kuomboleza na kumuenzi Mzee Kibao. He was a fighter, was not a coward. Na kuwa mimi… katika picha ambazo siwezi kuzitoa akilini ni picha ambayo wale waliomchukua wenyewe walikuwa hawamjui vizuri, kwa sababu kama kuna walichokuwa wanakitaka hawakukipata. Na ndio maana pengine ukaona kwamba hata walimtesa na kuharibu mwili, kwa sababu he would have known alikuwa anajua kwamba hapa this is the end, amefika mwisho, hakuna kubadilika. Na ni mtu wa msimamo hivyo.

Na mimi naamini ndani ya nafsi yangu kwamba mpaka wanamuua hakufa kinyonge pleading for his life hakufa kinyonge, umeona? So mimi ni namna yangu… ni namna yangu mwenyewe pia ya kuomboleza, ni namna yangu ya kumuenzi, kuendelea kupigania haki yake na haki za wengine ambao hawana sauti. Pengine au wengine ambao… majina nimetaja majina zaidi ya 81 ambayo mpaka sasa ni kimya. Umeona? Kwa hiyo tunajukumu sisi kupiganiana. Kama wananchi tunasema kwamba sisi ni wamoja, ni watu wa upendo, basi tuonyeshe kwa matendo pia.

Khalifa Said: Kama ambavyo umejaribu kugusia sasa hivi tu kwamba kuna watu wengine wengi ambao wamepotea katika mazingira ya kutatanisha na bado hawaonekani walipo. Kwa hiyo tukio la Mzee Kibao si isolated, in fact wakati linatokea… kuna matukio kadhaa nyuma yametokea na matukio kadhaa mbele yaliendelea kutokea. Na nilikuwa nataka kuupata mtazamo wako. Unadhani mamlaka zinazohusika ah kushindwa kuja na majibu yanayoeleweka kuhusiana na haya matukio inaweza kuwa ni moja kati ya sababu ya kile kilichotokea Oktoba 29 maandamano? Na pengine kama nchi, ah tungechukua jitihada zaidi za kuwapatia wananchi majibu ya yale matukio au haya matukio yanaendelea kutokea, pengine tusingeshuhudia kile ambacho tulikishuhudia Oktoba 29?

Mohammed Ali Kibao: Kabisa, kabisa. Ukiangalia miaka 10, 15 iliyopita ni mtiririko wa mambo haya. Na ndio maana nikasema hata kwenye ujumbe ule niliotoa Disemba 5 kwamba kama kuna yeyote anayetaka kujua kwa dhati tumefikiaje hapa kama nchi, toka tu popote uliza mwananchi yeyote. Muulize tu mtu ambaye yuko tayari kukuambia ukweli, atakwambia. Umeona? 

Kwamba tumefikia hapa kutokana na jinsi mambo yanavyoendeshwa, mojawapo na kubwa ni mambo haya ya watu kutekwa na kupotea, umeona, ah na kuuawa. Ah, ukiangalia kwa mfano swala la Tundu kupigwa risasi mchana, mpaka sasa kimya. Umeona? Alafu ah kukawa na escalation ya haya mambo. Umeona? Kwamba ilianza tu kwamba ah basi yule Tundu Lissu alikuwa ni mkorofi kule, umeona, Bungeni na ndio maana labda aliwaudhi watu fulani. 

Halafu polepole ukaanza: mwandishi wa habari hapa, sijui huyu mwanaharakati hapa, hapa huyu sijui… umeona… mpinzani hapa, mtu kapotea hapa, kapotea kule, kapotea hapa. Alafu yakaendelea. Sasa mimi binafsi najiuliza, je, na nadhani wengi wanaweza wakajiuliza, kuna uwezekano wa mambo makubwa matatu. Umeona? Kama kuna la nne na jingine basi unifahamishe Khalifa. Kwanza ni kwamba haya mambo yanatokea kwa sababu ah wanaoyafanya wametumwa. Umeona? Je ni hivyo? Ah wewe hatujui. 

Umeona? Eh hiyo ni possibility ya kwanza. Mimi nasema kama mtu ambaye nimefikwa, nikikaa nikijiuliza hivi kwa nini hatupati majibu nafikia conclusion hizi tatu. Hilo la kwanza. La pili: yanatokea na hayakemewi wala hayashughulikiwi kwa namna ambazo tunaziona kama mengine yanavyoshughulikiwa, kwa sababu yanawafurahisha au yanawanufaisha kundi fulani la watu. Umeona? 

Kwa sababu hayatokei kwenye vacuum. Umeona? Eh, yanatokea kuna cause effect. Kuna jambo linalosababisha haya mambo yatokee. Ah, kuna kikundi cha watu kimeamua kwamba fulani hata asiishi. Umeona? Kuna kikundi, kuna sababu zake. Hilo ni la pili.

La tatu na pengine la kutisha zaidi, ni kwamba je, haya yanatokea nje ya uwezo wa vyombo vya ulinzi na usalama? Kwamba hata ulinzi na usalama nao wanaogopa? Serikali nayo inaogopa kwamba imefikia hatua kwamba it’s out of control? Umeona? Eh, kwamba hata kukemea basi… Na ndio maana mimi nasema, hata kwa sababu tunaona Rais Samia sio mtu wa kurudi nyuma. Si tumeona juzi bwana alivyoongelea kwa ah kwa msimamo, umeona, kusema kwamba kama kuna mtu atataka kuleta vurugu na kuvurugika nchi basi tutatumia nguvu pia. Umeona? Sasa ile nguvu na ari na misemo ile hatuoni. Umeona? Hatuoni nguvu hiyo ikitumika kwenye haya mengine ambayo kila mmoja kama Mtanzania atakuambia kwamba “jamani hili ni tatizo”. Hatuoni hiyo nguvu.

Lakini huku unaambiwa bwana mbona uliacha mtoto akatoka usimwambie atoke? Umeona? Katoka, kauawa, basi. Umeona? Na ah ikifikia kwenye kulinda taifa serikali inatuambia, Rais anatuambia kwamba watatumia nguvu yoyote inayohitajika kulinda taifa. Je, kulinda taifa haihusishi pia kulinda uhai? Mimi kuna video moja ambayo kila siku naifikiria sana akilini. Soka… Soka anasema “jamani tubishane, tupishane kimawazo, tufunge, lakini ijapokuwa basi uhai wa mtu…” Nadhani unakuwa unaifahamu hiyo video. Anasema “basi uhai ule wa mtu urudi tu nyumbani ukaone ndugu zako, tuachieni huo pia”. Alafu mtu anapotea. Umeona? Kwa hiyo tunaona upande mmoja kwamba nguvu zikihitajika zinatumika, kama tukitaka kukemea jambo tunalifanya. Umeona? Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama tumeona nchi nzima ilifungwa juzi. Umeona? Kimya. Watu wakaambiwa kaeni ndani, wakakaa ndani. Kwa hiyo tuna uwezo. Lakini ikifikia kwenye haya, kimya. Sasa hilo ndio jambo ambalo linanipa mimi simanzi sana. Na hayo matatu ndizo possibilities. Au nikuulize wewe Khalifa, kuna possibility gani ya nne ambayo unaifikiria ah wewe kama mwandishi? Na niulize Watanzania kwa ujumla, kuna possibility gani ingine ya nne ambayo mtu unaweza ukaifikiria, kwamba haya mambo yanatokea na hatuoni nguvu na mipasho ah kama kwenye mingine?

Khalifa Said: Eh, mtazamaji swali hilo limewekwa mezani. Nadhani unaweza kuchangia kwa kutuandikia hapo chini. Nilikuwa nataka kukuambia kwamba Rais lakini amekemea haya matukio. Rais pia alijitokeza tukio la Mzee wako lilipotokea, ah akalaani na akaagiza uchunguzi ambao nataka kuamini kwamba ndio ambao unaendelea kwenye hili swali. Nilikuwa nataka nikuulize pia, lile tukio lililotokea kwa Mzee wako limekubadilisha vipi wewe kama mtu? Limekuwa na athari gani binafsi kwenye maisha yako ya kila siku?

Mohammed Ali Kibao: Hasira dhidi ya vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo nahisi vimemwangusha Mzee Kibao. Mimi nilikuwa neutral. Maswala ya siasa sikuchukua upande mimi. Na ukiangalia katika hata tweet zangu utakuta… na nilisema juzi hapo kuna wakati niliwaambia watu, “acheni upumbavu mnataka kugawanyisha nchi, mnataka…” umeona? Nilikuwa ni mtu wa kuamini kwamba ah… na nilimwambia pia Mzee Kibao, nikamwambia “Bwana mnataka tu CHADEMA wachukue nchi, mtaifanya nini?” Nakumbuka katika mazungumzo yetu nikamwambia hivi, nikiangalia hapo hamna wakati ule wa kina…, nikamwambia sioni mwendeshaji wa serikali hapo. Ndio ulikuwa mtazamo wangu.

Ah mtazamo wangu ilikuwa ni kwamba serikali ya CCM inaweza ikafanya… haifanyi vizuri na inaweza ikafanya mazuri mengi zaidi, lakini nilikuwa ni kwa upande mkubwa nikiamini kwamba ni taasisi CCM ambayo iko well established na ina uzoefu kiasi fulani, na kama wakitaka mabadiliko yanaweza yakafanyika. Umeona? Um sasa ukisema kunibadilisha, kwanza ni hilo la hasira ah dhidi ya wale ambao wanahisi kwamba wamemwangusha Mzee Kibao, hasa vyombo vya ulinzi na usalama. Na sio kwamba… naomba nitofautishe hapa kumdhuru na kumwangusha mtu. Kumwangusha mtu ni kwamba ile ah mategemeo yetu ilikuwa ni kwamba mgelinda maisha ya uhai na usalama wa Tanzania, ambayo kama tunavyojua haikutokea kwa Mzee wetu. Umeona? Ah lakini la pili ni kuniamsha niwe sehemu ya mabadiliko, ili ah yasije yakamtokea haya. Familia nyingine yoyote isipitie haya ambayo tumeyapitia sisi kwa zaidi kwa zaidi ya mwaka mmoja. Na hii naomba niseme kwamba haimaanishi kwamba nataka niwe mwanasiasa au mwanaharakati wa hivi wa vile, kwa sababu kuna mtazamo fulani ukiwa mwanaharakati. Nahisi kuna namna nyingi za kufanya mabadiliko. Mzee Kibao alitupigania sisi tupate elimu ya juu. Alhamdulillah, tumeshukuru tumepata hiyo. Kwa hiyo ni jukumu langu sasa, na nimeamshwa sasa kutumia chochote ambacho ningeweza kwa njia za amani, kwa njia za haki kabisa, kusaidia wengine ambao ah hayajafika haya yasiwafike, na wale ambao wanapitia haya katika nyakati kama hizi vile vile kuongelea kwa niaba yao kwa wale ambao ah wamekosa sauti.

Khalifa Said: Na kwa hiyo unafanya nini exactly? Kwa sababu najua kwamba wewe ni mwanateknolojia na umetengeneza tovuti mbili ambazo mimi nazifahamu. Kuna tovuti moja ya ‘Ijue Historia Yako’ ambayo hii pamoja na mambo mengine unaonyesha matukio mbalimbali ya kihistoria yanayoumba Tanzania kutoka ’61 mpaka 2025. Lakini pia ulikuwa umeanzisha website inaitwa ‘Kumbuko’ (In Memory) ambapo umejaribu kuweka majina na sura za watu mbalimbali ambao wametoweka katika mazingira ya kutatanisha kwa nyakati mbalimbali. Hizi ndizo ambazo jitihada wanazozichukua au kuna nyingine? Na nilikuwa pia nataka kujua nini kiko nyuma ya jitihada zote hizi ambazo unazichukua, especially hizi tovuti mbili ambazo umezianzisha.

Mohammed Ali Kibao: Asante kwa hilo. Sasa tofauti hizo mbili: ya kwanza ni ile ‘Ijue Historia Yako’ kwa sababu kuna mambo ambayo tunapitia sasa hivi Tanzania sio mapya. Umeona? Wala usiangalie mbali. Angalia tu nchi za jirani zilizozunguka. Nchi zote zinaanza uhuru, chama tawala kinaingia, wanashika madaraka, wanaendesha mambo, wanapigania. Nia ipo, nia ni nzuri, alafu tunakuja sasa tuna-introduce demokrasia. Um, tunapitia ni cycle ambayo inajirudia na ukiangalia hata katika ulimwengu kwa ujumla ni cycles ambazo zipo. Kwa hiyo kuna umuhimu wa kujikumbusha ah historia na kukuweka kwenye rekodi. Na ya kwanza hiyo ya ‘Ijue Historia Yako’ ni kujaribu kulinganisha matukio tofauti tofauti ambayo yametufikisha hapa. Moja ambalo tunalisahau sana ni ile Sheria ya Vyombo vya Habari. Nakumbuka kipindi kile watu walipiga sana kelele mitandaoni. Mimi nipo tu. Si unaona yako yanaendelea, shughuli zako wewe kwani yanakuhusu nini? Haya mambo ya… mimi sio mwanahabari. Kwa hiyo kama sheria mpya inapitishwa ya vyombo vya habari inanihusu nini? Umeona? Ndio attitude ambayo ah sikudharau lakini pia sikutilia maanani. Umeona? Sikufuatilia kwa ukaribu. Kwa nini wanahabari wanapigia kelele hii sheria isipite? Umeona? Eh, sikuelewa uzito wake. Lakini ukiangalia sasa nyuma ndio unakuta ah kumbe ndio tumefikishwa hapa. Hizi mabadiliko haya madogo madogo yanatufikisha mahala ambapo mtu mpaka unaogopa hata kusema “jamani mbona mmeua baba yetu?” Au kuna watu siseme mmeua, nikawa kwamba naituhumu serikali au vyombo vya ulinzi na usalama. Hapana, ameuawa. Hilo tunalifahamu it’s a fact kwamba kuna kikundi cha watu kimeua Mzee Kibao. Sasa mtu ameuawa mbona hatuoni? Umeona tumefikiaje hapa? Tumefikiaje hapa? Kuna nchi, tunaishi kwenye nchi ambayo mtu hata kuongea tu kusema “jamani napigania haki” unaogopa. Umeona yaliyotufikisha. Hilo ni moja.

La pili, la ‘Kumbuko’. Ah tunaona watu wanaongelea namba kwa mfano: “Eh watu wameuawa watu 2000.” Na mwingine anasema “Ah wamekufa…” Tunakumbuka kipindi kile Zanzibar “wamekufa watu saba tu”. Umeona? Sasa ukisema wamekufa watu saba tu au wamekufa watu 100 au 2000, unapoteza ule utu na ubinadamu. Umeona? Kwa sababu ni namba. Alafu mara nyingi sisi akili zetu ubongo unashindwa ku-process namba. Mfano nikikuambia wewe Khalifa au mtazamaji utafakari watu 2000 wako kiasi gani, hupati picha. Lakini nikikwambia Mzee Kibao ameuawa, nikikuambia Ben Saanane amepotea, nikikwambia Deus Soka amepotea, nikikwambia Mdude familia yake inamtafuta… Unaelewa kwa kuna umuhimu wa kurejesha ule ubinadamu. Kuna umuhimu wa kuweka rekodi ah na kujua ni watu wangapi na ni kina nani ambao walipotea. Ah hilo ni moja. Lakini pia kuwaenzi kama wanadamu. Mimi nisingependa Mzee Kibao awe ni namba tu kwa sababu kwamba ah kuna watu fulani namba fulani niseme, no, Mzee Kibao. Umeona? Hilo ni hilo. Na jitihada ninazozifanya hizi ni mwanzo. Kuna umuhimu wa sisi kujua ni jinsi gani nchi inaendeshwa. Kuna umuhimu wa kujua ni jinsi gani ambavyo sheria tulizonazo sasa hivi… Kwa mfano nilikuwa nikisikia “No reform no election.” Okay. What do you mean? Umeona? Mpaka kuna siku nikamsikia ah Heche anafafanua anasema “Unajua…” akavunja pale akasema kwamba “bwana unajua sisi tunaishi kwenye nchi ambayo Rais akitangazwa tu na Tume huna namna ya kupinga”. Ah kwa hiyo Tume ikiamka kesho ikitangaza kwamba Khalifa ni Rais, basi ndio Rais, hamna jinsi. Sasa hapo ndio nika… umeona? Kwa hiyo kuna mengi ambayo yanatokea ah ambayo mtu kama unaendesha shughuli zako kawaida unaona unaweza ukahisi hayakuhusu lakini ni muhimu sana kuyajua.

Kwa hiyo la kwanza ni kuenzi na kukumbuka na kurejesha utu na ubinadamu. Umeona? Tusiongelee tu namba. Lakini la pili na jitihada kubwa ambayo naifanya hopefully Mwenyezi Mungu akijalia ah karibuni ni kutengeneza kama ulivyosema mimi ni mwanateknolojia natumia taaluma yangu kutengeneza vifaa ambavyo vitasaidia kuwaelimisha ah Watanzania. Na kama muda ukiruhusu na ukipenda, ningeweza… ninaweza pia kufahamisha initiative ya tatu ambayo Mwenyezi Mungu akijalia Januari tutaianzisha.

Khalifa Said: Ielezee.

Mohammed Ali Kibao: Okay. Ah ya tatu ni ‘Ijue Haki Yako’. ‘Ijue Haki Yako’ haimaanishi kwamba wewe kama Khalifa sasa hivi ujue haki yako. Ni mwamvuli ambao una lengo la kumfahamisha Mtanzania. Kwanza nimefikwa, nimeibiwa mbuzi, nifanyeje? Umeona? Eh nataka niwape watu kifaa ah cha kuweza kuuliza maswali haya madogo madogo ya kila siku yanayohusiana na sheria.

Kilichonipelekea mimi nifanye hivi ni mauaji ya Mzee Kibao yalipotokea. Baada ya kupata confirmation kwamba tumepata mwili baba yenu, tulitafuta sisi sisi ushauri wa kisheria. Hatukutaka kushtaki mtu, sio kwamba tulitaka tushtaki, no. Natafuta tu sasa jamani likitokea hili jambo utaratibu wake unakuwaje? Hakuna mwanasheria ambaye alitaka kugusa hii kesi. Na siwalaumu, siwezi kuwalaumu kwa sababu hofu. Kuna wengine mtu anakwambia “Ya ningependa kukusaidia lakini ah nimepeleka hiyo swala ofisini pale nimeambiwa acha kabisa, acha, achilia mbali”. Kwa hiyo tunaishi katika mazingira hayo. Sasa hilo ni swala ambalo lilipata attention kubwa kitaifa na kimataifa. Sasa fikiria pale Handeni mtu amefikwa na jambo ataanzia wapi? Umeona? Kwa hiyo hatukujua hata tuanzie wapi. Sasa hilo nataka nitengeneze vifaa ambavyo vitasaidia watu kupata ushauri mdogo mdogo tu na kujifunza. Hilo ni moja. La pili ni ah kuwa kutoa vifaa vya uelimisho ah kwa Watanzania. Ni jinsi gani ambavyo sheria zinatengenezwa na jinsi gani ambavyo Watanzania kwa ujumla tunaweza kushiriki katika utengenezaji wa sheria hizi, kama ni kupinga au ku-support. Umeona? Narudia tena ya vyombo vya habari. Sheria ya vyombo vya habari uzito wake hatukuuona. Umeona? Na ukiuliza mtu hata sasa hivi kwamba sheria ilisemaje au kwa nini ilikuwa inapingwa? Mtu bado hatujui, umeona. Katiba kwa mfano, wenyewe tunasikia tu Katiba, kila siku Katiba Mpya, hatujui. Umeona? Wengi hatujui Katiba inasemaje, haki zetu ni nini kikatiba. Na siku zote tunasikia kwamba ukifanya hivi ni uvunjifu wa sheria. Nimeangalia mazungumzo juzi ya wewe na Jebra. Nimejifunza mengi sana kwa kweli na bado kama nchi tuna safari ndefu sana hasa kwenye swala la sheria. Umeona? Amehusia kwa mfano TanzLII, unaweza ukaingia tu pale ukapata hukumu mbalimbali zilizotolewa. Lakini swala la sheria liko kama ni swala ambalo tunalichukulia liko kule mbali na sisi. Na moja ya tatizo ni kwamba kwanza hujui mtu ukazipata wapi hizo sheria kwanza. Mbili, ukishaipata hiyo sheria inakuhusu na tatizo lako, ukianza kuisoma hujui uanzie wapi umalizie wapi. La tatu, nyingi zipo kwa Kiingereza, sasa tuko taifa Kiswahili. Umeona? Kwa hiyo kwa kifupi, kifaa ninachotengeneza sasa hivi na ambacho… nasema tu niko mimi mwenyewe pekee yangu sije nikaambiwa nimepokea pesa za kina Ford. Hapana jamani, ni mimi tu binafsi najitolea muda wangu kutumia taaluma yangu kutengeneza kifaa ambacho um kitawawezesha Watanzania. Kwa upande mmoja tunachukua hizi sheria mbalimbali tunazitafsiri kwa kutumia Artificial Intelligence alafu kwa mfano ukiingia kwenye chatgpt pale unaweza ukauliza maswali tofauti tofauti. Sasa natengeneza chatgpt ambayo inaweza kuwasaidia Watanzania ah kupata majibu mbalimbali kuhusu maswala ya kisheria na vile vile kuwashinikiza au kuwahamasisha watu kufuatilia na kushiriki. Kwa mfano kuna matangazo yametolewa kwamba tuna jambo linajadiliwa, kuna sheria inataka kupitishwa. Uijue inakuhusu vipi wewe binafsi katika maisha na itakuathiri vipi katika maisha yako ya kila siku ikiwa imepitishwa, ili mtu awe na uelewa zaidi kwa wale ambao wangependa. Hilo ndio lengo.

Khalifa Said: Sawasawa. Shukran sana bwana. Sasa tumalizie. Ah tumezungumza mazungumzo mazuri sana. Nilikuwa nataka kukuuliza tukiwa tunaenda kumalizia, unaweza kuisumarize vipi hali yetu sasa hivi kama nchi na upi ungekuwa mkakati wako wa kutoka hapo? Chukulia kwa mfano kama wewe ungekuwa Rais kwenye mamlaka yote ah, ni ipi summary ya nchi yako ya Tanzania hivi sasa hivi na mkakati wako wa kuitoa hapo ulipo unaonekana vipi?

Mohammed Ali Kibao: Kwanza niseme sitaki madaraka yote. Napenda maisha yangu. Alhamdulillah Mwenyezi Mungu amenijalia mtoto, naenda ah panapo majaliwa nirudi kutokujulikana, niishi tu. Napenda hivyo. La kwanza, um kuna siku nikupe hadithi kisa kifupi. Kuna siku tulikuwa tuna kama saa sita hivi usiku tumetoka kijiji kimoja kwenda kijiji kingine na Mzee Kibao tukakwama. Nilikuwa naendesha Suzuki. Sawa? Akaniacha nikakwama kwenye tope bana, unajua njia zetu za vijijini. Basi nikakanyaga mafuta pale na akaniambia “Hebu tulia kwanza, rudi. Rudi nyuma kidogo nenda mbele. Rudi nyuma nenda mbele”. Basi nikaanza rudi nyuma kidogo, unarudi cm moja unaenda mbili. Rudi nyuma, pengo linaongezeka. Tukatoka pale akaniambia “Unajua hili sio somo tu la kutoka kwenye matope. Basi wakati mwingine kwenye maisha pia ukikwama inabidi urudi uchukue hatua nyuma kidogo ili kwenda uchukue hatua”. Nasema hivyo kusema kwamba mabadiliko, kuna njia nyingi za mabadiliko. Tunaona mapinduzi njia mojawapo. Umeona? Sihamasishi chochote, nasema tu. Kuna kupiga kura ni njia nyingine. Umeona? Eh. Um. Lakini hakuna mabadiliko yanayotokea usiku mmoja. Umeona? Hata hapa tulipofika kwenye hali hii tuliyonayo sasa hivi, ni swala ambalo linachukua muda kutufikisha hapa. Kwa hiyo mimi mtazamo wangu ni kwamba inabidi turudi nyuma kidogo, alafu itatuchukua muda.

Mimi na mtazamo wa miaka 10 mpaka 20 kwa kutoa tu vifaa na elimu kukielimisha kizazi kijacho. Ah kwamba mtoto anayezaliwa leo anapofikia umri wa kupiga kura awe ni Mtanzania anayejifahamu. Awe ni Mtanzania anayefahamu historia yake. Awe ni Mtanzania anayeifahamu nchi yake kiundani, nchi inaendeshwa vipi. Tumesoma wote Civics lakini mpaka sasa mtu ukimuuliza hivi eh matawi matatu ya serikali hajui mtu. Umeona? Tunashindwa kueleza, mimi mwenyewe nikiwemo, umeona mmojawapo, nimesoma Civics. Kwa hiyo ni swala ambalo litatubidi turudi nyuma na ni swala ambalo litachukua muda. Na nikisema miaka 20 mtu unaweza ukaona ni mingi sana. Lakini miaka 20 iliyopita tulikuwa… alikuwa ni Kikwete Rais sindio? Sio muda mrefu. Unakumbuka yote ya Kikwete like it was yesterday.

Kwa hiyo hilo ndio lengo langu, na sina lengo la kufanya kazi na sitaki kuwekwa kwenye kundi la wanaharakati. Kuna umuhimu wa kuwa na harakati na kila mwanaharakati wana sehemu yao kubwa na muhimu katika taifa lolote. Umeona? I don’t diminish hizo ah lakini kuna umuhimu pia wa kuelimisha na kuchukua muda kuleta mabadiliko yanayodumu. Kuleta mabadiliko yanayodumu maanake tunaweza tukaleta mabadiliko leo hapa lakini yakawa ni mabadiliko ya muda mchache. Kwa hiyo hilo huu ndio mtazamo wangu na na nia yangu inshallah.

Khalifa Said: Sawasawa. Sasa hapo tumeelezea vitu vingi, unafanya vitu vingi na unapanga kufanya vitu vingi pia. Na nilikuwa nataka kumalizia na hili swali: Ah nini kinakupa ari ya kufanya yote haya? Nini msukumo? Hususan ukizingatia kama ambavyo tumejadili kulingana na mazingira yalivyo sasa hivi, vitu vyote vinaweza kufanyika katika mazingira ambayo ni ya hatari sana kwako wewe binafsi lakini na kwa wale walio karibu na wewe. Kwa nini haya mapambano ni muhimu? Kwa nini haya mapambano lazima yaendelee hata kama kuna hizi hatari ambazo utapaswa kukabiliana nazo?

Mohammed Ali Kibao: Nirudie tena, sijitoi mhanga. Ah nina hofu na ningependa kuishi maisha ya amani. Lakini pia nadhani kuna wengi ambao wanaishi sasa hivi katika hofu na wangependa vile vile kuishi katika maisha ya amani ambao hawana sauti. Kwa hiyo mimi namshukuru kwanza Mwenyezi Mungu kwa kumjalia Mzee Kibao fursa, uwezo na maono ya kutupa elimu. Umeona? Na ukishakuwa umejaliwa kuelimika kwa sababu mimi kuelimika kwangu kuna watu wengi ambao wali-sacrifice vile vile katika kumsaidia Mzee Kibao kuweza kutuelimisha. Sindio? Ah wangekuwa wabinafsi nisingekuwa hapa leo. Umeona? Mzee Kibao angekuwa mbinafsi nisingekuwa hapa leo. Kwa hiyo tuna jukumu la kulipa zile fadhila za wengine ambazo zimetusaidia kufika hapa tulipo na kuwasaidia wengine ambao wako nyuma yetu pengine. Ah ari na msukumo ah kama nilivyosema awali, kwamba hii ni njia yangu ya kuomboleza na kumuenzi Mzee Kibao na kumkumbuka na kumshukuru kwa yote ambayo alitusaidia. Lakini vile vile mimi nina watoto. Ningependa wanangu wawe ah na na uwezo wa wa kuingia wakati wowote na kutoka nchini bila ya hofu ah kwa sababu tu labda baba yao au mtu yeyote ambaye babake anahusika na maswala ya kisiasa basi asiishi kwa hofu. Umeona? Kama ambavyo tunayapitia. Si tunaona kwamba nina jukumu, na sikupewa fursa ambayo ninayo sasa hivi katika maisha ili tu basi niile vizuri umeona na nilale vizuri kwa usalama. Tuna jukumu la kusaidiana wote kama Watanzania, na kila mmoja kwa nafasi yake.

Mimi natumia tu nafasi yangu na inshallah Mwenyezi Mungu akijalia basi hopefully, na kwa msaada wa wengine ambao ni mwanasheria kama hivi na mazungumzo tunayoongea na wewe unapitia kama mwanahabari ni ngumu lakini kazi unaifanya, umeona, naelewa mazingira ambayo wanahabari sasa hivi wanafanya kazi nchini na nadhani serikali pia inaelewa ugumu ambao upo katika waandishi wa habari na vyombo vya habari kwa ujumla. Lakini sote na yeyote anayeangalia hapa ningependa tu kuhimiza kwamba sio lazima uwe mitandaoni, sio lazima mtu upige kelele. Kila mmoja naamini katika nafasi yake, kila mmoja wetu tuna uwezo na tuna jukumu la kutengeneza nchi ambayo tungeipenda tuione. Kwa sababu kama tusivyofanya hivyo, tutatengenezewa na wengine kwa maslahi yao wenyewe. Umeona? Tunajukumu sisi la kuwawajibisha viongozi wetu. Ah tunajukumu sisi la kupigania yale ambayo tunahisi kwamba wakati mwingine sio haki. Tunajukumu, tunajukumu hilo sote. Kwa hiyo msukumo ni huo tu wala wakati mwingine huhitaji msukumo. Na kama inafikia mtu mpaka unauliwa baba yako kinyama kiasi hichi na bado umekaa kimya basi ujue tatizo kubwa zaidi.

Khalifa Said: Asante sana Brother Mohammed. Nakushukuru sana kwa muda wako na utayari wako wa kuja kubadilishana mawazo na sisi. Ah kwa niaba ya hadhira yetu hapa The Chanzo tunakushukuru sana.

Mohammed Ali Kibao: Asante sana kwa kunipa nafasi na nadhani sijawahi kuongelea kwa kirefu kama nilivyoongelea hapa mengi. Ah na hopefully itasaidia na kuamsha japo Mtanzania mmoja. Na narudia tena jamani, sidhani kama kuna yeyote ambaye yupo katika mbele ya kamera na nyuma ya kamera hapa ambaye anataka machafuko nchini, ambaye anataka nchi iharibike. Mimi nchi ikichafuka, mchele ukipanda, hela nayomtumia mama inabidi inaongezeke pia. Kwa hiyo inatuathiri kila mtu kwa nafasi yake. Hakuna, sidhani kama kuna yeyote anayetaka machafuko. Tunataka haki, tunataka upendo, amani na uhuru vile vile wa kuishi na uhuru kimawazo. Kwa hiyo asante Bwana Khalifa kwa jitihada zako zote na asante kwa timu ya The Chanzo hapo, Shafii na wengine mlioko nyuma ya kamera kwenye editing. Asanteni sana kwa jitihada zote mnazozifanya.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×