The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Namna Sita Mzazi Anavyoweza Kuhakikisha Malezi Bora Kwa Mtoto

Hakuna mfumo maalum katika malezi ya watoto ila familia na jamii nzima ina jukumu kubwa katika malezi ya watoto, ikiwemo kuwalea kwa mapenzi makubwa.

subscribe to our newsletter!

Kuna usemi wa Kiafrika usemao, inachukua kijiji kizima katika malezi ya mtoto. Usemi huu unamaanisha kuwa malezi ya watoto yanahamasishwa na familia zao na watu wengine wanaowazunguka.

Hakuna mfumo maalum katika malezi ya watoto ila familia na jamii nzima ina jukumu kubwa katika malezi ya watoto, ikiwemo kuwalea kwa mapenzi makubwa.

Sasa basi, leo tutaangalia mambo sita muhimu katika makuzi ya mtoto ambayo ni upendo wa dhati; mfumo maalum wa maisha na malezi; kumuelewa mtoto; kuwa mfano mzuri wa  kuigwa; changamoto za utoto; na kushirikishwa katika familia.

Upendo wa dhati katika malezi ya mtoto ni muhimu sana. Upendo wa dhati humaanisha kumpenda mtoto pasipo na masharti, kumpenda wakati wote anapokosea na anapofanya vizuri, kumuonya na kumrekebisha kwa upendo ilihali akijua hata kama amekosea anarekebishwa kwa upendo.

Mapenzi kwa mtoto yanajenga uaminifu, misingi mizuri ya uadilifu na heshima. Mapenzi haya yalenge kumjenga mtoto kihisia na kisaikolojia na hii  itafanya kazi ya malezi kuwa rahisi.

SOMA ZAIDI: Kwa Nini Ni Muhimu Kumjengea Mtoto Tabia ya Kujitegemea Mapema

Siku zote jaribu kuwa karibu na mtoto wako; cheza naye inapobidi kucheza naye. Ukaribu wako na mtoto utamsaidia mtoto wako kuwa huru kwako na kuwasiliana na wewe muda wowote anapohitaji msaada wako.

Mfumo maalum wa maisha na malezi hugusa zaidi katika mazingira ambayo mtoto anaweza kukua, kujitambua na kujengewa mfumo mzuri wa tabia na maadili yanayokubalika na jamii nzima.

 

Mara nyingi inakuwa ngumu kumlea mtoto katika tabia fulani kwa sababu anapokua na kuwasiliana na wengine hujifunza kutoka kwao.

Mtoto huweza kujifunza mambo mabaya au mazuri lakini ni jukumu lako kama mzazi, au mlezi, kuhakikisha kuwa mtoto wako anakuwa na mfumo maalum wa maisha na malezi; siyo leo umesema hiki, kesho unasema kinyume na ulichoelekeza jana.

SOMA ZAIDI: Watoto Wanaoangalia Sana TV Wanaweza Kuharibu Miundo ya Ubongo

Siku zote, kama mlezi, jaribu kumuelewa mtoto. Elewa hisia zake, mawazo yake, juhudi zake yeye kama mtoto, msifu akifanya vizuri, mpongeze hata kwa kumkumbatia na kumshika mkono.

Watoto wanaopongezwa na kusikilizwa kwa makini hujenga kujiamini na kuthubutu kufanya mambo na kufanya vizuri zaidi katika maisha ya kawaida na masomo yao.

Watoto wanapojua kuwa familia zao zinawakubali na kuwaelewa huwajengea uwezo mkubwa wa kufanya vizuri zaidi.

Mzazi, au mlezi, kuwa mfano mzuri wa kuigwa inamaanisha kuwa watoto hujifunza kwa kuangalia watu wazima wanaowazunguka na huweza kujifunza mabaya au mazuri. Sasa basi, wewe kama mzazi, au mlezi, ni jukumu lako kuwa mfano mzuri wa kuigwa.

SOMA ZAIDI: Kwa Nini Ni Muhimu Mzazi Kumuomba Mtoto Wake Msamaha?

Siku zote jua kuwa wewe ni mwalimu wa kwanza kwa mtoto wako. Atajifunza kwako namna ya kuwasiliana na watu, namna ya kukabiliana na changamoto na kuzitatua. Umewahi kujiuliza mawasiliano yako na wengine yakoje?

Je, wewe ni mtu wa kugombana na watu hovyo hovyo hata kwa makosa madogo? Unatatuaje matatizo ya kila siku ya kifamilia? Yote haya mtoto huangalia na kujifunza kwako.

Tabia kama za ulevi, matusi na ugomvi huwafanya watoto wajue kuwa huo ndiyo mfumo wa maisha. Hivyo, kama mzazi, jifunze kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa mtoto wako na hata kwa wanaokuzunguka.

Kila umri wa makuzi ya mtoto una changamoto zake kwa mtoto mwenyewe na hata kwa mzazi.

SOMA ZAIDI: Fahamu Kwa Nini Watoto Wachanga Hucheua

Kila hatua ya umri mtoto apitiayo inamfunza masuala mbalimbali katika jamii, kuimarisha uwezo wao wa kutatua matatizo au changamoto zinazowakabili na changamoto hizi zisipokabiliwa zinaweza kuharibu mfumo mzima wa makuzi ya mtoto na hata  wa familia nzima.

Kama mzazi, ni vizuri ukampa mtoto nafasi ya kuweza kukabiliana na changamoto.

Kushirikishwa katika familia ni kuhakikisha mtoto anashiriki kikamilifu katika maamuzi ya kifamilia na hasa mambo yanayogusa maslahi yake binafsi, hata majukumu madogomadogo ya kila siku.

Hii humpa mtoto hisia za kuwa ana familia inayomkubali na kumtegemea, humpa mtoto nafasi ya kujiamini na kushiriki katika mambo mbalimbali ya jamii na kifamilia, humfanya achukue majukumu katika familia na pia kuwajengea uwezo wa kujitegemea.

Makala hizi za malezi huandaliwa na C-Sema, shirika lisilo la kiserikali linalojikita katika kuendeleza na kulinda haki za watoto Tanzania. Kwa maoni na ushauri, wapigie kwenye simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile, unaweza kuwapata kupitia kurasa za Facebook: Sema Tanzania, Twitter: @SemaTanzania, na kupitia barua pepe yao www.sematanzania.org.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *