The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Dr John Pombe Magufuli, Raisi Wa Tanzania Amefariki Dunia

Dr John Pombe Magufuli, Raisi Wa Tanzania Amefariki Dunia

subscribe to our newsletter!

Dk John Magufuli, Rais wa Serikali ya awamu ya tano, amefariki dunia jana Jumatano, Machi 17, 2021, katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya moyo yaliyokuwa yakimsumbua, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza.

Akiongea na televisheni ya habari ya taifa, Makamu wa Raisi, Samia Suluhu Hassan alithibitisha na kutangaza siku kumi na nne za maombolezo

“Kwa masikitiko makubwa nawajulisha kuwa leo tarehe 17 Machi mwaka huu 2021 majira ya saa kumi na mbili jioni tumempoteza kiongozi huyu Raisi wa  Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mheshimiwa Dr John Pombe Joseph Magufuli ambaye amefariki kwa maradhi ya moyo katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam”

Kwa mujibu wa Suluhu, Rais Magufuli alilazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) mnamo Machi 6, 2021, akisumbuliwa na tatizo la moyo la mfumo wa umeme, tatizo ambalo limekuwa likimsumbua Rais Magufuli kwa kipindi cha takriban miaka 10. Alitolewa Machi 7, 2021, kuendelea na majukumu yake, Suluhu aliongeza.

“Machi 14, 2021, [Rais Magufuli] alijisikia vibaya na akakimbizwa hospitali ya Mzena ambapo aliendelea na matibabu chini ya uangalizi wa madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete hadi umauti ulipomkuta,” aliongeza Makamu wa Rais Suluhu kwa sauti iliyojaa huzuni na simanzi.

“Mipango ya mazishi inafanywa na mtajulishwa. Nchi yetu itakuwa katika kipindi cha maombelezo kwa siku 14 na bendera zitapepea nusu mlingoti.”

Akiwa amechaguliwa Rais wa Tanzania kwa mara ya kwanza mwaka 2015, Rais Magufuli amekuwa Rais wa kwanza kufariki akiwa madarakani katika historia ya Tanzania.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *