The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Uchambuzi: Bajeti ya Wizara Ya Nishati 2024/25 Ni Ndogo Zaidi Kutokea Katika Kipindi Cha Miaka Mitano. Hiki Ndicho Kilichosababisha

Moja ya jambo ambalo linaonekana katika bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2024/25 ni kuwa bajeti hii imepungua kwa kiasi kikubwa, kwa takribani asilimia 38, hii ikiwa ni baada ya miaka minne ya bajeti kuongezeka. 

subscribe to our newsletter!

April 25, 2024, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2024/25, bajeti ya jumla ya shilingi Trilioni moja na bilioni mia nane (1,883,759,455,000). Bajeti hii inachukua takribani  asilimia 3.8 katika bajeti nzima ya Serikali kwa mwaka 2024/25.

Moja ya jambo ambalo linaonekana katika bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2024/25 ni kuwa bajeti hii imepungua kwa kiasi kikubwa, kwa takribani asilimia 38, hii ikiwa ni baada ya miaka minne ya bajeti kuongezeka. 

Sababu kubwa zilizoelezwa juu punguzo hili ni pamoja na kukamilika kwa mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere kwa ajili ya kuzalisha nishati ya umeme, lakini pili Serikali kuamua kupunguza bajeti kwa kuweka ukomo wa bajeti kuwa Trilioni 1.8.

Uchambuzi wa bajeti ya Wizara ya Nishati

Tumefanya uchambuzi wa bajeti hii kwa kuangalia maeneo mbalimbali ikiwemo mwenendo wa bajeti na vipaumbele vyake pamoja na utoaji fedha. Uchambuzi wetu, unatoa alama katika vipengele mbalimbali vya bajeti kwa madaraja matatu; A ikionesha inaridhisha, B inaridhisha ingawa ina changamoto na C ina changamoto  za msingi.

Kwa ujumla bajeti hii tunaipa alama A katika kuangalia mlolongo wa namna Serikali imekuwa ikitoa fedha, ambapo wastani wa miaka mitatu yenye taarifa ambazo zimekamilika yaani 2020/21 mpaka 2022/23 ni asilimia 89. 

Hii ikimaanisha sehemu kubwa ya fedha zilitolewa, huku mwaka 2021/22, fedha zikitolewa zaidi ya bajeti. Huu ni mwaka ambapo Serikali ilipata mkopo kutoka Shirika la Fedha Duniani kukabiliana na athari za Uviko-19.

Eneo la pili la utoaji wa taarifa wa bajeti, eneo hili tunalipa alama B, ikimaanisha ingawa taarifa zinaridhisha, bajeti ingeweza kuboresha maeneo kadhaa. Mfano wa maeneo hayo:

  1. Taarifa ya bajeti haijaeleza mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, mradi uliotengewa fedha nyingi zaidi ulitumia kiasi gani mpaka kufikia wakati wa kutoa taarifa za bajeti. Ingawa taarifa ya bajeti iimeweza kutoa maelezo ya msingi juu ya maendeleo ya mradi, kiasi cha fedha kilicholipwa katika mwaka wa bajeti kingetoa mrejesho kamili.
  2. Taarifa ya bajeti imeonesha miradi ambayo kwa ujumla wake inazidi zaidi ya Trilioni 3, ingawa kiuhalisia fedha za bajeti ni Trilioni 1.8. Inaeleweka kuwa baadhi ya miradi hufanyika zaidi ya mwaka mmoja wa fedha, taarifa hii haijaweza kufafanua vya kutosha na kwa urahisi kwa wasomaji wote kuelewa.
  3. Taarifa ya bajeti haijaeleza kuhusu miradi ambayo serikali imeiacha. Moja ya mradi ambao ulikuwepo katika mwaka wa fedha 2023/24 ni mradi wa Project Mawe, katika mradi huu serikali ilitegemea kununua mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi wa takribani Megawati 150 katika eneo la Tegeta. TANESCO ilipata kibali cha kutumia fedha za mkopo wa  Bilioni 303 kutoka Benki ya Biashara (NBC) kwa ajili ya mradi huu. Kwa mujibu wa ripoti ya CAG mradi huu serikali imeuacha kutokana na kuwa hautekelezeki. Taarifa ya bajeti ingeeleza kuhusu mradi huu, hasa kwa kuwa Ilikua sehemu ya utekelezaji wa mwaka 2023/24 na pia serikali ingeeleze miradi itakayotumika katika fedha hizo za mkopo.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *