The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Mwanaharakati Godlisten Malisa Aachiliwa kwa Dhamana, Asema Hajachunguzwa kwa Tuhuma Zozote

Amesema hajaandika maelezo yanayohusu tuhama za jinai

subscribe to our newsletter!

Dodoma– Mwanaharakati Godlisten Malisa na Mkurugenzi Mtendaji wa Gifted Heart Foundation amekanusha taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha kuwa amechunguzwa kutokana na tuhuma za jinai zilizokuwa zinachunguzwa dhidi yake.

Agosti 31, 2026 Wakili Dickson Matata alitoa taarifa ya kushikiliwa kwa Godlisten Malisa, baada ya kuwasili katika mpaka wa Namanga alipokuwa akirejea nchini kutoka Marekani kupitia Nairobi Kenya.

Kulingana na taarifa iliyotolea leo na Jeshi la Polisi inaeleza kuwa baada ya mahojiano wameachiwa kwa dhamana wakisubiri taratibu zingine za kisheria kukamilishwa. Akiongea na waandishi wa habari leo Malisa amesema, hawajaachiwa kwa dhamana kama inavyoeleza taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani Arusha.

“Wametuachia huru, kwa sababu sijadhaminiwa wala sijajidhamini. Lakini jambo la pili sijachunguzwa kwa tuhuma zozote za jinai. Sijaandika maelezo yoyote yanayohusiana na tuhuma zozote za jinai,” amesema Malisa wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuachiliwa leo.

Amesema kilichofanyiwa aliambiwa aandike historia ya namna alivyokamatwa katika mpaka wa Namanga.

“Ndicho ambacho nimeandika, kwamba tulikamatwaje tukafikishwa pale. Hawajanituhumu kwa chochote hawajanihoji kwa chochote. Wala hawajanitajia tuhuma ambazo zimewahi kunikabili zamani. Nimeachiwa huru na kila kitu changu nimerudishiwa simu na fedha na kila kitu na mabegi.”

Kabla ya kuachiliwa kwa Malisa wadau wa haki za binadamu, walitoa wito kwa Jeshil Polisi kutoa taarifa kuhusu mahali anakoshikiliwa Godlisten Malisa kwa kuwa hakukuwa na taarifa inayoonesha ameshikiliwa kituo gani cha Polisi.

Katika taarifa iliyotolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu THRDC Agosti 31, 2026, ilitoa wito kwa Jeshi la Polisi na Idara ya Uhamiaji kutoa mara moja taarifa rasmi kuhusu mahali Malisa anaposhikiliwa.

“Mamlaka ihakikishe zihakikishe usalama wake na zimwezeshe kuwasiliana na familia yake pamoja na kuonana na mawakili wake bila kuzuizi,” ikieleza taarifa hiyo iliyotolewa na Wakili Onesmo Olengurumwa Mratibu wa kitaifa wa mtandao huo.

Malisa ameweka wazi kuwa, baada ya kukamatwa na watu waliojitambulisha kuwa ni Polisi, waliewaeleza kuwa wanawapeleka katika kituo cha Polisi Longido na haikuwa kweli.

“lakini hawakutupeleka kituo cha Polisi Longido. tukapelekwa mahali ambako tulikuja kupafahamu baadae kwamba ni kituo cha diplomasia na utalii. Jumla ya askari Polisi walikuwa watano.”

Jackline Kuwanda ni mwandishi wa habari wa The Chanzo anapatikana mkoanni Dodoma. Unaweza kumpata kupitia jaquelinevictor88@gmail.com

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×